Whatsssssss!!!!!!!!!????

Mjinga mmoja alimwambia rafiki "unaonaje nikachukua likizo mwezi mmoja na wewe mwezi mmoja tukasafiri likizo miezi miwili? [emoji12][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]
 
Bounsa alipelekwa kufungwa gerezani, alipofika akaanza kutishia wafungwa, ''nasikia huku mnatabia ya kuwachezea kimaumbile wanaume wenzenu, jaribuni kama mnataka kifo ''kwa masifa akapiga ngumi ukutani, akapiga tena ukuta kwa kichwa, si akazimia,baada ya mda alipozinduka anashangaa ha? hasira hasara [emoji12][emoji13][emoji13][emoji13]
 
Jamaa alikuwa kila akienda baa anaagiza bia mbili2 na kunywa zote kwa pamoja.
MHUDUMU: inakuwaje kila ukija unaagiza mbilimbili kwa wakati mmoja?
JAMAA: huwa nakunywa na rafiki yangu sasa yeye kafariki namywea na zake. ikafika kipindi akawa anaagiza moja moja!
MHUDUMU: imekuwaje tena?
JAMAA: ahaa mimi nimeacha pombe sasa namsaidia huyu rafiki yangu. [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mwenye watoto 10 atapewa zawadi ya tshs milioni 10
Baba 1 mwenye watoto 9 akamuita mkewe na kumuomba samahani kuwa ana mtoto wa nje 1 hivyo akamchukue ili kutimiza idadi wanyakue donge nono, mkewe akakubali na jamaa fasta akaenda nyumba ndogo kumchukua mwanae, aliporudi home akakuta nyumba nyeupee kumuuliza mkewe watoto wako wapi mkewe akajibu "baba zao wamekuja kuwachukua" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa mmoja wakati amemsimamisha dada mmoja na wakati akimtongoza bahati mbaya/nzuri naniliu yeke ndani ya zipu si ikasimama.
Jamaa alichoamua baada ya hapo ni kuitoa nje na kuiambia "haya tongoza wewe mwenyewe na haraka zako" [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
DEMU: ninunulie pizza plz
JAMAA: una boyfriend?
DEMU: ndio ninae, kwann umeniuliza
JAMAA: umeshawahi kusikia wafanyakazi wa Tigo wanalipwa na Airtel?
DEMU: eeeeh yamekuwa hayo[emoji15][emoji15]
 
Dogo janja alimpa karatasi nyeupe mwalimu wake..
MWALIMU: mbona hujachora?
DOGO: nimechora ng'ombe anakula nyasi..
MWALIMU: (embu angalia hii karatasi haina kitu)
Hizo nyasi ndo ziko wap?
DOGO: ng'ombe amekula zote..
MWALIMU: ng'ombe yuko wap?
DOGO: ameshaondoka kwasababu hakuna tena nyasi za kula. [emoji12][emoji13][emoji13][emoji13]
 
Chizi 1 alitoka hospitali baada ya akili kuwa sawa wakamfanyia sherehe, baada ya nusu saa yule chizi akaingia stoo, akachukuwa panga akamfata baba yake na kuanza kumfukuza..dingi katimua mbio majiran wote wakashika vichwa wakijua mzee lazima atauliwa.
Dingi kakimbia hadi akadondoka ile anainuka tu chizi huyu hapa.
Chiz akampa panga baba ake akamwambia na wewe nikimbize. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa 1 kaikoleza bangi kisawa sawa, ikamtuma avue nguo zote, akaenda kwenye kioo akajiona kama amevaa suti, akatoka akaenda kwa wenzake, akawauliza vipi washkaji suti imenitoa? mmoja akajibu imekutoa sanaaaa mwanangu ila Tai umeifunga chini sana..!!!!! [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
MTEJA: Huyu kasuku simtaki anatukana sana.
MUUZAJI: Nitakupa mwingine mwenye uwezo wa kuongea lugha nyingi.
MTEJA: Anaongea lugha ngapi?
MUUZAJI: Mbili!
MTEJA: Ipi na ipi?
MUUZAJI: Kingereza na
Kifaransa,akinyanyua mguu wa kulia anaongea kingereza, akinyanyua wa
kushoto kifaransa!
MTEJA:Akinyanyua yote kwa pamoja anaongea lugha gani?
KASUKU: mwendawazimu mkubwa wewe, SINTAANGUKA, EBOH!!!!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
kipofu na mlemavu wa miguu walikuwa wakitembea pamoja, mara gari ilipokuwa ikipita ikawakanyagia maji, mlemavu wa miguu akasema ngoja nilikimbize gari niwakamate, kipofu akadakia "kausha mwana nilishasoma namba"[emoji12][emoji13][emoji13][emoji13]
 
MCHAGA NA MMAKONDE wanabishana kusema neno SUZUKI.
MCHAGA: ni Thudhuki babaa angu.
MMAKONDE: umekocha ni chuchuki"!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa mmoja alikua muongo muongo sana! Siku moja kakaa maskani na washkaji zake akawa anawahadithia...

"Baba yangu ni muwindaji,kuna siku alimuua Swala mkubwa kama ile Nyumba" huku akiwaonyesha wenzake nyumba kubwa kiasi iliyokua karibu na maskani yao,

Ghafla jamaa mwingine nae akarukia..

"Na mimi baba yangu alikuaga ni fundi wa kuchomelea "welding" kuna siku alitengeneza sufuria kubwa kama hiyo nyumba" nae akionyesha ile ile nyumba iliyofananishwa na ukubwa wa Swala na yule jamaa muongo muongo,

Yule jamaa muongo muongo akarukia..
"Acha uongo,baba yako alitengeneza sufuria kubwa kiasi hicho? Halafu sufuria kubwa lote hilo la nini sasa?

Yule mtoto wa "fundi wa kuchomelea" akamjibu yule jamaa muongo muongo .....

"Hilo sufuria alilotengeneza baba si la kumpikia yule swala mkubwa kama nyumba aliyeuawa na baba yako"

Jamaa muongo muongo akaondoka maskani bila kuaga na ndio ukawa mwisho wake wa kuongopea watu.
 
Umetisha mkuu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Jana niliamua kuchukua hatua muhim Sana maishani ya kwenda kupima ukimwi,kitu ambacho wengi wenu mnaigopa sanah.Hapa nimerudi na furaha tele baada ya kukuta clinic imefugwa.
Sipendagi ujinga mimi[emoji23][emoji23][emoji23]
 
MWALIM: Nitajieni madini mnayoyafahamu na yanapatikana hapa Tanzania.
MWANAFUNZI: maromani, masabato, malokore, maisilamu, Maluteri, maA.I.C, maEAGT.

WANAFUNZI HATUPENDAGI UJINGA[emoji23][emoji23]
 
Wanaume wa ukweli, siku ya meeting huenda hotelini mapema na kukutana na waiter na kumuambia "nikija na demu hata Kama Kuna Kila kitu ww Mwambie Kuna maandaz na chai tu.
Hatupendagi ujinga[emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtanzania, Mnyarwanda, na Mkenya walikamatwa na madawa ya kulevya China. Wakaambiwa adhabu ni mbili kifo au adhabu nyingine ambayo wakiishindwa pia wanauawa. Wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao. Wakapelekwa msituni wakaambiwa waingie msituni kila mmoja kwa njia yake halafu kila mmoja arudi na matunda 10 ya kufanana. Wakaingia msituni kila mtu njia yake.
WA 1: Mnyarwanda akarudi wa kwanza. Karudi na ma apple 10. Akaambiwa adhabu ni kumeza yote mazima mazima moja baada ya jingine bila kufunga macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa! Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili akashindwa kuvumilia akafunga macho. Akapigwa risasi akafa.
WA 2: Mkenya akaja ana Straberry 10. Akaambiwa masharti. Akaanza kula bila kufunga macho wala kulia wala nini. Alipofika cha 9 akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.
Wakiwa kuzimu Mnyarwanda akamuuliza Mkenya.
MNYARWANDA: vipi wewe mbona ulishindwa kuvumilia wakati ulibakisha tunda kimoja tu?"
MKENYA: kaka, nilishindwa kuzuia kicheko kwa maana nilimuona mtanzania kaja na mananasi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Me too nimecheka sana[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23][emoji23]
Nikiwa na stress tu nakuja kupitia huu uzi wako.
--vichekesho karibu 1,000, kila siku sivimalizi nacheka mpaka basi, leo ndo nimemaliza. [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
*Tukutane MMU na jukwaa la celebrities nakusubiri[emoji6]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…