Wewe kutokuwa tajiri unamlaumu nani?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Humiliki kiwanda chochote, hakuna bidhaa unayozalisha na kuipelekea nje; wewe kila siku ni kulia lia tu.

Mshahara ukichelewa tu kidogo, unakimbilia kwenye ule uzi pendwa.

Kwa upande wangu, mi nawalaumu wazee wangu walionipa elimu iliyofuta mawazo yangu niliyozaliwa nayo (kipaji), na kubeba mawazo (elimu) ya watu wengine yanayonifanya nifikiri nitakuwa tajiri kwa kuajiriwa miaka yangu yote.

Yaani ni sawa sawa na kompyuta uliokuwa unaitumia mwanzoni, kutoa ''hard disk'' ya zamani na kuiwekea ''hard disk'' nyingine yenye uwezo mdogo.

Nina ndoto za kuja kuwa mwekezaji wa uchimbaji wa visima vya mafuta huko mashariki ya mbali, je nitafanikiwa? ingawa sasa na miaka 77.

Je wewe unamlaumu nani, aliyekufanya usiwe tajiri?​
 
Sina mtu wa kumlaumu na huo muda wenyewe sina. Kila siku ni mpya na kila siku ina jambo jipya, kulaumu ni kuendelea kuishi wakat uliopita, unatakiwa kuishi leo, maana leo sio jana, leo inafursa mpya ambazo pengine jana hazikuwepo.
 
Sina mtu wa kumlaumu na huo muda wenyewe sina. Kila siku ni mpya na kila siku ina jambo jipya, kulaumu ni kuendelea kuishi wakat uliopita, unatakiwa kuishi leo, maana leo sio jana, leo inafursa mpya ambazo pengine jana hazikuwepo.
Wanasema ukilaumu, nawe utakuja kulaumiwa na kizazi chako
 
Wasingekupeleka shule ungekuja tena hapa kulia lia kuwalaumu wazazi wako, mtu unapewa elimu lakini hupangiwi utaitumiaje. Elimu haikufanyi wewe uwaze kuajiriwa ni wewe mwenyewe ndo unafikiri ukiwa na elimu unatakiwa uajiriwe
Ova
 
Utafanikiwa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ