WHO inatakiwa izijibu hoja za Rais Magufuli kwa umakini mkubwa. Tropical diseases kama TB, Malaria kwanini hazina chanjo na zinaua sana?

WHO inatakiwa izijibu hoja za Rais Magufuli kwa umakini mkubwa. Tropical diseases kama TB, Malaria kwanini hazina chanjo na zinaua sana?

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2019
Posts
1,521
Reaction score
4,381
Shirika la Afya Duniani ni kibara na chombo muhimu cha kutekeleza Sera za mabeberu moja wapo ya ajenda muhimu ya mabeberu ni kuitawala mifumo ya Dunia kwa ku-centralize mamlaka ili hii sera ifanikiwe ni lazima kwanza wajiimarishe kichumi waendelee kuwa superpowers na ili waendelelee super powers ni lazima wawazime incoming super powers system?!

Katika kutekeleza Sera yao ni lazima waue nguvu kazi ya wanyonge wao lzm waue uwezo wa kufikiria wa wanyonge wao ni lzma watengeneze mazingira nyonyaji kwa wanyonge wao.

Ndio maana sasa Ukimwi hautakaaa uishe malaria Tb nk lengo to control our reproductive potential.
 
Yaani!tatizo letu waafrika kila tatizo linalotukabili , tunamsingizia mzungu!!wakati matatizo mengi chanzo ni sisi wenyewe, tunajiamini tuna wasomi wengi, barani afrika, wameshindwa kuungana, kwa kupata ufadhiri wa nchi za kiafrika, na kutafuta chanjo ya ukimwi?

Hao incoming superpowers wako afrika?ambako viongozi wake ni warafi kupita kiasi, wao matatizo ya wananchi sio kipaumbele chao!!yaani miaka 60 toka uhuru hadi leo kiongozi anakuja kukuahidi maji safi?!!tumekubaliana mfumo wa demokrasia, lakini viongozi hawaheshimu maamuzi ya wananchi.

Hao wazungu wakisema inakuwaje wanapewa majina mabaya!!ila huyo huyo akikupa msaada jina linabadirika, hata vita vinavyoua watu wengi barani Afrika, chanzo kikubwa sio wazungu, ni ubinafsi tu wa viongozi wetu , humo ndio wakati mwingine wazungu wanajipenyeza!
 
Kuna chanjo inaitwa BCG ambayo ni chanjo ya kifua kikuu na watoto wachanga wote wanachanjwa... au TB na kifua kikuu ni tofauti?

Njia kujikinga na malaria zinajulikana na pia inatiba. Na kukosa chanjo ya magonjwa mengine haimaanishi basi na hili lisipatiwe solution. Mbona hatuachi kupokea dawa za ukimwi mkasema kwa kua haziponyeshi basi zisitumike? Lakini zinasaidia kufubaza na leo mwenye ukimwi anaeza ishi na asiyenao na asimuambukize.

Kifua kikuu kina tiba na mtu akianza kutumia dawa hakiambukizi tena huwezi fananisha na korona. So yes chanjo inaweza saidia wale ambao hawana maambukizi kutokupata means rate ya watu kuugua itashuka sawa na pandemic diseases zote lazma itafutwe njia ya kupunguza maambukuzi then huko mbele studies nyingine zikifanyika zitaweza kuleta majibu bora zaidi.

Usiombe ikakukuta, utakua wa kwanza kwenda kupanga mstari. Iliku huwezi kusafiri mpk uwe umepata chanjo ya yellow fever, mbona hamhoji hizo??
 
Kwani wameanza kicontrol dunia leo? Endelea kutega masikio usijilinde wewe na familia yako endelea kusikiliza mtu anayeangaliwa afya yake anakula nini ameamkaje, na vitu vingine vingi wewe na Mimi kajamba nani ....... Check up ulifanya lini kama si ulivyokuwa unaingia first year au form one....
 
Sasa kwa nini msitengeneze hizo chanjo?

Mnangoja mabeberu wawatengenezee halafu mseme chanjo si nzuri ni za mabeberu hamzitaki?

Gonjwa la Malaria ni la kwenu tropiki, unataka kutengenezewa chanjo na watu wa Ulaya na Marekani?
 
Kwani Polio, Surua, pepopunda zilizoisumbua dunia Zina chanjo au hazina?
Hawasomi hata kujua haya magonjwa yaliyosumbua dunia yalianzaje... yaliweza kupunguzwa vipi na mengine kutokomezwa kabisa. Yaani wengi wao wamechomwa sindano za ndui na homa ya manjano lkn wako wanaropoka ropoka hapa bila hata kuelewa. Yaani mara 10 hata wangekua wanaelezea labda side effect ambazo zinaweza kutokea na zikaleta madhara ningewaelewa.
 
Acha kukurupuka!Aliekuambia kuwa Malaria haina chanjo ni nani?Unafikiri ya kuwa kila anachoongea Magufuli ni fact?Magufuli ni MATAGA tu kama yalivyo MATAGA mengine,yaani kukurupuka!Kwa taarifa yako Malaria ina chanjo na pia kifua kikuu nayo ina chanjo!Uwe unafanya kwanza literature review kabla ya kuleta mada hapa.Siyo kila analosema Magufuli ni sahihi.Magufuli ni nasty leader ambae huwa hajui hata huwa anaongea nini!Huwa anaongea upupu kama mtoto mdogo alievaa pampasi.
6543.jpg
 
Moja ya nguzo tano za medical ethics ni ‘autonomous’ haki ya mgonjwa kuchagua aina ya matibabu given the options.

Jukumu la Dr ni kukuelezea ugonjwa wako na madhara yake katika mwili na dawa sahihi and other available options.

Swala la kukubali tiba ni lako mwenyewe awawezi kukulazimisha kutumia dawa mtu mwenye akili zako timamu (huo ndio utaratibu nchi za wenzetu).

Pamoja na kwamba awawezi lazimisha mgonjwa kufuata tiba, wana elewa pia kuna ‘psychological barriers’ kama sababu zinazochangia kwenye maamuzi ya kukataa tiba zikiwemo misinformation kuhusu hizo dawa, woga usio na uthibitisho wa side effects za dawa, woga wa kuchomwa sindano etc; na excuses huwa kama zile alizozitoa Magu (ata huko makwao wana changamoto hizo).

Kazi ya wataalamu pia ni kuhakikisha wanajaribu as much as possible to change the mind set ya mgonjwa pale inapowezekana kupitia elimu.

Kwa ivyo ni jukumu la wizara ya afya na wataalamu wake wa maswala ya madawa, virus infections, etc kuongoza hii vita kwa namna sahihi; ata kama nchi aitaki lockdown kumuendekeza Magufuli kwenye kila kitu wakati hiyo sio fani yake kutaleta madhara.

WHO wameshawaambia portion ya Tanzania ipo na hizi chanjo sio trial ni medical approved by science.

Ila tukumbuke tu WHO awawezi tulazimisha kuchukua in respect of medical ethics. Si ajabu tamko lao ni kwenye kujitoa kimaso maso tu mbele ya dunia maana demand ni kubwa.

Kwanini WHO watoe kauli yao one day baada ya speech. If you ask me tukatae wapeleke kwingine zinakohitajika baadae kama ikitokea mambo yakaenda mrama Tanzania wawe na ushahidi they did their part but we refused their services.
 
Kuna chanjo inaitwa BCG ambayo ni chanjo ya kifua kikuu na watoto wachanga wote wanachanjwa... au TB na kifua kikuu ni tofauti?
Umegusia jambo kubwa la chanjo ya BCG, hawa wenzetu wa mtaa wa Lumumba kazi yao kusikiliza na kurudia kauli za viongozi wa serikali ya CCM Mpya bila kuhoji au kuwaza.

Wanadai kuwa kiongozi mkubwa hakosei na ana taasisi ya Urais inayompa taarifa sahihi. Lakini kuna chanjo kibao naongezea chanjo zinazotunusuru na ulemavu wa Polio .
 
Back
Top Bottom