Kwanza mbona hata Zanzibar inatajwa sana?
Kuna watu wanapenda sehemu hata kwa jina tu.
Pili, Kenya ilikuwa ni koloni la Waingereza ambalo walilitayarisha kuwa kama Australia ya Africa. Walitaka ma settlers wa Uingereza waje kuhamia Kenya kimoja.
Ndiyo maana mpaka leo uchumi wa Kenya hulinganishi na wa Tanzania, kilimo, viwanda etc.
Angalia wanariadha wa Kenya wanavyopata international endorsements kwa sababu ya kujipanga vizuri tu, halafu angalia wanariadha wa Tanzania upande wa pili wa mpaka tu wanavyoshindwa kujipanga, hawa ni watu ambao ki baiolojia na ki genetic wako karibu sawa, tofauti ni business culture ya nchi tu.
Mpaka leo, regional headquarters za makampuni mengi ya kimataifa zipo Kenya.
Tatu,
Wakenya waponseruois kwenye biashara. Wana business culture inayieleweka kwa watubwa magharibi, sisi Tsnzania ambao tulitakiwa tuwe wapinzani wao tumelemazwa na Ujamaa. Ndiyo maana mpaka leo Tanzanite inaoatikana Tanzania tu, lakini inauzwa sana Kenya na India.
Benjamin Fernandez, Mtanzania aliyeanzisha mfumo wa malipo kimtandao wa NALA, alikuja Tanzania akataka kuweka makao makuu ya biashara zake Tanzania, akapata mpaka support ya rais, rais akasema atamsaidia kwa lolote analotaka. Lakini serikali ya Tanzania imem frustrate sana Benjamin mpaka akaenda kuanzisha makao makuu yake Nairobi. Maana yake analipa kodi Kenya badala ya Tanzania.
Ukiangalia "Ease of Doing Business" reports utaona kitu kinachotumia siku chache, au wiki chache Kenya, Tanzania kinachukua miezi. Wametupita mbali sana hapo Wakenya.
Free and open access to global development data
data.worldbank.org