What about R&D?..The Case of Foreign Aid Influx & 'A Japanese Expert' Invite

What about R&D?..The Case of Foreign Aid Influx & 'A Japanese Expert' Invite

Mkuu Dsm Mtaalamu aletwe sijapinga kuletwa mtaalamu, Kila nchi hata Japan yenyewe na US ina wataalamu kutoka nnje. Mimi ninachosema ni kuwa, sisi tunawataalamu wa ndani. hawa wataalamu wa ndani tunatakiwa tuwatumie. Tutawatumia je?

Kama tunaleta mtaalamu wa nnje kwa mkataba lets say wa 5 year awe yuko attached na wataalamu wetu wa nndani ili aweze kutransfer knowedge na akiondoka ujuzi ubakie na si akiondoka na mradi unakufa.

Japan wakati inaendelea ilikuwana na sera kama hizi na qute.
"3 Education Policies of Meiji Gvt to Build the Economy"
- Send talented student abroad in the field of Gvt administration, finance, engeneering and industry.
-- Invite foreign professors and technicians to Japan
-- Write text books in japanese by Japanese.
Source: www.nifty.com (Tamagawa University 2006)"

Kutumia au kushirikisha wataalamu wa ndani ni muhimu sana mkuu.
Hii ni muhimu sana mkuu. Mazingira ya Japan na tanzania ni tofauti sana. Akija na utaalamu wake ukawa adoped na mazingira yetu ya ndani hiyo ni nzuri. Ni muhimu na ni vizuri sana wanavyofanya JICA/Japan kwani wanatupa utaalamu napendelea sana watufundishe kuvua samaki na si kutupa samaki mkuu.

Tatizo langu mkuu sio kuwa tusilete wataalamu lakini hii tabia ya kuamini kuwa kila kizuri kinatoka nnje ni soo ipo siku tutaleta raisi mtaalamu kutoka nnje ili aje atuongozee nchi yetu.

Mkuu Mtoto wa Mkulima kama wewe hupingi hilo basi tuko pamoja.
 
Ni viwanda vingapi tulivyovi-taifisha na vikatushinda? hatuwezi, bado.

lakini hivyo hivyo vilivyotushinda sisi tukiwapa wawekezaji vianaendelea.

Elimu si kuta nne tu za darasani.

Juzi tu tumeona siku inafunguliwa kiwanja kipya cha mpira, tulipocheza na Mozambique, tulifanya nini pale kiwanjani?

Dar, kikubwa katika maisha ni maamuzi. If you believe that you cant do... huo ndio mwisho wako. Naamini wapo watanzania wengi wanaoweza ila serikali yetu ina imani kama yako!
 
Mkuu Mtoto wa Mkulima kama wewe hupingi hilo basi tuko pamoja.

Mkuu sipingi ila nasema tuwatumie wataalamu wetu, tutumie taasisi zetu kama SIDO, SUA, DIT, UDS, ESRF, REPOA, VETA etc. Ni muhimu sana kuwatumia wataalamu wetu mkuu.
Kama hatutawatumia watapractice vipi na lini?

Mkuu unajua miradi mingi ya Donors huwa inakufa jamaa wakiondoka kwa sababu wakija wanakuja na wataalamu wao na wakiondoka wanaondoka na utalamu wao. Sasa inabidi iangaliwe upya namna ya kuatach local people na hao wataalamu mkuu wa kutoka nnje otherwise siku zote tutakuwa tegemezi.

Nikupe mfano tuu unajua Tazania tunamakandarasi wengi sana? huwa wanafanya nini? Unakuta kampuni ya china wanakuja hadi na vibarua wakati mwingine wanakuja hata na wafungwa kufanya kazi wakiondoka na mradi umeondoka.

Practice makes perfect.
 
Wakati mwingine nadhani Dar es Salaam unapinga kwa ajili ya kupinga tu. Hapa kinachopingwa ni kile kilichoandikwa kuwa huyu mtaalamu mmoja kutoka Japan ndiye atakayetukwamua katika matatizo yetu na kutufanya nchi inayotegemea viwanda. Hawakusema kuwa huu ni mwanzo wa ushirikiano na serikali ya Japan katika kuikwamua nchi yetu bali huyu Bwana single-handedly ataweza ambacho watanzania karibu milioni 40 wameshindwa! Hivi unaamini kuwa baada ya huyu bwana kuandika ripoti yake ndipo wakina Sony, Toshiba, Toyota watakimbilia kuwekeza nchini mwetu? Nadhani ni Bin Maryam aliyesema kuwa tumeanza kuwa na siasa za mpirani. Nani asiyejua mambo yanayotuzuia kuendelea? Hao washauri wa nje na ndani wamekuwa wakituimbia kila siku lakini hatutaki kusikia. Tunataka njia ya mkato. Mimi ambaye si mtaalamu najua kuwa tunahitaji kuwekeza kwenye vifuatavyo ili kuvutia wawekezaji makini:
a) Kupunguza ukiritimba katika mambo yetu. Hii inajumuisha usiri katika mambo yetu.
b) Kuhakikisha kuwa elimu ya msingi tunayotoa inaendana na mahitaji ya sasa hivi. Kwa mfano kuna mrani wa One-laptop sisi hatumo.
c)Kuwekeza kwenye infrastructure. Hii sio barabara tu, bali bandari zetu, huduma za maji na nishati na communication.
d) Kuweka mfumo wa kodi ulio wazi.
e) Kuweka sheria zilizo wazi na zinazotekelezwa. Haki ni lazima ionekane inatendeka.

Wenzangu wataweza kuongeza mengine. Yote haya yako ndani ya uwezo wetu lakini hatutaki kuyafanya. Bila haya hao wawekezaji hawatakuja.Tunasahau kuwa hawa ni mabepari na kinachowaongoza ni bottom line. Hawalazimishwi hata siku moja na serikali zao kuwekeza pale ambapo hapana faida. Tukiweka mazingira bora watakuja wenyewe. Hawatasubiri taarifa ya hao tunaowategemea.

Kama alivyosema Mwafrika wa Kike hii ni kama ile ya kutafuta mganga wa kutuzalishia mvua wakati wote tunajua ni uharibifu wetu wa mazingira na vyanzo vya mito ndio culprits wakubwa! Naona badala ya timu yetu ya mpira peke yake kuwa kichwa cha mwendawazimu, nchi nzima inaelekea huko!
 
Hapo mkuu cha muhimu na kwa kifupi ni kuondoa within and beyond border constraints.

Jaribuni kusoma hii report hapa. Wawekezaji wengi huwa wanaiangalia hii report kabla ya kuwekeza.
http://www.doingbusiness.org/ExploreEconomies/?economyid=185
 
Mkuu sipingi ila nasema tuwatumie wataalamu wetu, tutumie taasisi zetu kama SIDO, SUA, DIT, UDS, ESRF, REPOA, VETA etc. Ni muhimu sana kuwatumia wataalamu wetu mkuu.
Kama hatutawatumia watapractice vipi na lini?

Mkuu unajua miradi mingi ya Donors huwa inakufa jamaa wakiondoka kwa sababu wakija wanakuja na wataalamu wao na wakiondoka wanaondoka na utalamu wao. Sasa inabidi iangaliwe upya namna ya kuatach local people na hao wataalamu mkuu wa kutoka nnje otherwise siku zote tutakuwa tegemezi.

Nikupe mfano tuu unajua Tazania tunamakandarasi wengi sana? huwa wanafanya nini? Unakuta kampuni ya china wanakuja hadi na vibarua wakati mwingine wanakuja hata na wafungwa kufanya kazi wakiondoka na mradi umeondoka.

Practice makes perfect.

Yote hayo tufanye na wataalam wa kutushauri tusiwache kuwaleta
 
Tatizo ni kwamba unasema na kujijibu mwenyewe, sasa kuna ubaya gani Tanzania ikileta mshauri wa Kijapan?

Dar es salaam.
Read between the line. Digest. Filtrate the meanining.

Tatizo si huyo mjapan tatizo ni ninyi SISIEMU.
Katika suala la ujenzi wa Technolojia Viwanda na Biashara ninyi SISIEMU Vision yenu ni Zero,mmeshindwa na hamsaidiki.

You belong to a Dumpstar.

Fikra zenu na dhamira zinawasukuma kuweka uchumi wa nchi mikononi mwa wageni kwa sababu mnaamini kwa dhati kwamba wananchi wa Tanzania kamwe hawawezi kuongoza mashirika yao wenyewe na kuyapeleka katika ufanisi.

Mmeshindwa kuwapa nafasi wananchi kuyanunua na kuyaongoza mashirika ambayo serikali ya chama cha SISIEMU imebuma kuyaongoza kwa sababu ya Uroho, Ubinafsi, Upofu wa maono na hamu na nia yenu chafu kutajirika kwa KIFISADI.

Ukweli kwamba Mashirika ya Umma yamekufa mbele ya Usimamizi wenu na mbele ya utaratibu usio wa kisayansi wa kuendesha mashirika mlioujenga kwa miaka 47, utaratibu ambao umefanya SISIEMU kukosa kabisa mwelekeo katika ujenzi na uendeshaji wa viwanda; si FREE TICKET ya kuuza kila Shirika kwa wageni na kuja kutamba Ki Umsloopagas hapa JF, kwamba kuweka viwanda mikononi mwa wageni ni jambo la msingi na jambo la maendeleo kwa wanchi wote wa Tanzania, na watanzania wote tunatakiwa kujivunia.

Watanzania hawajashindwa kumiriki na kuyaendesha mashirika yao ndani ya nchi yao.
Ninyi SISIEMU na serikali yenu ndiyo meshindwa na kulegea katika uongozi wa Mashirika na viwanda.
Uongozi wenu wa miaka 47 umeshindwa, umebuma umelegea kabisa kiasi cha kuamini kwamba mkipigwa Fobe na Wazungu Mashirika yenu yatadumu na uchumi wa nchi utafufuka.

Tanzania imeuza Dhahabu ya thamani ya $3,000,000,000.00 katika soko la dunia kwa muda wa miaka 6 tangu wazungu waanze kuichimba, hayo ndo maendeleo ambayo SISIEMU inaweza kujivunia Duniani kote, wakati ni 0.03% ndo imeingia kwenye mfuko wa serikali na ninyi SISIEMU kugawana 120% ya hiyo 0.03%.

Maendeleo na ndege upaa katika duru za SISIEMuni kujijaza manoti mifukoni mwenu na kwenye mifukio ya vimada wenu.

Watanzania wakiomba kununua mashirika ya umma ninyi SISIEMU macho yanawatoka midomo inatoa mapovu mikono inakinga ngumi na kupiga Ukelele mkuu kama radi za masika kule Morogoro na upiga kura ya turufu ya hapana. Hapna kwa wananchi ndiyo kwa wageni.
Yote hayo ni kwa sababu moja tu mnaweka kwenye mzani Rushwa kutoka kwa wageni dhidi ya kuwamirikisha mashirika wananchi ili wayaendeshe kwa nguvu zao wenyewe.

SISIEMU mmeshindwa katika Uongozi na Utawala wa kisiasa na kiuchumi sasa mnataka kwenda kuzimu na kila Mtanzania.
Jambo hilo la kutupeleka Watanzania wote kuzimu mimi Madela Wa Madilu nimelikata na nina uhakika wenzangu wengi tu hapa JF na Tanzania kwa ujumla wanalikataa.
Siku ya kwenda kuzimu ikifika Wewe Dar na wenzio wa SISIEMU mtaenda pekee yenu, amani iwe nanyi.

Ndugu yangu Dar, SISIEMU ikishindwa imeshindwa SISIEMU siyo Tanzania.
SISIEMU ni sehemu ndogo ya Watanzania.
SISIEMU si Tanzania wala haitakuwa.

Kumleta Mjapan ni tatizo lakini si Tatizo la msingi .
Tatizo la msingi ni Vision ya chama chenu cha SISIEMU ya kuamini kwamba ni wageni tu ndiyo wenye uwezo wa kushauri na kujenga uchumi.
Tatizo kubwa si mjapan tatizo ni ufinyu wa Mtazamo na wepesi wa kurukia ushauri wa nje kutoka kwa watu wageni kuliko kuweka umakini na upembuzi na kutumia ushauri wa ndani ulio jaa tele.

Hata kama mngeita Wjapani wote vipnga waje Tanzania kushauri na kuongoza mashirka kama SISIEMU bado iko madarakani uchumi utaendelea kubuma tu. Kuna utamaduni unaoendana na ukuzaji wa Teknolojia biashara na viwanda ambao ninyi SISIEMu mmeupa makalio.

Si hivyo tu hata kama Chama cha SISIEMU ,mashabiki na wapenzi w wake wote watapewa waingoze Japan baada ya miaka 3 Japan itakuwa ni moja kati wadaiwa wakubwa Duniani,na kwa mara ya kwanza tajiri mkubwa kuliko wote duniani atakuwa Mtanzania mwana SISIEMU Kwa nini?

Kwa sababu SISIEMU ni Bomu hakuna hirizi wala mzizi wa kuwaponya na jinamizi hili zaidi ya kifo chenu wenyewe.

SISIEMU mnatakiwa kufa ili mjiponye!!!?!!!

Wajapan wana interest na South Corridor ndiyo maana wamekuwa wepesi kuikubali Post hiyo ya ushauri.
Wajapan wanataka kuwapiga South na ninyi kwa tamaa ya pesa mmekubali kwii!! kwii!! kwii!! kwii!!
Wanataka Bandari ya Mtwara na Madini ya Chuma na makaa ya mawe yote yapatikanayo kule South.
Ndugu Dar kwa kuwaita Wajapan kuwa washauri wa Serikali ya SISIEMU mmepingwa kazu na kufungwa goli la fobe.

Dar es salaam Read my lips.

By the way where is your causin Mchambuzi????
 
Tukirudi kwenye mada. Unasema kuwa tuna priorities zingine na R & D hatuwezi. Watu wakisema NDIO TULIVYO, unaleta Uzalendo. Hii mada ina makundi mawili tu (kama binary function). Kundi la kwanza ni kukubali kuwa tunaweza na vitu gani vifanyike. Kundi la pili NDIVYO TULIVYO, ukiwa mjanja wewe ni Exceptional.

Haunitendei haki, Fundi mwenzangu! Nitakuwa mpuuzi nikisema kuwa Research and Development hatuiwezi. Ninachosema ni lazima tuangalie context. Matatizo yetu tunakimbilia prestige badala ya realities. Badala ya kutengeneza barabara tunanunua ma SUV ya bei mbaya kwa kisingizio barabara zetu mbaya! Huko Amani kuna kituo cha utafiti wa Malaria na kinafanya kazi nzuri sana. hatuioni hiyo. Hao watafiti wengi wao ni watanzania wenzetu, chuo kinaongozwa na mtanzania, tatizo linalotafiti ni hilo linaloua sehemu kubwa ya watoto wetu. Mbona hao hatuwaoni bali tunashinda kulalamikia miradi mbuzi kama ya Nyumbu? Sasa kama genetically tumeumbwa kushindwa, mbona huko tunafanikiwa?

Mimi nawapinga nyinyi mnaosema kuwa NDIVYO TULIVYO kwa sababu naona mnarahisisha mambo mno. Hamjaainisha kuwa mkisema hivyo mna maana gani? Tulivyo kama nini? Mazezeta? Wezi? Wazembe? Tuonaokumbatia uhalifu? Tulivyo kama nini? Nilitoa mfano wa Enron na Black na wenzangu wakasema hapo si swali la kuiba bali ni hatua gani wahalifu wanachukuliwa. Mimi nilitoa mfano huo kuonyesha wote, bila kuangalia rangi, tuna wahalifu miongoni mwetu. Kwa sababu wakubwa wetu ( ambao ni wachache katika jamii) wanakumbatia wahalifu haina maana kuwa waafrika wote tunafurahia wahalifu. Hao mnaowazungumzia wangeiba kuku manzese mahali ambapo mwananchi anauwezo wa kuonyesha hasira zake saa hizi wangekuwa marehemu. Hauwezi kusema jamii inayofanya hivi inakumbatia uhalifu! Na wanafanya hivi kwa sababu hawana imani na hizo institutions zilizopo kwa sababu wanajua haziangalii value zao. Hamuwezi kuwahukumu wote hawa kwa makosa ya wachache. kusema hivi si uzalendo, ni reality.

Tukirudi tena kwenye mada hii. Naamini kuwa moja ya matatizo yetu ni ile ya kudhani kuwa mkombozi wetu ni sayansi pekee. la, hasha hata hao mnaowaita mangwini wana sehemu kubwa katika tafiti. Naamini kuna haja ya jamii yetu kwanza kujaribu kuji'define' kama jamii. Tukisema sisi ni watanzania tuna maana gani? Nini kinachotuunganisha? Tunahitaji kufanya utafiti katika hizi social issues ambazo zitatupa uelewa na uwezo wa kukabili na kutatua matatizo ya kifikira yaliyotutawala.
 
Mtoto wa Mkulima na Mkandara na baadhi ya wachangiaji wengine, kuna kitu ambacho mmejaribu kukieleza hapo lakini naona hamkitaji; nacho ni UTAMADUNI. Utamaduni wetu ndiyo kitu kikubwa ambacho kinamfanya mkuu Nyani Ngabu asisitize, 'Waafrika Ndivyo Tulivyo'. Ni swala contentious hili, ndiyo maana saa nyingine ni vigumu hata kuliongelea kuwa ni chanzo chetu cha matatizo yaliyo mengi. Maana kuna wengine kitu utamaduni kimeingiliana na dini au imani. Ninacho ongelea hapa ni utamaduni wa kufanya kazi bila kusukumwa, utamaduni wa kufanya kazi kwa manufaa ya jamii yako badala ya tumbo lako tu.

Hebu fikiria sasa, sawa tunakubali ushauri kutoka kwa yeyote yule ambaye tuna imani naye na tunauhakika anaujuzi fulani hivi katika kuliko sisi katika kile tunachokitaka; lakini hapo hapo lazima tujue hakuna kitu cha bure maishani, kila kitu kina cost yake, na cost mojawapo ni utamaduni. Mfano, je huyo mshauri akianza kutuambia kuwa kafanyeni kazi za ujenzi wa mabarabara siku za jumapili au ijumaa ili kuondokana na matatizo yaliyopo?! Je akianza kutuambia kuwa ni lazima tuwanyonge wale wote walio iba hela za mabarabara?!... na maswala mengine mengine mengi yanayoweza kupingana na imani au tamaduni zetu. Utamaduni wa kuwa wawazi na kuteteana likiwa mojawapo.

Kila jamii ina matatizo yake na ina mambo ambayo ni ya kuigwa na jamii nyingine. Hata hivyo jamii nyingi zilizo endelea au tunazo ona zimeendelea zina vitu katika tamaduni zao ambavyo vinashabihiana sana na tamaduni zetu, na hizo elements ukiziangalia kiundani utakuta ndiyo factors kubwa sana zilizochangia maendeleo ya jamii zao. Nyani Ngabu anaposema kuwa 'waafrika ndivyo tulivyo' hata mimi nachukia na inanifanya nijihisi ovyo... lakini statement yake ina ukweli mkubwa tu ndani yake na kama mnavyomjua Nyani, one word from him replaces a ten fold words for many of us.

Mfano mzuri kwa Afrika yetu ni kutazama nchi ambazo tunaona zina ahueni kuliko sisi... je ni nani aliye nyuma ya hiyo ahueni?! Kuna article naiandika muda mrefu sasa nilisha promise kuiweka hapa kama thread, itakuwa siyo ndefu sana lakini ni ambayo mimi nina imani ina jibu au basi niseme moja la majibu makubwa ya matatizo yetu mengi... nilipromise nitaandika baada ya kuona mwelekeo wa thread iliyokuwa inaongelea issue ya Dr. Watson.

Hiyo ya kuhitaji kuchapwa viboko na kuunga mkono, ndio maana mpaka leo tu-masikini na mitaji ya asili tunayo.

Natumaini unaongelea viboko vya kiakili... maana hivi ndiyo hatukuchapwa, viboko vya kuchapwa matakoni na migongoni vilifanywa sana na Wajerumani wakati wa kujenga reli ya kati, lakini naona tuliota sugu, maumivu yakatoweka hata baada ya uhuru miaka arobaini na... hatujaweza kujenga reli nyingine kwa nguvu yetu wenyewe kutokana na uchungu maumivu hayo... will we ever learn?.... (UTAMADUNI - maana mtu ni vigumu sana kukubali wake ubadilishwe na mtu mwingine!!)

Inabidi tutafute washauri na huyu mmoja hatutoshi, kila sehemu tunahitaji washauri na mpaka watendaji hatuna, tunahitaji watendaji vile vile.
Kweli kabisa tunahitaji watendaji katika ngazi zote, makada wa vyama hadi Rais... lakini je, tutawapata watendaji wa namna hii hali tuna UTAMADUNI wetu wa kulindana katika KILA SEHEMU maishani mwetu?! Maana matamko ya kuleta maendeleo miaka nenda rudi na bado yanaendelea kutolewa hii leo...

Leo kuna mifano hai kibao, wawekezaji wote, wameleta wataalam kutoka nje, hata makarani simpo tu. Kwa nini? jibu tunalo lakini hatutaki kuukubali ukweli, bado ni kidogo sana wawezao hapa kwetu na wengi (majority) ni opportunists tu. Utakaloambiwa fanya utasema unaliweza kumbe wapiiii? Hao wataalamu wetu mnaoongelea wako wapi? wanafanya nini? nani aliowazuia kuonyesha utaalam wao? mnaandikia mate wakati wino upo?

DSM, naona umejijibu hapa kama tu vile Madela alivyofanya hapo awali, au jibu la Nyani Ngabu limekuingia?!

SteveD.
 
Wakati mwingine nadhani Dar es Salaam unapinga kwa ajili ya kupinga tu. Hapa kinachopingwa ni kile kilichoandikwa kuwa huyu mtaalamu mmoja kutoka Japan ndiye atakayetukwamua katika matatizo yetu na kutufanya nchi inayotegemea viwanda. Hawakusema kuwa huu ni mwanzo wa ushirikiano na serikali ya Japan katika kuikwamua nchi yetu bali huyu Bwana single-handedly ataweza ambacho watanzania karibu milioni 40 wameshindwa! Hivi unaamini kuwa baada ya huyu bwana kuandika ripoti yake ndipo wakina Sony, Toshiba, Toyota watakimbilia kuwekeza nchini mwetu? Nadhani ni Bin Maryam aliyesema kuwa tumeanza kuwa na siasa za mpirani. Nani asiyejua mambo yanayotuzuia kuendelea? Hao washauri wa nje na ndani wamekuwa wakituimbia kila siku lakini hatutaki kusikia. Tunataka njia ya mkato. Mimi ambaye si mtaalamu najua kuwa tunahitaji kuwekeza kwenye vifuatavyo ili kuvutia wawekezaji makini:
a) Kupunguza ukiritimba katika mambo yetu. Hii inajumuisha usiri katika mambo yetu.
b) Kuhakikisha kuwa elimu ya msingi tunayotoa inaendana na mahitaji ya sasa hivi. Kwa mfano kuna mrani wa One-laptop sisi hatumo.
c)Kuwekeza kwenye infrastructure. Hii sio barabara tu, bali bandari zetu, huduma za maji na nishati na communication.
d) Kuweka mfumo wa kodi ulio wazi.
e) Kuweka sheria zilizo wazi na zinazotekelezwa. Haki ni lazima ionekane inatendeka.

Wenzangu wataweza kuongeza mengine. Yote haya yako ndani ya uwezo wetu lakini hatutaki kuyafanya. Bila haya hao wawekezaji hawatakuja.Tunasahau kuwa hawa ni mabepari na kinachowaongoza ni bottom line. Hawalazimishwi hata siku moja na serikali zao kuwekeza pale ambapo hapana faida. Tukiweka mazingira bora watakuja wenyewe. Hawatasubiri taarifa ya hao tunaowategemea.

Kama alivyosema Mwafrika wa Kike hii ni kama ile ya kutafuta mganga wa kutuzalishia mvua wakati wote tunajua ni uharibifu wetu wa mazingira na vyanzo vya mito ndio culprits wakubwa! Naona badala ya timu yetu ya mpira peke yake kuwa kichwa cha mwendawazimu, nchi nzima inaelekea huko!

naomba usome post zangu zote hapo juu, ndio utaelewa nilichokisema.
 
Huyu mtaalam wa Japan ni bogus na to me ni usanii tu wa serikali.

I think this is not fair sentense, do you know him? imean professionally?

Kwa nini anashambuliwa kwa kuja kwake? Nagu ameeleza wazi amekuja kutokana na maombi ya raisi, hivyo serikali ya Japan ikaridhia na kutupatia huyu jamaa.

Mtu huwezi kujua kila kitu, mimi na appreciate kwa ujio wake, kwa sababu Wajapan tofauti na wachina they are very hard working, committed and honesty.

I hope we can learn something from them.
I wish i could be part of his/her team, actually ningeutilize hii chance na kujifunza effectively.
 
STEV D.
Ni kweli kabisa culture inaplay role kubwa sana kwa maendeleo ya sector yeyote mkuu ndio maana tuna watu wachonga vinyago wanatoka sehemu fulani, wahunzi wanatoka sehemu fulani, wafanya biashara wanatoka sehemu fulani, wavuvi wanatoka sehemu fulani. Hiyo ni utamaduni na geographical location inajenga tabia fulani.

Utamaduni huo huo ndio unafanya watu wengine kuwa ni wavivu wanapenda kucheza ngoma kukaa vibarazani nk. Wakati utamaduni huo huo unafanya watu wafanye kazi hata masaa 12 kwa siku.

Hapa Japan kufanya kazi ni culture. Ukiingia ofsini saa tatu kutoka oficially ni saa kumi na mbili lakini hakuna anayetoka watu wanafanya kazi kama hawanaakili nzuri ndio maana tunaita Japan ni Seven Eleven ( Kazi kuanzia saa moja had saa tano usiku)

Ni culture mkuu. Asante sana kwa kunikumbusha hilo.

KWA UFUPI HUWA NAPENDA KUSEMA KUWA OUR POVERTY IS IN OUR MIND.

Na hii ndio huwa inatufanya sisi tuamini kuwa hatuwezi kufanya chochote. Mkipata mda someni kitabu cha Bill Cosby "WAKE UP PEOPLE"
 
But my thing is...why would these people give us money anyways? Who gave them the money that they have? Why can't we make/ have our own money?

Who told you that we don't have our own money? We do. Isipokuwa zinaliwa na wajanja wachache kupitia mikataba mibovu yenye kusikitisha sana.

Wahisani wakileta misaada, wanasimamia wenyewe ili iwafikie walengwa. Matokeo yake ni kwamba pesa tunazokusanya kutokana na kodi zinaliwa kupitia EPA, RICHMOND you name it.

Chukulia hizo dola milioni 700 za Bush ambazo zimeonekana kama ni neema kubwa sana kwa Watanzania, wakati pesa za Richmond na EPA peke yake ukizichanganya zinakuwa zaidi ya nusu ya pesa hizo alizotoa Bush kisha akaonekana kama malaika wa nuru. Pia EPA ni akaunti ndogo tu pale BOT kati ya nyingi zenye mianya ya kuchotwa pesa. Mengi mtayasikia.

Tatizo kubwa ni mfumo mbovu wa ukusanyaji na usimamizi wa mapato na matumizi ya pesa zetu wenyewe. Sheria ikichukua mkondo wake bila kujali cheo wala rangi ya mtu tutapiga hatua.
 
I think this is not fair sentense, do you know him? imean professionally?

Kwa nini anashambuliwa kwa kuja kwake? Nagu ameeleza wazi amekuja kutokana na maombi ya raisi, hivyo serikali ya Japan ikaridhia na kutupatia huyu jamaa.

Mtu huwezi kujua kila kitu, mimi na appreciate kwa ujio wake, kwa sababu Wajapan tofauti na wachina they are very hard working, committed and honesty.

I hope we can learn something from them.
I wish i could be part of his/her team, actually ningeutilize hii chance na kujifunza effectively.

Are japanese honest??

Do you know anything about YAKUZA???
 
situliwahi kuwa na professa wa umaskini kutoka Peru na MKURABITA yake mbona umaskini unanawiri! hizo 133bn+75bn zilizoliwa mchana kweupe tena mbele ya JK zingekuwa managed vizuri tusingehitaji huyo mjapani.

kichefuchefu kiko kwenye mikopo ya JK kanda ya ziwa, kama sio mngoni au mnyakyusa huwezi pata mkopo posta bank, ACB ndio balaa yale mala rushwa ya NMB yamekimbilia huko!

tuliwahi kuomba list ya watu walionufaika na mikopo hiyo ilikuwa ugomvi tukaambiwa sisi madiwani wanafiki sana! kama hakuna wizi na ukabila mbona hawataki kubandika majina ya walionufaika katika ofisi za WEO!
 
Tunahitaji kweli mtaalamu kuja kututatulia matatizo kama haya ya Mfamaji? Hawa wakienda kwenye Chamber zao za biashara na kutoa hadithi kama hizi haji mtu kuwekeza? Huu ni UTAMADUNI unaobadilika!
 
Tumekuwa na kawaida ya kuwalaumu wataalamu wetu kwa kila kitu bila kuangalia mazingira wanayofanyia kazi. Huyu mtaalamu mgeni atapewa kila ushirikiano ( tumeona wote jinsi waziri alivyomchangamkia), atapewa ofisi inayoendana na hadhi yake ili asije akaumwa mbu wa malaria, atapewa usafiri wa nguvu, atafutiwa nyumba au hoteli sehemu mwanana na cha muhimu kupita yote atapewa access kwa kila mtu na kila kitu! Huyo mtaalamu wa kitanzania vyote hivi hapati na ni ndoto tu kutegemea kuwa wakubwa watakuwa na muda wa kumsikiliza. Huyu mgeni hata akija akatoa pumba wote watamsifia maana hakuna mwenye ubavu wa kumnyooshea kidole. Yule mtaalamu mzalendo ataitwa kwa wakubwa na kuelekezwa na mtu ambaye hana ujuzi wowote katika fani yake. Ripoti zake ( ambazo ameandika katika hali ngumu kwa sababu mgao wa karatasi ni mkali na kompyuta mbili zilizopo zote ziko kwa mkuu) zitabaki zikikusanya vumbi. Huyu mgeni ataruhusiwa kupekuwa kila mahali wakati mwenzetu atakumbana na Confidential kila atakapogeuka. Kwa vile huyu mgeni ana usafiri unaojazwa mafuta kila wakati hata pata shida kutembelea sehemu husika kila anapohitaji. huyu mtaalamu wetu akitaka kusafiri ataambiwa vote imekwisha au fedha zilizobaki kwenye vote zimebakizwa ili kama Mkuu AKITAKA kussfiri asipate shida. huyu mgeni akitaka kumuona kiongozi yeyote serikalini hana hata haja ya appointment, yeye ni kupiga simu tu na milango inafunguliwa. Mtaalamu wetu akipiga simu atasukumizwa kwa OS maana wote wako busy kumjibu. Huyu mwenzetu akija kukutana na huyo mgeni atagundua kuwa ni graduate wa juzi kutoka polytechnic na yeye alisoma huko huko alikotoka na ujuzi wa miaka mingi. Pamoja na haya yote viongozi wake watamwambia awajibike kwa huyu mgeni. na akija sema, jamaani kuna tatizo hapa, ataonekana ana wivu. Sasa ndugu zangu, mnategemea nini kutoka kwa huyu mwenzetu?
 
Back
Top Bottom