JERO: Ulikua wapi ndugu yangu, mbona huonekani.....?
ELFU KUMI: Daah ndugu yangu mwenzio nazunguka tu kwa kutumia "wallet" na "ATM", mara nimeingia Bar, mara Casino, juzi nlikua Uwanja wa Ndege nikakaa sana pale kisha nikaenda Mlimani City nikatoka nikaenda Holiday Inn kisha nikachukuliwa nikapelekwa Masaki, vipi wewe pande zipi.?
JERO: Looh, mwenzio kila siku kwa Mama Ntilie, muuza mkaa, nikibadili kiwanja labda utanikuta kilabuni.
ELFU KUMI: tafuta wenzako 19 ili muwe kama mimi, mwenzako namsubiri pedeshee yeyote twende zetu serena hotel [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23]