Whatsssssss!!!!!!!!!????

Whatsssssss!!!!!!!!!????

Mtoto kaamka asubuhi analia...
Hii iii iii iii, Mama anamuuliza vipi mwanangu asubuhi yote hii unalia nini?,
Mtoto anaendelea kulia tena kwa sauti kuubwaa. Baba anambembeleza "sema basi mtoto mzuri". Mtoto anawaambia wazazi wake huku akiendelea kulia "Nimeota ndoto mbaya sana". Wazazi kwapamoja wanamuuliza "umeota nini".
Mtoto anawajibu,"Nimeota tumefungua shule" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa kanunua mashine kaipeleka
nyumbani. Kazi ya mashine ni kila
ukisema uongo inagundua ni uongo na
inakukandamiza makofi hapo hapo.
Wakati wa msosi wa usiku jamaa akaileta
mashine imekaa kama roboti akaiweka karibu na meza. Akaanza: Mwanangu, leo
wakati wa shule ulikuwa wapi? Mtoto
akajibu: nilikuwa shule baba (Twaaaaaap,
mashine ikamlamba vibao). Samahani
baba ila kwa kweli nilienda kuangalia
sinema kwa kina Mudi. Dingi: Sinema gani? Dogo: Aki na Ukwa. (Twaaaaaaaap,
mashine ikamlamba makofi), samahani
baba, kiukweli ilikuwa ni sinema ya zile
picha mbaya za wakubwa. Dingi: toto
pumbavu sana, enzi zangu mimi hata
sikutamani kuangalia picha za kijinga kama hizo. (Twaaaaaaaaap, mashine
ikamzaba dingi makofi). Mama akaingilia
huku anacheka: Hahahaha, ndo mtoto
wako huyo (Twaaaaaaaaaaaaaap,
mashine ikamkandamiza mama makofi)
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mdada kaenda Salasala kumtembelea
Mkaka. Alipofika kwa mkaka akaingia
chumbani kwa mapenzi
akamwambia Mpenzi, naomba shilingi alfu kumi na tano nilipie taxi niliyokuja nayo.
Mkaka kaingiza mkono mfukoni kutoa pesa ghafla akashtuka!!!
Mkaka: Unasema umekuja na Taxi?
Mbonaumevaa helmet ya Bodaboda?[emoji12]
 
EBOLA" ni tishio:-
Mgonjwa mmoja wa Ebola alipanda madhabahuni
kumshukuru Mungu kwakua AMEPONA,
Baada yakumaliza ushuhuda ile MAIKI
akairudisha kwa Mchungaji!
** Mchungaji akamwambia mpe mzee wa kanisa!
** Mzee wa kanisa akamwambia mpe kiongozi wa
Ibada!
** Kiongozi wa ibada akasema mimi sihusiki na
mambo ya ushuhuda mpe Katibu!
ASKOFU akaona ni usumbufu wa hali ya juu,
akamwambia hiyo MAIKI umezawadiwa
nenda nayo tu nyumbani!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mlevi mmoja aliingia kwenye daladala na
kukaa siti ya mbele halafu akaweka begi
lake kwenye siti ya pembeni kisha
akapitiwa na usingizi. Mara akaingia mlevi mwingine kwenye
daladala hiyo na kulitoa begi la mlevi wa
kwanza kisha akakaa. Mlevi wa kwanza alipoamka alipeleka
mikono yake alipokuwa ameliweka begi
na kuanza kufungua zipu ya suruali ya
mlevi wa pili akidhania ya kwamba ni zipu
ya begi lake, baada ya kufungua zipu
alianza kupapasa ndani ya zipu hiyo. Kwa hasira akauliza, "nani kaweka ndizi na machungwa
kwenye begi langu?[emoji12][emoji13]
 
Mwanafunzi Mtiifu
Mwalimu Majaliwa ni mwalimu pendwa katika shule ya upili ya Mtakuja. Wanafunzi wanampenda sana kwa sababu amekuwa akitoa nasaha nzuri sana kwa vijana wake.
Siku moja aliamua kuzungumuza na wanafunzi wake mara baada ya kumaliza kuwafundisha. Mwalimu alianza kwa kuuliza wanafunzi nini wanafanya baada ya school?
Mwanafunzi wa kwanza akajibu , “naenda kwa Fereji Kibwana kununua bangi.”
Wapili akajibu , “naenda kwa Fereji Kibwana kununua vidonge vya kulevya.”
Watatu akajibu, “naenda kwa Fereji Kibwana kununua bia.”
Wanne akajibu, mimi huwa napumzika, nasoma Quran,navuta uradi na natafuta rizki.”
Mwalimu: Manshalah kijana mzuri na hodari sana. Na jina lako ni nani?
Mwanafunzi wa nne: FEREJI KIBWANA.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Shehe na Padri walikutana ktk ndege1,
Padri: Karibu kitimoto
Shehe: Sisi Haturuhusiwi kula kitimoto.
Padri: Pole, mnakosa UTAMU...!
Walipofika Airport wakaagana
Shehe: Msalimie mkeo
Padri: Sisi haturuhusiwi kuoa,
Shehe: Pole, mnakosa UTAMU...! Je, yupi kati yao anakosa UTAMU ZAID?[emoji12][emoji13]
 
Mnyakyusa mmoja aliwaalika watu katika mazishi ya mama yake. Baada ya kushusha jeneza wakatia ndani ya kaburi viazi, mchele na kuku kadhaa. Mhaya mmoja akauliza, 'Vya nini hivyo?'
Akaambiwa, 'Wafu huenda safari ndefu sana, hivi atakula njiani'.
Mhaya akazama kwenye wallet, akatoa laki 2, akaidondoshea akisema, 'vikiisha hivyo atanunua vingine'. Mkurya mmoja akadondoshea laki moja akasema, 'Isipotosha ataongezea hii'
Mchaga akatoa cheque book, akaandika cheki ya laki 5, akachukua ile laki 3 kwenye kaburi na kuacha cheki akisema, 'bora ukachukue hela mbele ya safari kwa cheki. Vibaka wasije wakakuibia bure'.....
Shikamoo wachaga![emoji12]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Katika kijiji kimoja palikuwepo mganga mmoja mashuhuri sana. Alifahamika kwa namna ambavyo aliweza kuwatibu wagonjwa, kutabiri, na hata kutatua migogoro iliyojitokeza kijijini.
Siku moja walikuja wezi na kuiba ng'ombe wa wanakijiji. Wanakijiji, wakamuendea mganga ili aweze kuwaambia ni nani wameiba ng'ombe zao. Basi mganga akawaambia wawaite wanakijiji wote mkutanoni ili pia atumie wasaa huo kuwabaini wezi. Mkutano mkubwa ukaitwa, wakakusanyika watu wote wakiwemo na wale wezi maana walisema "twendeni tukaone kama atatutambua". Basi mganga akajitokeza pale mkutanoni..akaanza kusema sema maneno aliyoyajua yeye, kisha akawakazia macho wanakijiji na kusema..."wezi ni hao walioota pembe vichwani mwao". Wale wezi kwa mshtuko mkubwa wakashika vichwa vyao kuvikagua...na hapo hapo mganga akasema WAKAMATENI HAO WALIOSHIKA VICHWA!..
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dogo kaingia saluni ya mtaani kwao, kinyozi
akamnong’oneza mteja: "unamuona huyo dogo
anayeingia, ni kilaza na mbulula hakuna
mfano. Booonge la mjinga. Ziro kabisa.
Angalia, ngoja nikuhakikishie kwamba dogo ni
mpumbavu"
Kinyozi akachukua noti ya buku 2
akaweka upande mmoja wa meza na noti ya
buku 1 akaweka upande mwingine. Akamuita
dogo akamwambia "unataka ipi kati ya hizo
noti mbili?"
Dogo akanyonya kidole, akachukua
noti ya buku 1 akaondoka zake. Kinyozi
akamwambia yule mteja, "umeona!!? Mara zote
dogo ndo hivyo hivyo. Hajifunzi kabisa ipi
kubwa ipi ndogo. Kilaza"
Baadaye yule mteja akaondoka saluni, mtaani
akakutana na yule dogo analamba booonge la
ice cream, akamuuliza:
" hivi kwa nini ulichukua
noti ya buku ukaacha ya buku mbili?"
Dogo
akamjibu: "siku nikichukua noti kubwa, yule
kinyozi atajua nimeanza kuwa na akili na
mchezo wa kufaidi hela utaisha. Muache
aendelee kuniona mbulula nifanye yangu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bongo Movie Bana Eti Jambazi Kamnyoshea Mtu Bastola Alafu Anamwambia . NITAKUCHINJAAAA..

Nimezima Tv, Nimeona Niingie Jamii Forum[emoji119][emoji119][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23] [emoji23] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Baada ya Talaka mke kamtumia mume meseji "Nasikitika kukujulisha kuwa binti uliyemlea kwa miaka 20 sio mtoto wako" Mume akajibu "Duh! Nashukuru Mungu kwani nilikuwa nikiumia rohoni kila siku kwamba natembea na binti yangu[emoji13] [emoji13]
Mkuu mbavu znavunjika [emoji23] [emoji23]
 
Najua vitu vitano (5) kuhusu wewe!!
1. Unasoma hii msg
2. Wewe ni mtu
3. Huwezi kutamka neno "P" bila kufumbua mdomo
4. Umejaribu kuona kama utaweza
6. Unacheka[emoji16]
7. Uso wako unafuraha, na umeiruka No. 5
8. Umeangalia kama kuna No.5 kweli umeiruka
9. Unaendelea kutabasamu kwasababu nakupatia
10. Umeipenda hii msg[emoji23][emoji23][emoji23], Utaiiba[emoji12]

*_STRESS NI NINI..?_*
*_Stress ni pale unapompa msichana lift halafu akazimia ndani ya gari yako na humjui wala hujui kwao. Ulimkuta tu njiani ukamsaidia.!_*
*_Noma zaidi ni pale unapoamua kumpeleka huyo msichana hospitali na akabainika ana mimba dokta akaanza kukupongeza kuwa unakaribia kuitwa baba!_*
*_Stress ya tatu ni pale unapokataa na kumwambia dokta mimba si ya kwako, mara ghafla msichana anazinduka na kudai mimba ni ya kwako?_*
*_Stress ya nne ni pale dokta anapoamua kukupima ili kuthibitisha, na baada ya vipimo anakwambia mimba si yako kwakuwa huna uwezo wa kumpa mwanamke mimba.!_*
*_Stress ya mwisho ni pale,, unaporidhika majibu ya doctor kuwa huna uwezo wa kumpa mwanamke mimba lakini unakumbuka nyumbani una mke na watoto wawili.....!!![emoji12][emoji13]

STORI FUPI YA KUCHEKESHA
Siku moja nikiwa stand ya mabasi nikiwa naenda kumsindikiza rafiki yangu....nikamuona binti mrembo saana! Aliyevaa nguo za thamani kubwa sana yaani ukimuangalia huna haja ya kujiuliza mara mbili kuwa huyu ni tajiri au mtoto wa tajiri flani ...basi yule binti mrembo alishuka katika gari ya bei mbaya Range Rover SUV huku akiwa analia...na akiwa amempigia magoti mkaka mmoja mchafu aliyedhoofu sana inaonyesha labda alikuwa hapati chakula yaani ukimuangalia haraka huwezi kumtofautisha na wale waokota vyakula barabarani...basi yule dada mrembo akiwa kapiga magoti alianza kumbembeleza yule kaka "mimi sitaki pesa , sitaki nyumba, staki wigs, staki brazillian yaani staki chochote kutoka kwako bali ninachotaka ni penzi lako tu,busu lako tu,na joto lako tu..huyu dada mrembo alitamka maneno haya kwa hisia sana hulu akilia kilio si cha kitoto, nilipoyasikia hayo maneno ya huyo dada kwanza sikuamini, pili nilichanganyikiwa kabisa sababu huyo kaka chokoraa hata habari hakuwa nayo na alikuwa hata hamtizami japo usoni huyo dada mrembo, nikasema huu upuuzi sasa huyu kaka kama hampendi huyu dada na kashindwa kumwelewa na kuthamini pendo la kweli la yule dada... dadeki mi kidume najitosa kwa huyu dada liwalo na liwe!.....nikatoka pale niliposimama nikaelekea alipo yule msichana alipopiga magoti ili nikafanye yangu maana mrembo alitia huruma hatari......nikamfikia yule mrembo...mara mkaka mmoja akanishika bega...unajua alichonambia??
OYAA WE JAMAA UNAZIBA CAMERA WE HUONI TUNASHOOT FILAM HAPA..[emoji13][emoji13]

Pedeshe mmoja alikuwa kaamua kumtoa
mke wake ‘out’ siku ya Valentine.
Akampeleka Njenje, wakati muziki
unaendelea ghafla akapita msichana
mzuri sana akaja kuwasalimia, jamaa
akasimama akamsalimia kwa furaha, kisha msichana akaendelea na mambo
yake. Mke akamuuliza Pedeshee, ‘ Nani
yule?’ akajibiwa, ‘Yule ndie mchepuko
wangu’. Mke akawaka kama moto wa
kifuu. ‘Yaani unanambia bila aibu kitu
kama hicho? Mie nataka talaka yangu’. Pedeshee akajibu kwa upole, ‘Hakuna
tabu talaka ntakupa, ila ndio ukumbuke
hakuna tena sfari za Dubai wala China,
na utaanza kutegemea usafiri wa
Bodaboda’ Mke akapoa moto wake.
Wakati wakiendelea kununiana, ghafla akaingia rafiki yao akiwa na kimwana
pembeni. Mke akamuuliza Pedeshe,
‘Rafiki yako badala ya kuwa na mkewe
namuona na mwanamke ndie nani yule?’
Pedeshe akajibu, ‘Yule ndie mchepuko
wake’. Mke akacheka kwanza kisha akasema,’Haloooo mchepuko wetu mzuri
kuliko wa kwao au sio mume wangu’.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom