Watanzania watu wabaya sana.
Eti watu wako tayari kusifia malaika wa miaka 20 kuuza bar kisa anaingilia ugomvi wa mtu wanayemuonea wivu.
Jamii forums ni ya great thinkers ila honestly kuna kundi la watu humu wana roho mbaya kama wachawi halafu hadi kuna wazee wenzangu kwenye hilo kundi kudadeki!
Kila anachoffanya Diamond lazima wakikosoe,kila anapopiga hatua lazima wajikusanye humu wamvunje moyo.Kuna kumkosoa mtu ili hili kundi la hawa wanga kazi yao ni moja tu,kuvunja moyo wakidhani wakifanya hivyo hao wanaowavunja moyo kwa kuwaita domo,sijui mama ubaya au sijui mwizi watashuka kuwa level zao.Wenzao ndio kwanza wanazidi kupanda.
Acheni wanga nyie mnajijua na kundi lenu mnatia aibu kila mwenye roho safi anajua nyie kundi lenu ni la watu wenye roho za kwanini.Kwanini Mange awe hivi,kwanini Diamond awe hivi.
Kila siku mpo hapa page kwa page bila aibu kuwavunja wenzenu moyo,yaani kila ukiingia jf hawa viumbe wapo busy hivi mna ajira nyie?Sidhani.
Mnatia huruma sana badala mtumie akili zenu kupanda juu nyie mnazitumia kujaribu kushusha waliopandishwa na Mwenyezi Mungu.
Mtawezea wapi.
Mtapika majungu sana ila hao mnaojaribu kuwashusha hawatashuka hata mfanyaje hadi siku Mungu atakapoamua kuwashusha.