Wewe kutokuwa tajiri unamlaumu nani?

Wewe kutokuwa tajiri unamlaumu nani?

Humiliki kiwanda chochote, hakuna bidhaa unayozalisha na kuipelekea nje; wewe kila siku ni kulia lia tu.

Mshahara ukichelewa tu kidogo, unakimbilia kwenye ule uzi pendwa.

Kwa upande wangu, mi nawalaumu wazee wangu walionipa elimu iliyofuta mawazo yangu niliyozaliwa nayo (kipaji), na kubeba mawazo (elimu) ya watu wengine yanayonifanya nifikiri nitakuwa tajiri kwa kuajiriwa miaka yangu yote.

Yaani ni sawa sawa na kompyuta uliokuwa unaitumia mwanzoni, kutoa ''hard disk'' ya zamani na kuiwekea ''hard disk'' nyingine yenye uwezo mdogo.

Nina ndoto za kuja kuwa mwekezaji wa uchimbaji wa visima vya mafuta huko mashariki ya mbali, je nitafanikiwa? ingawa sasa na miaka 77.

Je wewe unamlaumu nani, aliyekufanya usiwe tajiri?​
Mbona kuna wenzio na elimu hio hio wamekuwa matajiri na wana viwanda? Mimi najilaumu mwenyewe. Nimeshindwa mwenyewe tu simlaumu yeyote.
 
Nailaumu serkali sikivu ya CCM iliyotuletea umasikini huu wa kudumu
 
Back
Top Bottom