What's so special about Nairobi?

What's so special about Nairobi?

Nairobi Money Heist.jpeg
 
Sio kweli Nairobi ni Jiji kubwa Mjini sio pa kawaida kama unavyopazungumzia...mimi nimeenda majiji mengi Duniani ila Nairobi nawapa Sifa yao ya uzuri...
Hyu anasema alienda kibiashara kuna uwezekano alienda kule westland kwa wasomali
 
Nairobi ni half London kabla hujaenda huko kwa wazungu hakikisha umepita Nairobi utoe tongo tongo

Ujamaa na Ccm vimetukosesha mambo mengi sana

Kigali ni ndogo sana kwa Nairobi kuanzia ukubwa wa eneo majengo na vingine ila kwa usafi Kigali ipo juu sana
Nairobi kuna tongotongo gani la kutoa pale mazee 😀,sema wale watu mindset yao tu ya ubepari inawabeba sie ujamaa umetufanya tujione we are nothing at least sasa hivi kidogo ndio tumeanza kushtuka
 
Ukoloni wa Kenya ulikuwa wa ki settlers zaidi, waliwekeza sana wakati wa ukoloni mpaka leo kuna wazungu wanamiliki ardhi za kutisha Kenya. Hata kuondoka kwa wazungu Kenya ilikuwa kwa mbinde sana, rejea ishu ya maumau.

Wakati wa vita baridi Kenya wao waliamua kujiunga na West na kubaki katika ubepari. Haikuingia katika siasa za ujamaa.

Lugha ya Kingereza nayo inawebeba sana, Kiswahili sio lugha inayozungumzwa sana nje ya Africa Mashariki.

Serikali zote za Kenya zimekuwa wanaheshimu sana property rights na uwekezaji binafsi. Kenya sio rahisi serikali kuingilia mali au biashara binafsi kwa sababu ya siasa. Kuna watu walikwapua ardhi wakati wa uhuru lakini hawajawahi kunyang'anywa mpaka leo. Odinga alivyokuwa mpinzani wa serikali kwa miaka yote asingeweza kufanya biashara na kuwa na ukwasi mkubwa kama alio nao leo ingekuwa nchi nyingine za Africa Mashariki.

Pia Kenya wameweza kutumia rasilimali chache walizo nazo kwa ufanisi zaidi na pia kutumika kama kituo cha biashara na magendo ya rasilimali za madini kutoka nchi nyingine nyingi za Africa. Kuna kitu huwa kinaitwa laana ya rasilimali ambayo hupata nchi nyingi zenye rasilimali nyingi, huenda Kenya kutokuwa na rasilimali nyingi pia wameepuka hilo na kujikita zaidi katika biashara.
Hii kitu nakubaliana nawe 100%,kenya mambo ya siasa na biashara wameyaweka mbali mbali japo wafanyabiashara wao wakubwa ni wanasiasa
 
Umeongea vyote sawa kuna hili la wakenya "kuabudu Sana wazungu"..
Waajiriwa wa Kikenya huwa waaminifu Sana wanapoajiriwa na Wazungu.....
Wabongo Ile culture ya Ujamaa na kujitegemea imepelekea pia tuwe
"Masikini jeuri"...hatuwababaikii wazungu Sana na tuna culture ya "kuiba kazini "very very unique
Mtu anaajiriwa haulizi mshahara..anauliza wenzie "hapa mnaishi vipi"... culture ilianzia mashirika ya umma sasa imekuwa kila sehemu....mgeni akileta kampuni Tz anapaswa kuwa makini mno na kila mtu...dereva ataiba mafuta... secretary ataiba karatasi...etc ..
Hivi kuibiwa muajiri wako ndio kutoabudu Wazungu?
 
Sio kweli Nairobi ni Jiji kubwa Mjini sio pa kawaida kama unavyopazungumzia...mimi nimeenda majiji mengi Duniani ila Nairobi nawapa Sifa yao ya uzuri...

Kwa hiyo umeenda Windhoek, Gaborone, pia Rabat mpaka Doha, lakini Nairobi ukaipa sifa yake!!!?
 
Uwezi kuishi Tanzania alafu ukaenda Nairobi ukasema n pa kawaida sana aisee Nairobi n kitu kingine kabisa kuanzia

1. Watu wa Nairobi wapo fasta sana

2. Maisha ya Nairobi n ghali lakin yamenyooka

3. Biashara za Nairobi n kubwa na mzunguko n Mkubwa ukiwa na akili kutoboa n sekunde.

4. Viwanda n vikubwa na vingi hurahisisha Biashara.

5. Barabara hapa wako vizuri Sana Mara 100 ya dar es salaam

6. Makasi na majengo hapa ndio utaweza kubattle kidogo na mji pendwa wa DSM Ila wale wa Makasi duni wengi n nyumba za bati(hii unaikuta hasa kwenye mijibya zamani yenye wakazi wengi na kipato Chao Cha kawaida wengi wao ndio mahustler wanafanya nairobi iwe Kama ilivyo Sasa) Ila usishangae kukuta apartment Kama 100 kwenye compound moja alafu nnkali mbaya alafu sio moja unakuta Kijiji kimependeza hii unaikuta nje ya mji.

7. Club na starehe na wanawake hapa maisha n parefu sana hasa ukiwa na hela za kimawazo za Tanzania Ila wanawake wapo hata saa 1 asubuh n wewe na Bob yako

8. Ushapu wa akili na kujenga hoja huu mji wapo vizuri ukizubaa umeachwa feri

9. Utii wa Sheria na kuwajibika kwa Polisi hapa kila mtu anajua anatakiwa afanye nn WAP na kwasababu gan Nairobi Polisi sio tishio kwa wananchi hapo wanazunguka wawili wawili na bunduki sio ajabu kila baada ya dk 10 ukaona Askari wanapita na bunduki kula Doria Ila Cha ajabu raia wa Nairobi anabishana na Askari Kama mwanae na Askari ananywea.

10. Usafiri wa Nairobi upo kila mahali anzia public na hz Kama Uber hukonndio umefika muda wowote saa yoyote unapata usafiri I kuwa makini Sana na uombe MUNGU kuibiwa au kudhulumiwa n nje nje

11. Usalama wa Mali na wewe mwenyewe hapo kwa wewe mwenyewe Usalama upo kiasi hasa Kama wewe n mgeni Ila kwa Mali yako sio uwenyeji au ugen wakikiweka kwenye Rada uchomoki hata Kama Askari amekaa pembeni in Nairobi vitu Kama simu kuibiwa n fasta tuu hata uiweke pin ya namna gan inaibiwa na inaenda kutolewa Nairobi Hadi Askari wanaibiwa akiwa na uniform Tena kazini pia usjaribu kununua vufaa vya kieletronic eneo moja linaitwa LUTHULI hapo wamelia sio walikuyu, wajaluo, wakamba sijui wameru Yan Tena mgen ndio usiseme hapo mie ndipo ninaponunuaga vifaa vya electronic Ila n uombe MUNGU ogooa duka unapita wadada wakuita sa nyingine kukushika shati na kusema yes customer, karibu hapo usiingie ukiingia utajuta na pesa yako.

Mengine mtaongezea wengine mliofika

Ila msifananishe Nairobi na mji wa ajabu Dar Es Salaam.
 
Back
Top Bottom