Whatsssssss!!!!!!!!!????

Whatsssssss!!!!!!!!!????

Siku moja nimeTuliaa LightHouse pale naskizia kibreezz! Mara akapita kidemu toto Heluwaaa! Nikasema simuachi.. nikatoa noti ya 10000 nikaandika namba zangu angu (07582000***) halafu nikamuita pphsss phsss! Mrembo umeangusha pesa, yule demu akaichukua pesa hata hakuisoma, mara hajafika mbali namuona anainunulia Mihogo. Alinisunyaaaa!!! ANYWAYYY hiyo haikua shidaaaaa. Shida ni Yule jamaa wa Mihogo ananisumbua daily alifikiria mm ni yule Demu !! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
KOMA😀
 
Umenyonya matiti ya mamako miaka miwili hujampa kitu chochote mpaka sasa ila umenyonya ya kademu kako kwa miezi mitatu na haitoi maziwa na umemnunulia iphone 7
[emoji117]wanaume tupendaga ujinga
[emoji12][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]
 
MTALII: Do you have vegetables here.
MTAFSIRI: Mnavyo vijimeza hapa.
WAITER: Vijimeza vidogo hatuna.
MTAFSIRI: No sir, they don't have.
MTALII: OK, fine, do you have hot dogs.
MTAFSIRI: Sawa, je mnao mbwa wa moto.
WAITER: Loh! Bwana we, hatupiki mbwa hapa.
MTAFSIRI: They don't cook here
MTALII: What type of snacks do you have here.
MTAFSIRI: Aina ngapi ya nyoka mnao hapa,
WAITER: We bwana we hapa hatupiki aina yeyote ya nyoka, mwache akale nyumbani kwao.
MTAFSIRI: They don't cook any type of snacks here, maybe you can go back and eat at home.
MTALII: OK, at least give us a cocktail juice.
MTAFSIRI: OK, tupatie hata juisi ya mkia wa jogoo.
WAITER: Hebu tokeni na bangi zenu hapa, tena
sasa hivi kabla sijakasirika.
MTAFSIRI: Lets get out of here
Muhudumu hapendi ujinga[emoji12][emoji13]
 
MWALIMU: kwanini umechelewa?
MWANAFUNZI: kuna mambo yangu nilikua nafanya
MWALIM: mpuuzi wewe, hivi shule na mambo yako kipi bora??
MWANAFUNZI: ticha nikaushie
MWALIM: nakuuliza unanijibu hivyo!! Njoo hapa, Piga magoti
MWANAFUNZI: poa tu
MWALIM: Kwanza unaitwa nani, darasa la ngapi?
MWANAFUNZI: Juma Scorpion la Saba D
MWALIM: sawa wewe utafaulu nilikua nakutania tu ingia darasani [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna dada mmoja alichumbiwa na watu wanne
1.msanii
2.mvuvi
3.mwindaji
4.doctor .
Siku moja dada huyo alienda mtoni kufua ghafla alitokea mamba akamchukua akazama nae majini palepale msanii akatunga wimbo akaanza kumwimbia mamba akatokeza kichwa juu,palepale mwindaji akampiga risasi mamba akafa na dada alibaki akitapatapa ndan ya maji palepale mvuvi akaogelea kwenda kumuokoa akamleta nchi kavu palepale doctor akamtibu majeraha mpaka akapona.
Swali linakuja je ni nani anayestahili kumuoa kati ya watu hao wanne?
NIJIBU KWA MAANA SIPENDAGI UJINGA[emoji12][emoji13]
 
ASKOFU alipitisha Kanisani Mchango wa Kuchangia Ujenzi wa KANISA,waumini Wakatoa Tshs 35,000/= tu.
Ghafla Majambazi Wakaingia Wakaliteka KANISA na Kuamrisha kila Mtu atoe alichonacho Mfukoni, Wakakusanya Tshs Milioni 8, laki 2 na senti 50, Baadaye wakamkabidhi ASKOFU ili aendeleze Ujenzi wa KANISA. [emoji12][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dada zangu muwe mnakagua hand bag zenu asubuhi kabla ya kutoka nyumbani. Panya kachomoka kwenye handbag ya Dada mmoja kwenye daladala. Tafrani basi zima karibia dereva asababishe ajali, konda karuka huyo.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimeumwa na jino moja la chini, nimeng'oa meno yote ya chini ili iwe funzo kwa meno ya juu.
Sipendagi ujinga mimi[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Leo mchana nimewakuta vipofu wawili wakipigana
Basi nikapaza sauti na kusema ninamsapoti huyo aliye na kisu.
Ghafla wote wakaanza kukimbia mmoja kule mwingne huko. Ila hakuna aliyekuwa na kisu
Huwa sipendagi ujinga mimi[emoji23][emoji23]
 
Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem'bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika "NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU"
Mpaka sasa tumemwacha bado hajapata msaada.
Hatupendagi ujinga sisi[emoji12][emoji13][emoji13]
 
Nilikutana na mshikaji wangu Tandika stendi ya mbagala, akanistua kwa nyuma akisema "malogy mathematic ndio wewe? upo kaka?". Nikamjibu nipo kiongozi tunasindikiza wenye maisha yao, akacheka sana, Mara akaanza kuzungumizia
matatizo ya familia yake, nikamwambia tuyaache hayo mimi mwenzako nimepitia makubwa,
aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake,
NIKAMSTOPISHA nikamwambia " Unadhani familia yako ina matatizo?" Basi sikiliza kisa changu hiki….
"Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa tu, mimi na huyo mjane tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu ambae alikuwa mkiwa baada ya kufiwa na mama kitambo tu akaamua kumuoa binti yangu wa kambo (yaani binti wa huyu mke wangu niliyemwoa akiwa mjane), hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe wa mkwe wake.
Baadaye binti ya mke wangu yaani binti yangu wa
kambo (ambaye kwa sasa ndiye mke wa baba yangu na hivyo kuwa pia mama yangu wa kambo)
alipata mtoto wa kiume. Mtoto huyo wa kiume
akawa mdogo wangu kwa sababu tulichangia baba mmoja. lakini kwa vile pia alikua ni mtoto wa binti wa mke wangu papo hapo akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake huyo mdogo wangu.
Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa msichana (yaani binti ya mke wangu ambaye pia ni mke wa baba yangu) ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake na mwanangu (mwee!!). Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kuwa shemeji wa mtoto wangu (achilia
kuwa babu yake!!) ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wa binti yake mwenyewe . Mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe.
Kabla sijammalizia jamaa akaondoka
Mimi sio mtu wa mchezomchezo
*Sipendagi Ujinga [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa Kaenda Kuiba Mbuzi Usiku Wa Manane Aliporuudi Nae Akamfunga Nje Ya Nyumba Yake,
Asubuhi Wenye Mbuzi Wanatafuta Mbuzi Wao Wakamkuta Nje Kwa Jamaa Wakamgongea Hodi Kumuamsha Jamaa
Jamaa Akauliza Nani Nyie? Wakajibu Sisi Wenye Mbuzi Mnasemaje?Tumemfuata Mbuzi Wetu Akajibu Si Huyo Hapo Nje Mumchukue Kwani Mimi Nilivyokuja Kumchukua Niliwaamsha [emoji12][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa alikuwa kwenye daladala pembeni kuna dada mrembo kakaa. Kamlia timing kwa muda kisha halafu akamuuliza JAMAA: Samahani dada unaitwa Google?
DADA: hapana, kwanini umedhani naitwa hivyo?.
JAMAA: "Una kila kitu nnachokitafuta [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
DEMU: Gud mornie bebi..
JAMAA: poa
DEMU: eti unaijua nyimbo ya SALOME?
JAMAA: ndio
DEMU: naomba niimbie kidogo naipenda.
JAMAA: salome juu ya kaburi lako naliaa ahaha kilio unakisikiaa..
SIO KWAMBA HAKUMWELEWA, ILA JAMAA HAPENDAGI UJINGA [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
DOGO: shkamo bro
KAKA: marahaba mambo
DOGO: mambo sio mabaya sana
KAKA: kuna mpya?
DOGO: ndiyo, waif kajifungua leo asubuhi na mimi nilikuwa sijajiandaa kabisa. Naomba nosaidie kama laki 1 hivi, samahani kwa usumbufu
KAKA: dogo kwani mimba umpe jana jioni huyo mkeo? kama wewe umeshtukizwa kwa miezi 9, basi mimi nitakupa hiyo laki baada ya miezi 18.
Sipendagi ujinga [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa mmoja alialikwa katika harusi. Akafika mlango wa 1 umeandikwa kulia ni ndugu wa maharusi, kushoto ni wageni waalikwa, akaenda kushoto maana yeye alialikwa. Akakuta mlango wa 2 umeandikwa kulia wenye zawadi kushoto wasio na zawadi, yeye hakuwa na zawadi.
Mlango wa 3 umeandikwa kulia wanawake kushoto wanaume, akapita kushoto akajikuta ametokea nje mtaani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
DEMU: mambo
THOBY: poa mzima?
DEMU: me mzima sema nina shida
THOBY: shida gani tena
DEMU: nimekuwa mnene sana sana halafu nina mafuta mengi sana mwilini, nifanyaje yaishe?
THOBY: fungua sheli [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23]
 
MAMBO YA FEDHA

Kuna jamaa alipewa shilingi 9836287636 ...acha uvivu, najua hujasoma ni kiasi gani hicho cha fedha na mbaya zaidi hujagundua kwamba katikati ya namba hizo kuna herufi A...safi sana, najua umeangalia tena kuiona hiyo herufi, bahati mbaya hujaiona.[emoji12][emoji12][emoji12][emoji12]

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hii kweli supa market[emoji119]
 
Back
Top Bottom