Ahsante kunifumbua macho ndugu yanguuuu (in sukumas voice) nitajitahidi kuchangamka nao japo kupiga piga dtori za billa msingi naona inaboa. Fanya unipe somo how to detect my crushes
Ha ha! Hata mi mwenyewe nakosaga vitu vya kuzungumza nao ila Kama utakuwa na mazoea nao hutakosa utapata tu mkuu mengine huja hukohuko pasipo fahamika😜
How to detect her it's very easy but it's very hard sometimes kukubali kuwa is she flirting with me 😂😂
Ipo hivi vitu huwa vina uwili mtu akiwa hakupendi au Hana interest na wewe utajua kutokana na vijitabia vyake ila kinyume na hizo tabia inamaana yupo interest nawe! Hiyo ndio point kuu
Mtoto wa kike akikupenda utaona haya
Atataka kuwa karibu nawe kwa maana ya kutaka kuongea nawe,kukaa pembezoni nawe n.k hiyo haitoshi maana hata kikawaida anaweza fanya hivyo but different is here
Mara nyingi utakachoongea hata kama ni cha kipuuzi atakishika! Kituko chako utakacho muambia hata kama hakichekeshi yeye still kitamvunja mbavu.. pia ktk maongezi maswali yake mengi ni yakutaka kukufahamu!
Jambo lako hulishughulikia mapema maana unakipaumbele kwake..
Ukishaanza kuditect vitu vidogo vidogo anza kuangalia her body language akiwa mbele yako!
Miguu yake hupenda kuilekeza kwako maana anataka attention yako kwake Kama ananywele hupenda kuzishikashika hata kama hana sababu ya kufanya hivyo! Pia hupenda kushika shingo yake kumbuka haya huyafanya akiwa hajitambui kama ndio viashiria vyenyewe ni ubongo tu humfanyisha bila kupenda.. chengine akiwa karibu nawe anaweza kukushika kama bahati mbaya coz she wants contact with you.. Kuna kitu kinaitwa macho haya pia ni uchawi mwengine 😂😂😜
Ulishawahi kuwa umekaa umetulia then unageuka nyuma ama pembeni unakuta kitoto cha kike kimekukazia jicho kinakuangalia ila utakapo kutanisha macho tu ye anaondosha anaangalia pembeni..?
Ukiona hili linajirudiarudia hehe sisemi.
Bado tupo kwenye macho hapohapo..
Hili linahitaji utulivu macho ni ishara kubwa Sana kama mtu umempenda maana pindi ukutanapo na umpendae hicho cheusi kwenye jicho nimeisahau sijui ndo pupils!! Huongezeka ukubwa!!
Sasa hapa unatakiwa ujue akiwa kawaida kanakuwaje na akikutana nawe kanakuwaje..
Chengine cha kuangalia ni marafiki za huyo unaeshuku anakupenda wanawake hupenda kuwaambia rafiki zao hisia zao so pindi unapotokea kwa rafiki zake how they react..??
Hukukaribisha kwa mbwembwe kidogo za kipekee pia sometime hutia kiutani n.k kiufupi utaona care fulani hivi na wengine utakapofika nao huwaachia kiuwazi chenu hivi cha faragha n.k na wengine huenda mbali na kuanza kukuita shem n.k
Mkuu mambo ni mengi unaweza pia tafuta ila njia kuu ni hapo juu na usikariri ambae unagombana nae leo kesho ndo anaweza kuwa wako!
Ukishaona hayo ndugu Kama nawe utakuwa umemkubali be a gentleman..
Anza kumjali ajisikie huru nawe,atakapokwama mkwamue haijalishi ni kwa hela au vipi kwake hata kitu kidogo tu ukimtendea jua kikubwa kwake! So hapo unaanza kumteka zaidi chengine huwa wanauzika kukuona upo interest na wanawake wengine so Kama umemkubali care about her but be normal usizidi Sanaa ili uendelee kuweka shauku kwake zaidi kuwa normal tu asije akajiona hakufai..
Kwa hayo machache nafikiri utapata kitu.