Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Tahadhari! Mwandishi wa Uzi huu amejikuta anajiuliza yeye Ni Nani baada ya subconscious mind kuleta kumbukumbu kadhaa katika Maisha yake, kwahiyo anawaza Kwa sauti kubwa!!!
Nikiwa shule ya msingi nadhan Darasa la tano au la sita, wanafunzi wenzangu waliniambia huwa wanamuona Baba yangu kwa binti mmoja hivi, ingawa mpaka sasa hivi ninavyoandika ni mama yangu mdogo kwa maana aliolewa mke wa pili na Baba. Kwa umri ule ingetarajiwa ningeenda straight kumwambia mama au mtu mwingine yoyote Yule lakini sikufanya hivyo kabisa na hii Siri ndio naitoa Leo
Najikuta najiuliza WHO AM I
Kuna kipindi miaka ya 2003/4 nilienda na girlfriend wangu club, akaniaga anaenda washroom, akachukua Mda kidogo kurudi nikasema ngoja nitembee kidogo pale ukumbini,dah nikamuona ameshikwa makalio na mwamba kama wanakiss hivi. Nikapita kimya hakuniona, sikumuuliza chochote na tuliendelea Kula gudtime, nilikuja kumwambia siku nyingine kabisa, akabaki anajikanyaga Tu.
Najiuliza WHO AM I
Kuna kipindi nilikuwa na kirukuu / suzuk carry, nikampa jamaa mmoja aniletee hesabu,kumbe nae anatoa deiwaka bwana, aliyepewa deiwaka akapata ajali na alikuwa hajui gari vizur, nikaingia gharama na hasara Kwa matengenezo, huwezi amini jamaa hakuwahi kuomba msamaha hata kidogo, hakuonyesha kusikitika hata Kwa kinafiki, ni jamaa kutoka ilikodondoka Ile ndege hivi majuzi, nikajua huenda ni hulka zao, sikusema chochote wala kulalamika Kwa yeye kutoomba msamaha.
Najiuliza WHO AM I
Unaweza kunitukana au kunitamkia maneno ya hovyo hovyo nikakuangalia Tu na kujifanya kama hakuna kitu kilichotokea, na siweki kinyongo Rohoni
Najiuliza WHO AM I
Nahisi hata kama siku ikija kutokea Nikamfumania mama watoto wangu ingawa sipendi wala kufikiria kuja kutokea, sitarusha ngumi au kuleta fujo kwa yeyote yule isipokuwa kumpa talaka Tu Kwa roho Safi.
Najiuliza WHO AM I
Natambua kuna baadhi ya watu baada ya kusoma Uzi huu watakuja na comment za kejeli na matusi na Maneno ya ovyo ovyo lakini sitawajibu chochote kile na wala sitakwazika.
Najiuliza WHO AM I
Kutoka kwangu ETUGRUL BEY
Ni hayo Tu!