Halaiser
JF-Expert Member
- Apr 3, 2014
- 4,230
- 6,653
Mkuu naomba niongezee kidogo. Suala la Malaria linafahamika. Chanzo na kuenea kwake na madhara yake kunaeleweka vizuri tu. Hatuhukui tahadhari wala hatahangaiki kupambana nao ni pale tu Wazungu wanapotoa misaada. Watu wamegaiwa neti wao wanakwenda kuzungushia kwenye mboga zao dhidi ya kuku. Yaani mboga ni muhimu na ni kipaumbele chao kuliko afya zao. Wengine wamefunga neti lkn wavivu kuzishusha. Mambo ni mengi ktk hilo lkn eti Phd holder wa Sayansi anajitokeza hadharani kulalama juu ya uwepo wa Malaria. Mlitaka Wazungu waje wawashushie au kuwafugia neti usiku mlale?? Kwa hawa wenzetu walishatokomeza Malaria kwa miaka mingi.Yaani!tatizo letu waafrika kila tatizo linalotukabili , tunamsingizia mzungu!!wakati matatizo mengi chanzo ni sisi wenyewe, tunajiamini tuna wasomi wengi, barani afrika, wameshindwa kuungana, kwa kupata ufadhiri wa nchi za kiafrika, na kutafuta chanjo ya ukimwi!!?
Viongozi wetu wamejawa na uroho wa Madaraka na wala hawana hata chembe ya Uzalendo ila hutumia neno lile ili kuwalaghai raia waweze kuwatawala.
Viongozi wengi wa Kiafrika hununua silaha za kivita kwa Wazungu siyo kwasababu kuna vita bali kuwaangamiza raia wao wenyewe ili waendelee kuwanyonya halafu wanakimbilia kuwalaumu Wazungu.
Shule hadi leo hazina madawati na tunajigamba tuna misitu ya kutosha lkn hatuhangaiki kujitatulia tatizo hilo kwasabu Viongozi wetu wanataka magogo yauzwe nje ili wanunue slaha za kuwalinda na kuwaangamiza Wakosoaji wao. Upuuzi huu tunawasukumia Wazungu kuwa ni Wanyonyaji.