Ni mtumishi wa Mungu wa ukweli. Ana mume na watoto 3, wawili wa kike na mmoja wa kiume. Mume wake anafanya TRA na ni mchungaji msaidizi wa kanisa moja la Kilokole. Mume wake ametokea Kigoma. Hivyo yeye ni mama Mchungaji. Inasemekana yeye ni Mnyamwezi wa kuhamia lakini asili yake ni Congo (Ingawa hapa sina uhakika sana)!
Ni mtumishi ambaye ameinuliwa na Mungu mwenyewe! Pia anajua kukaa magotini pa Bwana na ndiyo siri ya kukubalika kwake. Inasemekana yeye kama yeye alianzia chini sana! Alikuwa na duka la nguo, workshop ya kushona nguo & designing Kariakoo ambayo ameifunga mwishoni mwa mwaka jana.
Ni kweli alikuwa anaenda kufunga mzigo Dubai n.k. Kwa sasa sijui kahamishia biashara hiyo wapi! Pamoja na mume wake, wana studio ya kurekodi miziki ya Injili Kigoma. Kwa anayetaka habari zaidi ani PM lakini nadhani zinatosha!