What a blow! What a shame! Ni aibu gani hii..?

JIFUNZENI KWA MADULO

Mwl. John Pambalu

Alipokuwa kileleni, Madulo alijiona alfa na omega. Kauli zake zilijaa kiburi: “Sisi ni taifa huru, hatupangiwi,” “wanatuchukia kwa sababu ya mafuta,” na “wakosoaji wanalipwa na mabeberu.”

Ukosoaji ulipoongezeka, lawama zilipelekwa nj kwa maadui wa kufikirika, wakati mateso halisi yalitendeka ndani.

Utawala wake uliishi kwa hofu: utekaji, mauaji, ufisadi na matumizi ya nguvu kupita kiasi. Alipewa sifa na wapambe, akasifiwa na viongozi wa dini waliogeuka wasifiaji badala ya sauti ya ukweli. Wananchi walilazimishwa kushangilia; wengine wakasombwa kwenye maroli kuonesha “uungwaji mkono.”

Leo simulizi inageuka. Madulo ametekwa na nguvu zilezile alizozitumia huku mamilioni ya wananchi wake wako barabarani wakisherehekea, si kwa chuki bali kwa hisia ya ukombozi.

Huu ndiyo mwisho wa kiburi: pale sauti ya wananchi inapovunja ukuta wa propaganda.
Funzo ni moja: viburi vina mwisho. Hakuna mtawala aliye juu ya haki, wala aliye salama dhidi ya siku ya kuwajibishwa. Ukimya wa ukweli haufi. huchelewa tu.

Wasalaam
John Pambalu
jpambalu@gmail.com
 

Bwana Thadei Kweka aliyeshirikiwa na Jeshi la Polisi, aliomba msaada kupitia ubalozi wa Marekani Tanzania, wakampelekea fomu asaini ili apate huo msaada kutoka Serikali ya Marekani, Jeshi la Polisi awali lilimgomea lakini tukio la leo la Maduro iliwafanya waruhusu asaini hizo fomu za Ubalozi wa Marekani na kumuachia huru na kumfutia mashitaka na Sasa yupo huru kama raia Mwema katika nchi hii. Sijawahi ona mtuhumiwa anapewa hukumu ya kuachiwa weekend wakati mahakama hazifanyi kazi weekends. Hii ni maajabu
 
Rekodi mpya kabisa 2026😂😂😂
 
Huyu kakosa hiyo bahati

TAARIFA KUTOKA FAMILIA YA CLEMENT MWANDAMBO

"Jeshi la Polisi Mbeya lilimkamata kaka yetu Clemence Mwandambo tarehe 29. 12. 2025 alipokuwa ameenda kuripoti na wakakiri kwamba wanamshikilia Katika kituo cha polisi kikuu Mbeya

Kaka yetu alitakiwa awe anaripoti kila Jumatatu alipofika wakamkamata

Familia tulipoenda kumpelekea Chakula wakasema hayupo na hawajui alipo, baada ya siku Kadhaa kama familia tukaendelea kifuatilia tukagundua yupo Kituo cha Polisi Inyala Jijini Mbeya.

Tulipoenda Inyala tulimpelekea chakula hawakutana tumuone wakasema yupo ila hatutakiwi kumuona baada ya kweli baada ya Muda ikaja gari landCruza ikiwa na Tinted ikamchukua mzee wetu kwa macho yetu tunaona ikaelekea uelekeo njia ya kwenda Iringa.

Baada ya hapo hatujawahi kumuona tena ndugu yetu hatujui anakula nini? Kama anamakosa apelekwe mahakamni kwanini hawataki kumpeleka mahakamani kama shwria inavyotaka? Hatujui ni mzima au wamemuua kama wamemuua watupe maiti yetu tukazike.

Sisi kama familia tunalitaka jeshi la Polisi liseme alipo ndugu yetu.”
 
Fi
Fomu alisaini kabla ya tukio la Venezuela, ila kaachiliwa baada ya tukio la Venezuela
 
Wale watu form zao unazijua zilivyo ngumu, kila kipengele kina "If YES, explain why with full, valid, and legal evidence?" "If No Skip"...
Unadhani hapo watajaza nini zaidi ya "No" zote na mwisho kusign hakuna kesi...



Cc: Mahondaw
 
Democratic Country.
 

Attachments

  • d8962308dfbe47f48115ac708cc0851f.mp4
    14.8 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…