Whozu afungiwa miezi 6, Mbosso na Billnass wafungiwa miezi 3. Wote wapigwa faini Tsh. Mil. 3. Wimbo wa 'Ameyatimba' umewaponza

Whozu afungiwa miezi 6, Mbosso na Billnass wafungiwa miezi 3. Wote wapigwa faini Tsh. Mil. 3. Wimbo wa 'Ameyatimba' umewaponza

Wamechelewa mno! Wimbo umeshaenea sana na umeshaacha athari kubwa sana katika jamii.

Mimi bado najiuliza kichwani mwa vijana kuna akili gani kwa sasa, mbona maisha yana mengi zaidi ya maudhui ya ngono! Kwa nini hawaoni katika engle iliyo kinyume na ngono? Kuna usalama kwa watoto wetu kesho kweli?
 
Wasanii Mbosso Billnass wametozwa faini ya milioni tatu kila mmoja na kufungiwa kutokujishughulisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia leo November 04, 2023 kutokana na Wasanii hao kushirikishwa kwenye wimbo wa ‘Ameyatimba’ ya Whozu ambao maudhui yake yanatajwa kukiuka kanuni za maadili.

Kwa upande wake Whozu ametakiwa kushusha mara moja video ya wimbo wake wa ‘Ameyatimba’ kwenye digital platform zote, BASATA imemtoza faini ya Tsh. milioni 3 na kumfungia kujishughulisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi 6 kuanzia leo November 04, 2023.

BASATA imesema Whozu alichapisha video ya wimbo huo Nov 02, 2023 akiwashirikisha wasanii wenzake Mbosso na Bill Nass, na kwamba wimbo huo una maudhui yanayokiuka kanuni za maadili kutokana na kuwepo ishara ya vitendo vinavyoashiria matusi kinyume na Kanuni ya 25(6) (j) pamoja na vitendo ya unyanyasaji, ukatili na udhalilisha wa utu wa Mwanamke kinyume na Kanuni ya 25(6)-(f) “Msanii huyu ameshaonywa mara mbili na kutozwa faini mara moja huko nyuma kwa kukiuka taratibu za kuzingatia maadili katika kazi za sanaa lakini bado ameendelea kupuuza”

“Baraza limeshatoa na kuzindua mwongozo wa maadili katika kazi za sanaa ambao unapatikana katika tovuti yetu www.basata.go.tz, hivyo ni jukumu la kila Msanii na mdau wa sanaa kuzingatia maadili katika kazi za sanaa”
 
Utakuta nayeye badala ajutie adhabu anavimba kwamba basata wananijua🤣🤣🤣,
Hivi vitoto sijui tumevitoa wapi,
Nyege hizi nyegezi.
 
Mtoto mdogo anakuwa nchawii.

20231104_232459.jpg
 
View attachment 2804044

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtaka Msanii Whozu kushusha mara moja video ya wimbo wake wa ‘Ameyatimba’ kwenye digital platform zote, pia limemtoza faini ya Tsh. milioni 3 na limemfungia kujishughulisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi 6 kuanzia leo November 04, 2023 kutokana na wimbo huo kuwa na maudhui yanayokiuka kanuni za maadili.

BASATA imesema Whozu alichapisha video ya wimbo huo Nov 02, 2023 akiwashirikisha wasanii wenzake Mbosso na Bill Nass, na kwamba wimbo huo una maudhui yanayokiuka kanuni za maadili kutokana na kuwepo ishara ya vitendo vinavyoashiria matusi kinyume na Kanuni ya 25(6) (j) pamoja na vitendo ya unyanyasaji, ukatili na udhalilisha wa utu wa Mwanamke kinyume na Kanuni ya 25(6)-(f).

“Msanii huyu ameshaonywa mara mbili na kutozwa faini mara moja huko nyuma kwa kukiuka taratibu za kuzingatia maadili katika kazi za sanaa lakini bado ameendelea kupuuza”

“Baraza la Sanaa la Taifa kupitia Sheria Na. 23 ya Mwaka 1984 na Marekebisho yake ya Mwaka 2019 ambayo inatoa Mamlaka kwa Baraza kusimamia Maadili ya msingi kwenye Sekta ya Sanaa kwa Kanuni ya 25(1)-(8) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018.

Pia soma - BASATA angalieni jinsi wasanii wanavyohamasisha ngono chafu
Hii nyimbo nilishaewekea mashaka kwenye aina ya video yake tangu nliposkia audio yake hasa verse ya mboso [emoji23]
 
Tanzania ni nchi yangu. Ila kuna wakati huwa inanivuruga sana akili.

Kila nikiuwazia ule wimbo wa Zuchu wa Honey, na kushushwa vyeo kwa wale walimu wakuu wawili wa shule za msingi! Kisa tu eti wanafunzi walionekana kuuimba na kuucheza!! Ndiyo akili inavurugika kabisa.
 
Back
Top Bottom