Imani kila mtu anayo mkuu, Tatizo ni kwamba Inapozungumziwa Imani inakua based kwenye dini.
Mimi sina dini ila nina Imani, Mfano:
•Hapa ninachati nawewe nikiamini utajibu hii quote wakati sijui kama utakufa au nitakufa dakika 1 mbele kabla hujajibu, Au huenda labda dakika 2 mbele JF itafungiwa lakini bado naitumia, hii ni Imani.
•Ninamalengo ya siku, wiki na Mwaka, Tena kila siku ninajiambia lazima siku fulani nifanye kitu fulani bila kuwaza kwamba huenda nikawa nimekufa, hii ni Imani.
•Napanda basi kuelekea mkoa X nikiamini nitafika, hii ni Imani.
•Ninaelekea mahali X may be sokoni huku nikiamini nitafika na nitapata ninachokitaka hii pia ni Imani.
•Mimi ninafanya Body workout, ninakula balance diet na kufanya mazoezi kwa bidii nikiamini vitaniletea matokeo, hii pia ni Imani.
Kabla hatujaendelea, Kwa uelewa wako Imani ni nini?