Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Sishangai ulicho andika hapa sababu umesema haujui kiingereza.Ndio maana najiuliza mbona unashupalia sana kuhusu ushindani na kupingwa ? Jibu linaonyesha ya kuwa hauko makini juu ya kuhakiki habari, na kila anaye nituhumu kwa ubishi na ushindani mwisho wake aibu inarudi kwake kwani wengi huwa hawajui wanachokiegemea au kukurupuka.
Swali langu halijakutaka unitajie abiria walio potea, swali langu limekuta unitajie watu japo watatu tu ambao wamepotelewa na ndugu na jamaa zao, ungekuwa makini hili swali ungekaa na ukajiuliza kwanini nimeuliza walio potelewa na ndugu na sio walio potea ? Sasa umakimi unatakiwa uwe nao.
Usichokijua ni kuwa, nimefunzwa kuutafuta ukweli tokea shinani yaani kwenye msingi,msingi ambao bilo huo msingi jengo halisimami.
Sasa nimekuliza "A" unajibu "B" yaani unajibu nisicho kuuliza. Kwa kutokuwa kwako makini, kule mwanzo ukajidai unanikosoa, hatimae ukakosea kunikosoa.
Nahitimisha ya kuwa, sina haja ya kuanzisha uzi sababu maswali yangu yako wazi na yamejitosheleza, narudia tena na tena, kama hivi tu hujibu ulichoulizwa nikianzisha mada itakuwaje ?
Umenikumbusha kitabu fulani kiitwacho "The Incoherence of the Incoherence" cha Ibn Rushd. Yaani kuna watu mnakosea kukosoa, yaani unahisi unamkosoa fulani kumbe unakosea wewe unaekosea.
Ukirudi tena, uongeze umakini mzee,ujibi unachoulizwa.
Karudie kusoma yale majina kisha angalia kwa makini, kila baada ya jina la muhanga na kazi au cheo chake kuna mabano linafuata jina la ndugu wa muhanga, kisha mambo ya anuani n.k.
Unaelewa nini ukiona father, wife, Sister?
Mimi nimekujibu ulicho uliza na taarifa za ziada.
Unajiaibisha mkuu wangu, na huu ndio tunaoita ubishi sio mijadala.
Ingekuwa majadiliano basi ungejipa muda kusoma taarifa nilizokuwekea na kuuliza usichoelewa na kukiri ulicho kosea.