Steve D na wengine wamezungumzia utamaduni wetu. Hiyo mimi nakubaliana nayo maana utamaduni ni dynamic na si static. Huu tunaouita utamaduni wetu kwa sehemu kubwa umechangiwa na mtazamo wa dini tulizoletewa( uvaaji wa nguo fupi kwa mfano) na fikra nyingine geni. Hao wazungu ni hivi karibuni (kihistoria) walikuwa wakitupa kinyesi kwenye barabara. Walikuwa hawaogi na waliamini kuwa maradhi mengi yanatokana na pepo chafu. Hawa walikuwa wananyongana hadharani na waliamini kwa dhati kuwa wao wameletwa hapa duniani kuwakomboa wengine. Mengi ya haya hawayafanyi sasa. Ninachowapinga wakina Nyani Nguba ni pale wanapo'imply' kuwa sisi ndivyo ytulivyo genetically, kwamba hatuna jinsi ya kujibadili. Ndiyo maana mmoja wetu akatufananisha na nyani maana hata ufanye nini nyani atabaki nyani tuu. Nyani angesema "huu ni utamaduni wetu" nisingempinga.
Mfano uliotolewa wa viwanda vya korosho ni mfano mzuri lakini si pengine kama ilivyotarajiwa. Ushauri wa kuanzisha viwanda vya korosho ulitoka World Bank. Tanzania wakati ule ilikuwa na surplus kubwa (amini usiamini) na sehemu moja ya kuwekeza ikaonekana ndiyo hapo. Walichosahau ni kuwa soko letu kubwa lilikuwa India ambao wao walikuwa hawana interest na kununua processed products kutoka kwetu kwa maana wanaviwanda vyao. Wao wakaendeleza mashamba yao Goa na kununua raw cashew kutoka sehemu nyingine. Tukakosa soko hata kabla ya kuanza kuzalisha! ni maamuzi kama haya yakitegemea ushauri wa watu ambao ukweli hawana uchungu sana na sisi ndio uliochangia kutufikisha hapa.
Tulijengewa Mbegani Fisheries Institute huko Bagamoyo na watu wa Norway. Chuo kizuri sana lakini kililenga kwenye uvuvi wa trawlers ambazo wao wamezizoea. Sisi uwezo wetu ni ngalawa. Walipoondoka chuo kimebaki kuwa kambi ya mazoezi ya timu za mpira. Malengo yake hayakuzingatia hali halisi ya watanzania na si kwa sababu watanzania ndivyo walivyo! Wangeangalia namna gani ya kuboresha hizo ngalawa au kuwawezesha hao wavuvi wadogo wadogo namna ya kumudu hizo trawlers pengine hadi leo kingeendelea kupeta.
Tumekuwa kichwa cha mwenda wazimu, kila kukichwa tunamtafuta nani aje kutunasua. Kuna thread humu inazungumzia jinsi serikali ilivyodharau ushauri wa idara ya hali ya hewa kuhusiana na ukame uliotukumba hivi karibuni. Hatukutaka kuwasikia hawa wataalamu wetu. the rest is history. Tunakumbuka pale wataalamu wa tanesco walipoagizwa waendelee kuzalisha umeme hata pale maji yalipofika critical point! Mifano ni mingi. Lakini hizi zote ni tamaduni na zinaweza kubalika.
Nitamalizia kwa kutoa mfano wa nchi mbili za kiafrika, Gabon na Botswana. hizi zote zimejaliwa utajiri mkubwa wa rasilimali, moja mafuta mwingine almasi. Gabon wamejenga Libreville kuwa mji wa kisasa na huduma zote zinazopatikana ulaya. Wanasema mafuta ya manukato, mavazi ya bei mbaya vyote vinapatikana hapo. wote tunajua vituko vya rais wao, mabling bling n.k. lakini wananchi wake wengi bado wanaadhirika. Wanaokota makombo dampo. Sasa mafuta yao yanaelekea ukingoni hawajui watafanya nini. Ukiangalia Botswana hadithi ni tofauti. wao utajiri wao wamewekeza kiasi cha kuifanya ni moja ya nchi zilizopata maendeleo ya kasi DUNIANI. Hatuwasikii wakitamba. Rais wao hakuwa na makuu. Wote hawa ni waafrika. Tamaduni tofauti lakini ni waafrika. Ni sisi wenyewe kutafuta viongozi wenye mapenzi, uchungu na upeo wa kuona mbali ili watuongoze kutoka katika hali hii tuliyonao. Viongozi watakaoiangalia hali yetu na kutupa mipango inayoendana nayo, kutumia rasilimali yote tuliyojaaliwa (utaalamu, madini, ngoma n.k) katika jitihada za kujikwamua. hao wanaotoka nje waje kutusaidia lakini mwelekeo tuutoe sisi wenyewe.
Aluta Continua.