Just venting, Mkuu Bin Maryam, just venting! Chagua unapotaka mengine dharau!
Nilikuwa nafuatilia posti zako. Nimekuelewa msimamo wako na samahani kwa kutokutendea haki.
Nadhani moja ya sababu ya kutumia wataalamu wa nyumbani ni kupunguza gharama. Kuna kipindi nadhani wataalamu kutoka nje walikuwa wanachukua sehemu kubwa ya payroll ya malipo ya mishahara ya serikali. Je tumefika wapi?
Vilevile tatizo kubwa linalokuja ni kuwa tunapokea misaada mingi lakini malipo ya mishahara ya consultants na watalaamu kutoka nje inakula sana misaada yenyewe na hivyo kutofikia walenga.
Nilipomaliza masomo yangu nilirudi Tanzania na nikawa natafuta na CV yangu ilijaa masomo niliyosomea. Kwa sababu sikuwa na ku-connection yoyote huko Tanzania niliondoka na kuja Marekani.
Hapa nilihamua kuanza ngazi ya chini kabisa. Lakini uzoefu na mafunzo niliyopata nikiwa kazini ninajua kabisa ninachofanya kina VALUE gani. Na nikihamua kurudi nyumbani ninajua nitakachofanya kitakuwa na mchango gani.
Si kweli kuwa mtu anayemaliza MIT, Havard, Yale, Cambridge atarudi bongo na kufanya kazi vizuri. Mambo mengi ya shule ni historical facts, unapofanya kazi unapata uzoefu. Kwa mfano ukiwa shule, kama wewe unasoma computer science basi mawazo yako yatakuwa huko. Lakini ukiwa kazini unakutana na wachumi ambao wanakupangia bajeti, unakutana na Marketing watakaokupa picha ya kitu wanachouza. Hivyo elimu yako ni sehemu ya Grand scheme of things.
Kama ningepata kazi Tanzania baada ya kumaliza shule, nisingefanya tofauti na wanavyofanya watanzania wengi. Ningetafuta SUV kubwa, nyumba Masaki na mke mzuri.
Kazi zote zinazofanya hapa ni lazima kwanza niwakumbuke kwanza share-holder, Mteja na mwishoni mimi mwenyewe. Share-holder ndiye aliyeweka mtaji wa kuniwezesha mimi kufanya kazi na kulipwa mshahara. Je kazi yangu, itaweza kutoa faida ya kumlipa share-holders? Je kazi ninayofanya inaweza kumfanya mteja atumie pesa zake? Na hivi ndio vitu vilivyonifanya nibadili utamaduni wangu wa kitanzania. Ninapokwenda kazini siendi na kichwa juu kuwa nilipata division one na A ya hesabu, au upper second degree. Nakwenda kazini nikiwa na attitude ya kumaliza kazi zangu katika muda na bajeti inayotakiwa.
Hivyo kusema kuwa wataalamu Tanzania wapo ni kitu kimoja. Lakini mazingira na attitude ya wataalamu hao kuleta mafanikio ni kitu kingine.