Mwawado!
Ahsante kwa Taarifa Lakini sherehe ni saa 10 jioni Taarifa unatueletea saa 8 Mchana sasa kwa wale wa mbali nafikiri hawatafaidika na taarifa hii.Tafadahali pamoja na kuwaga na kuwahutubia Na nyinyi msisahau kumuuliza maswali na mojawapo naomba liwe hili ,Mheshimiwa Kuna mfununu kwamba CEO wa kampuni ya Richmond ni rafiki yako wa karibu na ndicho kilichopelekea kuishauri serikali kuipatia tender kampuni hiyo ambayo haikuwa hata na ujuzi wa maswala ya umeme, sasa yeye kama balozi wetu wakati huo haoni kwamba alitanguliza ubinafsi kuliko utaifa ktk kutuletea kampuni bomu na kuisababishia Taifa hasara ya mabilioni ya Fedha? Na kama akisema hahusiki je yeye aliishauri ni nini serikali kuhusiana na kampuni hiyo hasa ukizingatia ya kwamba kwa nafasi yake kama balozi alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo kwa masilahi ya TAIFA? Nawatakia sherehe njema!