supermarket
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 7,453
- 10,952
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Mchaga aliamua kufungua bustani ya wanyama akafanya kiingilio 10,000/= hakuna aliyeingia akashusha 5,000/= pia hakuna aliyeingia akashusha tena 2,000/= hakuna aliyeingia akashusha 1,000 pia hakuna aliyeingia akaamua kufanya bureeeee watu wakaingia na walikua wengi mno akafungulia Simba mmoja akafanya bei ya kutokea nje ni 20,000/=@
ALIKUSANYA HELA KAMA MCHANGA!
*WACHAGA HATUPENDAGI UJINGA KABISA[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna Methali zimekwisha muda wake wa matumizi.
Mfano:
1. Mwenzako akinyolewa tia maji.
_Siku hizi tunanyoa kwa mashine. Ukitia maji zinateleza hazinyoleki.
2. Barua ni nusu ya kuonana.
_Siku hizi watu wanaonana kwa watzap. Mkingojea barua mtakufa bila kuonana.
3. Akili ni nywele.
_Vipi kuhusu Mawigi?
4. Mchagua jembe si mkulima.
_siku hizi tunatumia zaidi matrekta ya kukodi.
5. Alalae usimuamshe akiamka utalala wewe
_siku hizi unaweka alam mwenyewe unaamka husubiri kuamshwa na mtu.
6. Polepole ndio mwendo
_siku hizi kuna mwendo kasi ukienda polepole utabaki.
Hatupendi mambo ya kizamani[emoji1][emoji1]
ahahah nimerudi tena kwa uzi juu nivunje mbavu mie.Nimemtembelea rafiki yangu nyumbani kwake mida ya saa saba hivi na tayari alikuwa karibu kusonga ugali.
Nikamuwahi wakati alitoka nje, nikaongeza maji kwenye sufuria kumbe sikujua alipima maji kulingana na unga uliobaki.
Sasa hivi tunakunywa uji hatuongeleshani.
Kumbe wote hatupendi ujinga...!![emoji23] [emoji23] [emoji23]