Siyo kweli. Statistics zinasema ndege za kawaida zinapata ajali nyingi kuliko hata hizo helcopters.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Jamaa umeongea uongo wa viwango vya juu.
Helicopters zina moving parts nyingi kuliko ndege za kawaida.
Helicopters zinatembea height fupi kutoka kwenye ground hivo muda wa kufanya maamuzi kukitokea tatizo ni mdogo.
Haziko stable, ndege ya kawaida yenye engine mbili ikizima engine moja inaweza tua kwa kutumia ile moja iliyobaki, helicopter haiwezi maana tail rotor ikizima ujue ajari hiyo wakati main rotor ipo. Kama ina blade tatu au nne, moja ikiharibika tatizo kubwa la kuleta ajari.
Ukizima engine zote za ndege inaweza serereka angani kilometa kadhaa maana mabawa yake yanatoa force ya kuiweka angani, helicopter ikizima engine ni chini tu.
Ndege ikipata ajari inaweza dondokea tumbo "belly" helicopter inazunguka angani na lazima ianze kichwa juu miguu chini au idondokee upande.
Helicopter inaruka na kutua mara nyingi katika flight hours zake kuliko ndege. Hizi ndo moments ambazo zinaleta ajari mara nyingi zaidi hivo risk kwa copter ni kubwa.
Fanya ukaguzi, fuata sheria zote lakini rate ya ajari ni kubwa kwa helicopters.