Wanajamvi,
Naomba mwenye taarifa hizi kama kweli zilitokea tufahamishane. Eti ni kweli kuwa huyu mwimbaji mzuri wa sura, umbo na kipaji kikubwa aliwahi kuchepuka nje ya ndoa yake?
Nimezisikia hizi taarifa mitaani zimezagaa sana, tena kwa mtu mmoja mmoja, zikidai eti alitoka na kigogo mzito wa serikali ya awamu ya nne na alitangulizwa nje ya nchi na baadae kigogo huyo akafuata na kisha wakawa wamevunja amri ya sita ya Mungu wetu.
Huu ni mwezi wa pili sasa nasikia tetesi hizi zikisemwa chini kwa chini. Kama mjuavyo lisemwalo lipo,na kama halipo basi linakuja,na hakuna siri chini ya jua. Karibuni wadau mchangie tubaini ukweli uhalisi.