supermarket
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 7,453
- 10,952
Mjinga mmoja alimwambia rafiki "unaonaje nikachukua likizo mwezi mmoja na wewe mwezi mmoja tukasafiri likizo miezi miwili? [emoji12][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umetisha mkuu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Jamaa mmoja alikua muongo muongo sana! Siku moja kakaa maskani na washkaji zake akawa anawahadithia...
"Baba yangu ni muwindaji,kuna siku alimuua Swala mkubwa kama ile Nyumba" huku akiwaonyesha wenzake nyumba kubwa kiasi iliyokua karibu na maskani yao,
Ghafla jamaa mwingine nae akarukia..
"Na mimi baba yangu alikuaga ni fundi wa kuchomelea "welding" kuna siku alitengeneza sufuria kubwa kama hiyo nyumba" nae akionyesha ile ile nyumba iliyofananishwa na ukubwa wa Swala na yule jamaa muongo muongo,
Yule jamaa muongo muongo akarukia..
"Acha uongo,baba yako alitengeneza sufuria kubwa kiasi hicho? Halafu sufuria kubwa lote hilo la nini sasa?
Yule mtoto wa "fundi wa kuchomelea" akamjibu yule jamaa muongo muongo .....
"Hilo sufuria alilotengeneza baba si la kumpikia yule swala mkubwa kama nyumba aliyeuawa na baba yako"
Jamaa muongo muongo akaondoka maskani bila kuaga na ndio ukawa mwisho wake wa kuongopea watu.