WHO inatakiwa izijibu hoja za Rais Magufuli kwa umakini mkubwa. Tropical diseases kama TB, Malaria kwanini hazina chanjo na zinaua sana?

Ufahamu duni! Unaelezwa ya magonjwa na chanjo na dawa wewe unarukia condom, ili iweje. Zinakusaidia sana?
Eti unaletewa na mzungu. Mzungu yupi? Ukimuona mzungu yeyote unamuona ni mkombozi, mkombozi wa nini? Yani mzungu mmoja akifanikiwa race nzima unaipa sifa!
 
Unalaumu taasisi za kimataifa kufanya corona politics wakati wewe unafanya kitu kile kile.

Moja ya sababu kubwa za western medicine kupewa kipaumbele ni uwazi. Wao wanafanya kila kitu kwa uwazi from research to approval of medicine and the whole process is open for scrutinisation as it evolves.

Kuna dawa si miaka mingi nyuma at clinical trial in UK kuna mtu alikunywa vidole vyake vya mikono vikauka ikabidi baadhi vikatwe na watu kadhaa kwenye hiyo trial waliathirika, hilo swala lilichukua headlines so things do go wrong sometimes.

Lakini hadi dawa kuruhusiwa kuuzwa it has gone through enough open scrutiny from external regulators before being approved by independent body.

China na Russia hawana utaratibu huo mchakato wao aupo wazi ndio maana inakuwa ngumu kupewa endorsement ya dawa zao haraka.

Hata swala la COVID lenyewe how it’s handled huko ulaya kuna viongozi walikuwa wana mtazamo kama wa Trump na wananchi wengi wamechoka lockdown; tatizo viongozi wao awawezi kwenda kinyume na ushauri wa kisayansi unaotolewa na wataalamu wao na WHO.

Swala la Africa kupewa vaccine sio kwa mapenzi ya wazungu kwetu; ni WHO ndio walio fight wakati research zinaanza tu kutaka chanjo zikipatikana nchi maskini nazo zisaidiwe sio chanjo zote zinunuliwe na nchi tajiri.
 
Mkuu kwa uelewa wangu finyu, chanjo uwa ni kwa magonjwa yanayosababishwa na virus, TB inasababishwa na bacteria, Malaria inasababishwa na plasmodium nacho siyo kirusi.
Chanjo ya UKIMWI itaptikana tu maana siyo kila ugonjwa hupatiwa chanjo mapema mengine yanawahi mengine huchukua muda. COVID -19 ni jamii ile ile ya virusi ya COVID kama MERS na SARS ambavyo tayari walikuwa na data zake na zimewasaidiakujua wapi pa kuanzia.
Sijawahi kusikia kama kuna chanjo ya ugonjwa usiyosababishwa na virus.
Siyo medical expert ni layman naweza kwua siko sawa.
 
Sasa kwa nini msitengeneze hizo chanjo?

Mnangoja mabeberu wawatengenezee halafu mseme chanjo si nzuri ni za mabeberu hamzitaki?

Gonjwa la Malaria ni la kwenu tropiki, unataka kutengenezewa chanjo na watu wa Ulaya na Marekani?
Ni kweli kaka.
Lakini what so far WHO wamefikia /kushauri juu ya hoja ya Mh.Magufuri juu ya magonjwa mengine kutokuwa na chanjo?
 
Ongeza Ebola. Jibu ni kuwa haiwasumbui wazungu. Laiti ingewasumbu wangeshatoa chanjo. Afterall ni biashara ya makampuni makubwa ya dawa
 
WHO ni nani ?, Na Tanzia ni WHO au sio WHO ?, Na kama Magonjwa haya yanasumbua sana nchi za Tropics / Africa Kwanini Waafrica wenyewe wasipate hio Chanjo ? Nyumba yako inaungua alafu unauliza kwanini maji hayakuja kuzima haraka moto ? Hapo unamuuliza jirani yako ambaye yeye ana shida ya mafuriko (cha kujiuliza wewe unatoa / ulimpa msaada kwenye mafuriko yake).

Food for thought...., walio-katika jitihada za kutafuta chanjo / madawa ni big pharmaceutical corporations they invest time and money (na sio kama njia ya sadaka) bali mwisho wa siku wapate return on investment ; Kampuni hizi sio wabaguzi wa rangi / bali they know only one color (i.e. Money).... they are there to make money in the end...,
 
Muulize mheshimiwa kwanini NIMRI haitafiti chanjo za maradhi yanayotukabili badala ya kusubirl wasioyapata watutengenezee chanjo.
 

Kwahiyo WHO wamjibu Magufuli kwani ni taasisi ya serikali ya Tanzania?
 
Well said mkuu [emoji120][emoji120] kwanza mimi hakuna kitu nachukia kama kulaumu wengine for my failure or my mistakes, Sana sana nitajaribu kuwa close na huyo mtu ili nijue amefanikiwaje na mimi nakwama wapi?? Kabla ya uhuru lawama ilikuwa ni kwa wakoloni, sasa bara zima la Afrika tuko huru bado lawama ni kwa wazungu, sasa wanaitwa mabeberu (mbuzi dume), sijui mbuzi jike ndiyo sisi au vipi yaani. Mbaya zaidi na sisi tunao wasomi na maprofesa lakini bado tumekomaa tuu kulaumu eti chanjo mbaya, mara dawa feki etc kwa nini sisi hatufanyi hizo tafiti sasa na kuja na chanjo zetu??
 
Sasa kwa nini msitengeneze hizo chanjo?

Mnangoja mabeberu wawatengenezee halafu mseme chanjo si nzuri ni za mabeberu hamzitaki?

Gonjwa la Malaria ni la kwenu tropiki, unataka kutengenezewa chanjo na watu wa Ulaya na Marekani?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji120][emoji106][emoji106][emoji106]
 
Umeongea vema sana mkuu. Mimi kinachonikera ni mtu mmoja kupangia watu 50 milioni, nina imani kabisa kuna watu wako tayari kupata hiyo chanjo ili iwanusuru na hili balaa but kwa sababu za kutafuta ujiko wa kisiasa watu watakosa hii chanjo.
 
Ujinga ni mzigo kweli. Je, umewahi kusikia ugonjwa unaosababishwa na Bacteria wenye Chanjo? Au protozoal disease yenye Chanjo? Chanjo ni kwa viral diseases tuu ambazo kutokana na complexity ya virus, inakua ngumu kutengeneza specific drug itakayokua effective kwq watu wote. Rejea mfano wa virus wanaosababisha mafua (Influenza and respiratory sysintial virus, pamoja na kuwa wamegunduliwa kitambo Hadi kesho hawana dawa, Ila Chanjo tuu.
 
HAPA NI JAMBO LA FOCUS TU.

UMEWAJIULIZA KWANINI! WAGANGA WENGI WA KIENYEJI (JADI) WANAFOCUS tiba ya "Nguvu za Kiume "tu ? 🤣🤣🤣😁

Wakati Luna magonjwa mengi? Mfano.
1.Macho
2.Ukurutu
3.Usubi
4.Pumu.....to mention few!

MKUU WAO KIPAUMBELE CHAO NI KINGA YA CORONA KWA SASA.😃😃😁😁🤣🤣
 

Attachments

  • images (2).jpeg
    29.5 KB · Views: 1
Umeongea vema sana mkuu. Mimi kinachonikera ni mtu mmoja kupangia watu 50 milioni, nina imani kabisa kuna watu wako tayari kupata hiyo chanjo ili iwanusuru na hili balaa but kwa sababu za kutafuta ujiko wa kisiasa watu watakosa hii chanjo.
Ni Tanzania tu raisi wa nchi anaweza waongoza medical professionals katika taaluma yao na wakamuachia. Kwingine kote kiongozi akijaribu anajibiwa bila ya uoga.

For the most part Magufuli is stating his personal opinions and his moral viewpoints but not scientific facts.

Kama raisi anaweza shauriwa namna sahihi ya kuzuia rate za maambukizi anaweza kukataa lockdown which is fine kwanza watanzania wenyewe walio wengi awaitaki.

Lakini kumnyamazia anapobeza watu kuvaa barakoa kama sehemu za kuchukua tahadhari na kutokana na kauli zake wanaofanya ivyo wanabezwa na viongozi wake au kukataa chanjo ambazo hana scientific information nazo huko ni kinyume cha preventive measures approaches to reduce the risks of spread; inashangaza kuona wataalamu kukaa kimya.

I can understand wale anaowateua kuogopa kwa sababu za kulinda mkate wao; ila kuna watu wamebobea kwenye maswala ya communicable diseases na wameajiriwa kama wataalamu kutokana na elimu yao and want nothing to do with politics kundi ili kukaa kimya ni ishara ya uoga uliopitiliza.
 



☝️Hizo ndio sababu medical professions in US walikuwa na ugomvi na Trump. Kauli zake zilikuwa zinachangia sana hardcore supporters wake kutotaka kufuata ushauri wa kitaalamu.

Huyu wetu anaruhusiwa kusema anavyotaka without rebuke ya wataalamu wapo wanamuangalia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…