WHO wazitaka nchi za Afrika kufungua shule

Trubarg

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2020
Posts
4,388
Reaction score
7,223
Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (UNICEF) yamezihimiza nchi za Afrika kufungua shule na kuhakikisha watoto wanakuwa salama dhidi ya virusi vya corona.

Mashirika hayo yamesema kuendelea kufunga shule kwa muda mrefu kunahatarisha ustawi wa watoto hao ikiwa ni pamoja na kutopata mlo kamili, mimba za utotoni pamoja na aina mbalimbali za uhalifu.

“Lazima tukahikishe kuwa juhudi za kudhibiti virusi vya corona hazitufanyi tuishie kuwa na kikazi kibovu. Kama mbavyo nchi zinafungua biashara kwa usalama, pia tunaweza kufungua shule,” Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO Afrika.

Nchi sita pekee kati ya nchi 39 za Afrika ndizo zilizofungua shule kwa mujibu wa takwimu za WHO na UNICEF. Baadhi ya nchi hufungua shule kisha kuzifunga baada ya maambukizi ya corona kuanza kuongezeka, huku nyingine zikifungua kwa ajili ya wanafunzi wanaomaliza au wenye mitihani.

Wakati Tanzania ikiwa imefungua shule katika ngazi zote za masomo, Kenya imefuta mwaka wa masomo 2020, na shule zitafunguliwa mwaka 2021.
 
Ajabu sana kama bado kuna watu wanaongozwa na mabeberu

Baadhi ya nchi zimewaruhusu wanafunzi wa mwaka wa mwisho kurudi shule ili wafanye mitihani

Baadhi ya nchi zimewaruhusu wanafunzi wa mwaka wa mwisho kurudi shule ili wafanye mitihaniImage caption: Baadhi ya nchi zimewaruhusu wanafunzi wa mwaka wa mwisho kurudi shule ili wafanye mitihani.

Shirika la afya duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa mataifa la watoto- UNICEF yameyazitaka serikali za Afrika kufungua shule zenye mazingira salama wakati huu wa janga la corona.

Wanasema kufungwa kwa shule kwa muda mrefu kuna madhara kwa wanafunzi na mashirika hayo yanazitaka serikali kuwekeza katika huduma za usafi ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona katika taasisi za masomo.

Mashirika hayo mawili yamesema kuwa wanafunzi wanawekwa katika hatari ya lishe duni, mimba za utotoni na ghasia wakati huu wa kurefushwa kwa muda wa kukaa nyumbani.

Shule katika bara la Afrika ni "mahala salama " kwa watoto, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa WHO Matshidiso Moeti.

"Hatupaswi kusahau juhudi zetu za kudhibiti Covid-19. Wakati nchi zinafungua shughuli za kila siku kwa kuzingatia usalama, tunaweza kufungua tena shule ," alisema katika mkutano wa video Alhamisi.

Kufungwa kwa muda mrefu kwa shule kunaathiri maisha ya baadae ya watoto na jamii, kwa mujibu wa Mkurugenzi mkuu wa Unicef wa kikanda Mohamed Fall. Ni nchi sita tu za Afrika ambazo zimefungua kikamilifu shule, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika nchi 39 na WHO na Unicef.

Baadhi ya nchi zilifunguliwa na baadae kufungwa kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

Nyingine zinafungua shule kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa masomo yao kwa ajili ya kufanya mitihani muhimu.

Nchi kama Kenya zimefuta mwaka wa masomo wa 2020.
 
Taratibu majibu yanaanza kuja,kiukweli tumuombe mungu tu atuokoe na mabaya yoyote yasitupate ktk maisha haya ya kawaida.

Magonjwa kwa kweli ni mitihani tu,tuende nayo na kukabiliana nayo lakini so kujifungia na kufunga nyumba za ibada
 
Hehehe Kenya itafungua shule sasa.. WHO na UNICEF ndo wamesema. Huu ni ushauri wa kisayansi.

CS Magoha ameanza re-opening procedures. Hatusubiri tena 2021.

Wazungu wameshasema tufungue.
 
Naona wanafuata nyayo za Magufuli.

Mkuu usiwe mvivu wa kufikiri,lazima utambue kuwa Corona imeathiri nchi nyingi kwa utofauti,kuna waliopigwa sana na wengine kidogo hivyo masharti ya deal nayo ni tofauti pia. Huwezi kulazimisha nchi zote za afirica zifanye kama Magufuli
 
Hehehe Kenya itafungua shule sasa.. WHO na UNICEF ndo wamesema. Huu ni ushauri wa kisayansi.

CS Magoha ameanza re-opening procedures. Hatusubiri tena 2021.

Wazungu wameshasema tufungue.
Magoha Yuko likizo ya siku 14 nyumbani. Kurudi kazini itategemea Kama Uhuru atamrudisha
 
Mpaka sasa waliokalia kuti kavu ni Magoha na Kagwe, hao hawarudi. Ila ndio hivyo toka jana walianzisha mchakato wa kurudi shuleni. Na kwakuwa WHO na UNICEF wamesema bhas hilo litatekelezwa haraka sana maana hao ndio wataalam na wanasayansi wanaoaminika zaidi hapo kenya.
 
Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (UNICEF) yamezihimiza nchi za Afrika kufungua shule na kuhakikisha watoto wanakuwa salama dhidi ya virusi vya corona.

Mashirika hayo yamesema kuendelea kufunga shule kwa muda mrefu kunahatarisha ustawi wa watoto hao ikiwa ni pamoja na kutopata mlo kamili, mimba za utotoni pamoja na aina mbalimbali za uhalifu.

“Lazima tukahikishe kuwa juhudi za kudhibiti virusi vya corona hazitufanyi tuishie kuwa na kikazi kibovu. Kama mbavyo nchi zinafungua biashara kwa usalama, pia tunaweza kufungua shule,” Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO Afrika.

Nchi sita pekee kati ya nchi 39 za Afrika ndizo zilizofungua shule kwa mujibu wa takwimu za WHO na UNICEF. Baadhi ya nchi hufungua shule kisha kuzifunga baada ya maambukizi ya corona kuanza kuongezeka, huku nyingine zikifungua kwa ajili ya wanafunzi wanaomaliza au wenye mitihani.

Wakati Tanzania ikiwa imefungua shule katika ngazi zote za masomo, Kenya imefuta mwaka wa masomo 2020, na shule zitafunguliwa mwaka 2021.
Uhuru is stupid leader
 
Back
Top Bottom