Waungwana waliolelewa na kufundwa heshima nzuri, huwa hawahadithii mambo yao ya faragha waliyofanya na wanawake.
Kwa sababu mambo hayo ni ya faragha.
Kwa sababu wameyafanya katika uwili wao, hayakuwa kwa faida ya jamii kujua kwa kuhadithia mitandaoni.
Kwa sababu kuhadithia ni kujivua nguo mwenyewe.
Kwa sababu kuhadithia kunaweza kumdhalilisha mwanamke.
Kwa sababu kuhadithia kunaweza kuhalalisha na kuchochea ngono zembe.
Lakini, inawezekana hayo ni maoni ya zama zetu tuliosoma vitabu vya Sheikh Shaaban Robert na kujua uungwana ni nini.
Na labda watoto wa zama za mitandao wanakuja na fikira tofauti.
Sent from my typewriter using Tapatalk