Who is MIZENGO PINDA? (private & Public)

Kwa hiyo kifupi jamaa anaanza na usanii, bongo kiboko!

Hii ofisi wanaidharaulisha kwa watu wanaowapa.
 
Aiy shoga wee.. mkumbushie mzee basi walau ile nafasi ya Mama Mbathia kwa kuanzia jamani....
......Huyu mama Martha Mlata ni Form IV........naona anafanya kozi fulani fulani ili kujiendeleza...........
 
Kwani kila mtu anayeoa lazima awatangazie Watanzania... mmeambiwa ana mke, hamtaki..
 
Na kwani kuoa au kuolewa ni lazima?
Hivi Condoleeza ameolewa? Au ni lesbian?
 
Yombayomba kwa data ambazo zimeshawekwa ni za kweli kuwa mizengo alioa mke wa kwanza akafa na akamuoa mdogo mtu naye akafa.
Na data za uhakika ni kwamba Tunu ni mke wake wa tatu,Pia tunu anafanya kazi usalama wa taifa ila wanasema hataendelea kwenda kazini kwa sasa kwa vile amekuwa mke wa PM.Hizi ndio data za jikoni na za uhakika.
 

Nahisi tunahama kutoka katika mada halisi, kilichotakiwa hapa ni kumjua Mhe. Pinda kwa undani na sio kudiscuss issue zake personal ili kujudge, kwenye speech yake kuna kitu alikisema ambacho kama sisi kweli ni watu wenye uwezo mzuri wa kuchambua mambo tungekuwa tunaongelea ni jinsi gani tunaweza kuwa msaada kwake yeye kama PM na sio kuwa CRITICS. Nahisi aliongea kitu km hiki "Yeye kama binadamu ana mapungufu na hakuna mtu aliye perfect 100% ivyo basi ni wajibu wa kila mmoja wetu kuweza kumsaidia pale tunapoona kwamba anakosea au mambo hayaendi kama inavyotegemewa kwake"
Sasa basi kama JF ndio inaongoza kwa kuleta unyanyapaa dhidi ya watu wanaowahisi kuwa wana matatizo ya kiafya then naona tunapotea na inafaa tujiangalie vizuri maana hata sisi tunosema haya tunahitajika kuwa na uhakika na afya zetu vilevile!

Wengi wetu tumekuwa persimists sana, tunahitaji kuangalia kwamba je huyu aliyepewa huu uongozi anaweza kuongoza tunavyotegemea?
Kuliko kuanza kuongelea mavazi na vitu vingine ambavyo havina TIJA kwetu... what can clothes do if the mind is corrupt??

Kusema tuseme lakini pia ni bora tutumie uwezo wetu kutafakari kabla ya kusema na hiyo ndio BUSARA.

At JF We dare to talk openly and wisely!
 
Ashakum si matusi. Hii thread ndiyo moja ya sababu wakati mwingine hii forum inakatisha tamaa. Tuko ukurasa wa 15 na bado, tukijadili uvaaji wa PM, mke wa PM na mmoja alitaka kujua kabila la PM! Haya yote yatatusaidia nini katika hiki tunachodai ndiyo kilio chetu? Mimi naamini kuwa hali haiwezi kubadilika bila kuwa na structural changes. PM aliyepita alikuwa na kila haki kisheria kufanya biashara. Naamini kuwa kama hao Richmond wangetekeleza mkataba kama inavyopaswa tusingekuwa tunamzungumzia Pinda sasa hivi. Cha kujiuliza ni kuwa tulifikaje pale tulipofika katika mfumo wa serikali tuliokuwa nao? Itakuwaje watu wachache waweze kudharau taratibu (hata kama kwa nia njema) bila system kuwastukia? Hao wanaoitwa wataalamu na wanataaluma walikuwa wapi? Itakuwaje walikubali kupitisha maamuzi ambayo kitaaluma ni dhahiri wangeona yana matatizo? Mabadiliko gani yafanyike ili wakina Pinda na wenzake wasijikute wameingia katika mitego iliyowanasa waliowatangulia? Muungwana mmoja alianzisha thread inayohusu hili suala (angalia http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=9676 lakini kwa vile haiuhusu masuala ya ugoni wala kumbomoa mtu hakuna anayetaka kuchangia. Wote huku tuko huku tukijaribu kumvua nguo Pinda! Tuna tofauti gani na hayo magazeti ya udaku?
 

Fundi Mchundo (Technician)
Nakupa respect zote mkuu... tulitakiwa hapa tujadili burning issues na siyo kuulizana vitu ambavyo havina faida kwetu.

Udaku kwa folder hili sio safi, mimi naona hii thread tuihamishie kwenye Udaku....
 
Wakubwa naona tunahama mada kabisa.....!! Baadala ya kudiscuss critical issues watu wanaanza kusema mambo ya PM na ngoma? nani aliwambia kama mtu ana ngoma hawezi kuwa kiongozi? Kinacho takiwa nikujua tu kwamba huyu bwana ana mke au hana, ana watoto au hana na wana hali gani kiuchumi? na sio hali gani kiafya?? Tukijua hali zao kiuchumi itatusaidia sana kujadili kama mabadiliko makubwa ya kiuchumi yatatokea hapo baadaye kwenye maisha yao ya kila siku!! Vinginevyo tujadili uwezo wake wa kupambana kwa dhati na ufisadi na rushwa matizo ambayo ni kama kansa kwa TZ hivi sasa, na si kudwell kny petty petty issues!

festog
 

NInavyojua TUNU na Mizengo wanaurafiki wa zaidi ya miaka 7 hivi kwani wakati Mizengo anapewa uminister walikuwa wote ila sijui kama walikuwa wanaishi wote lakini walikuwa wapenzi. Lakini jibu nafikiri limeshapatikana kuwa mke wa PINDA ni TUNU so tukubali na kuheshimu majibu.
 
Naomba kuuliza, nimesikia kuwa jamaa ni "born again". Ningefurahi kupata confirmation toka kwa mtu wa karibu au anayemjua vema huyu mheshimiwa..!!

Plse...!!!
 
Naomba kuuliza, nimesikia kuwa jamaa ni "born again". Ningefurahi kupata confirmation toka kwa mtu wa karibu au anayemjua vema huyu mheshimiwa..!!

Plse...!!!

Kishazi ivi huu udini na ukabila unatusaidia nini sisi watanzania?
Mods can you please move this thread to Nyapesi/Udaku? I feel like it doesnt desrve to be in this folder maana michango mingi imekaa kiudaku udaku!!!
 
Kishazi ivi huu udini na ukabila unatusaidia nini sisi watanzania?
Mods can you please move this thread to Nyapesi/Udaku? I feel like it doesnt desrve to be in this folder maana michango mingi imekaa kiudaku udaku!!!

Inabidi watu wajue kila kitu kuhusu PM wao, heading yenyewe imekwambia private and public sasa unategemea nini?

Hata hayo ya Richmond yalianza kama udaku.It's a thin line between udaku and fact in a country with "information starvation" kama Tanzania.Sasa kama wao wenyewe hawatoi info utalaumu vipi watu ku speculate, speculations ambazo zinaweza kabisa kuwa na ukweli.
 
Naomba kuuliza, nimesikia kuwa jamaa ni "born again". Ningefurahi kupata confirmation toka kwa mtu wa karibu au anayemjua vema huyu mheshimiwa..!!

Plse...!!!

Kishazi,

Hata Chiluba 1991 alikuwa 'born again' ila ndo raisi aliyeifilisi Zambia kwa rushwa!
 

Mkuu Pundit,

kumbe hilo ni tatizo lako wewe, baki nalo kwa sasa. Hebu tuanze kujadili sasa huyu PM focus yake ni nini hasa katika kutekeleza ndoto ya maisha bora kwa kila Mtz? Anaonyesha umakini kiasi gani kwenye maamuzi yake? Je, atatuletea mvua made in Thailand? Atafukuza watendaji kwenye sight visit mbele ya waandishi wa habari?
 
Kambi ya Upinzani Bungeni imemtahadharisha Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda(Baby Face), kuandaa sera ya Taifa ya kulinda, kutunza na kusimamia matumizi ya rasilimali za nchi ili kuzuia uporaji wa maliasili hizo kupitia mikataba mibovu na ufisadi.
 
Kishazi ivi huu udini na ukabila unatusaidia nini sisi watanzania?
Mods can you please move this thread to Nyapesi/Udaku? I feel like it doesnt desrve to be in this folder maana michango mingi imekaa kiudaku udaku!!!

Wacha kukurupuka ndugu Dmussa, swala la kuuliza kama mtu kaokoa au la halihusiani na udini. Angekuwa ni Muslim tungeuliza kwa standards pia za kumuslim. Swala la kujua spiritual status ya mtu, inampa any rational being confirdence juu ya mtu. Nikijua kuwa Kikwete ni Alhaji na Ustadh (tena anayefundisha Madrasat) nitakuwa na comfo juu ya integrity yake. The same applies kwa mtu kama mama Lwakatare, kuwa kwake mtumishi napata imani na integrity yake. Hayo maswala ya Chiluba alikuwa "born again" but akaifilisi nchi, ni maswala ya mtu mwenyewe. Kuokoka au kuwa shekhe versus kuwa mtu wa kidunia ni maamuzi ya mtu, sio lazima, na ndio maana kuna mafuska vile vile, na hata kuna wachungaji wanaamua kumwacha Mungu kwa tamaa zao na kuanza ufisadi kanisani aidha kwa kula sadaka au kula misaada. So, swala la kupotea kwa integrity ya watu wenye maadili ya kimungu, tusili-generalize, wapo ambao wana misimamo yao bado ya kimungu, na wako stable vile vile.

So kama waziri mkuu, ni mtu aliyeokoka tunafurahi as tunaexpect yeye kuwa na hofu ya Mungu. Na kama angekuwa muislamu mwenye maadili tungefurahi vile vile kwa sababu ya the same expectations kuwa, atakuwa na hofu ya Mungu. Kwa hiyo mheshimiwa hilo swala au concept ya udini ing'oe kabisa unless kama wewe una hiyo mentality hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…