Wewe ni mhenga?

Wewe ni mhenga?

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
33,894
Reaction score
76,810
-Kama unapigiwa simu unainyanyua juu kisha unauliza nani huyu tena anapiga! Wewe ni mhenga

-Kama ulitumia mafuta ya kimbo ya kopo la chuma wewe ni mhenga ndugu yangu.

-Lingine kama ulioga kwenye bafu lenye mlango wa gunia huku unatoka kwa kukanyagia visigino usichafuke...wewe pia ni mhenga tena mhenga kweli.
 
Kama wewe ulipigwa picha ukaisubiri kwenda kisafishwa kwa miezi mitatu ikaja imeungua ndugu yangu wewe ni mhenga.
Tena kwa muda huo unaifuata unaambiwa bado haijasafishwa
 
Hahaha.

Kama wewe umetumia sabuni ya Komoa na mafuta ya Yolinda kaka wewe mhenga.

Acha kuvaa mlegezo kabisa.
Kama wewe ulikuwa unajipaka mafuta kula/ng'ombe/samli, wewe ni muhenga
 
Hahaha..

Bwana tena mapozi ya kwenye maua ya zahanati au shule.....
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Siku ya kupiga picha, mpiga picha anaenda kuitwa kijiji cha jirani unaendesha baiskeli ikiwa na tairi kipara, haina raba za pedeli, umevaa viatu vya matairi, haina breki, breki uikaba tairi la nyuma au mbele kwa mguu, kengele hamna unatumia mluzi..

Wewe ni muhenga uliyebobea..

Ukifika nyumbani kwa mpiga picha, unakuta hayupo[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Wakati huo huku nyumbani watu wanaoga wavae nguo nzuri maalum kwa matukio maalum, tayari kwa kupigwa picha, Wewe ni Muhenga mwenye PhD ya Uhenga..
 
Kama ulikuwa unazungusha cassete na peni wewe ni muhenga

Kama ulikuwa unakula gud gud chocolate wewe ni muhenga

Kama ulikuwa unachana nywele na chanuo la chuma unalipitisha kwny moto wewe ni muhenga

Kama ulikuwa unaweka vimstari kwny shati la shule ukipiga pasi wewe ni muhenga

Kama ulikuwa unavaa raba za dingi hana uwezo ( dhl) shuleni wewe ni muhenga

Kama ulikuwa unapenda matandu na ukoko unayaloweka na mchuzi viloane ndo ule wewe ni muhenga

Kama ulikuwa jnakisubiria kipindi cha mama na mwana redio tanzania wewe ni muhenga hama kwenu kajitegemee
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Siku ya kupiga picha, mpiga picha anaenda kuitwa kijiji cha jirani unaendesha baiskeli ikiwa na tairi kipara, haina raba za pedeli, umevaa viatu vya matairi, haina breki, breki uikaba tairi la nyuma au mbele kwa mguu, kengele hamna unatumia mluzi..

Wewe ni muhenga uliyebobea..

Ukifika nyumbani kwa mpiga picha, unakuta hayupo[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Wakati huo huku nyumbani watu wanaoga wavae nguo nzuri maalum kwa matukio maalum, tayari kwa kupigwa picha, Wewe ni Muhenga mwenye PhD ya Uhenga..
Hahaha.

Kama ulinunua nyama kwa viungo wewe ni mhenga.

Unauziwa mguu, mkono, mbavu wewe mi mhenga.
 
Back
Top Bottom