Huyu ni mwadada Mtanzania ambaye anaishi ughaibuni kwa sasa, huyu Dada amejizolea umaarufu mkubwa uliomfanya kua na wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii kutoka na aina ya taarifa zake ambazo huzitoa ama huziandika.
Why Mange Kimambi?
Kutokana na umaarufu wake kwenye mitandao ya kijamii kuandika taarifa zinazohusu mtu yeyote pasipo kujali cheo chake au nafasi yake kwenye jamii,Inaelezwa kua hutumiwa na watu maarufu na viongozi wakubwa kupewa taarifa za siri na kuzivujisha kwenye mitandao ya kijamii! Pia kwa mujibu Mwanamitandao mwingine "lemutuz" ni kwamba huyu dada ni "FUNDI" wa kuzipata taarifa za watu maarufu kupitia marafiki zao ambao yeye hujipenyeza kama rafiki na kuzoa kila aina ya taarifa za siri atakazoona zina umuhimu kwake.Hii ndio sababu ya kufanya aaminiwe kwa taarifa zake ambazo kwa kiasi kikubwa wakati mwingine hata wahusika wakiulizwa hukiri kua ni kweli.
Binafsi nilikua simwamini kabisa Mange Kimambi kwa kujua ni mtu anayejitaftia umaarufu kwenye social media kupitia mapungufu ya maisha ya watu. Lakini baada ya kuwasikia waliokua wakihojiwa kwenye vyombo vya habari baada ya kuandikwa na yeye wakidai kua ni kweli taarifa hizo ni zao, mfano wao ni William Malecela "Lemutuzi" baada ya yeye kuandikwa na huyo kuhusu maisha yake, Mwingine ni Waziri Makamba ambaye naye aliwahi kuandikwa na huyu Dada akihusishwa na kumdanganya mzungungu mmoja kua atasaidi apate tenda kwenye ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, na Makamba alikiri kumfahamu mzungu huyo japo alikana tuhuma dhidi yake.
Kwahiyo mpaka sasa huyu Dada kulingana ukaribu wake na watu mbali mbali maarufu na wengine ni viongozi katika jamii kupitia mitandao ya kijamii,na ujasiri wake wa kuandika chochote anachokisia pasipo kujali athari yake ndiyo sababu ya baadhi ya watu kuanza kutozipuuzia habari zake.