Whozu ananunua gari baada ya kulipwa Tigo Fiesta..

Hatuishi kwa kuigana tunaishi kwa kufanya yale tunayoona yanaendana na maisha yetu na mahitaji yetu.
As long as ela kaitolea jasho lake hakuna aliyemchangia ana haki ya kununua chochote na kuifanyia chochote amabacho anaona kinafaa.
Halafu kununua gari ni jambo gumu kuliko kujenga kwakuwa gari mara nyingi inahitajika ulipie cash wakati nyumba unajenga kidogo kidogo japo ni kwa muda mrefu.
So kama aliweka lengo la kununua gari katimiza, basi hata kama ana lengo la kujenga atatimiza Inshallah.
 
Hiyo si asset ni liability asset ni kitu kiwe kinaongezeka samani na kuingizia sasa hapo zinatoka kila siku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo si asset ni liability asset ni kitu kiwe kinaongezeka samani na kuingizia sasa hapo zinatoka kila siku

Sent using Jamii Forums mobile app
Aliyefundisha watanzania maisha ya kuigana sijui ni nani.
Unaweza nunua gari ambalo kila siku linahitaji mafuta lakini ikakuwezesha kufanya michakato yako ambayo inakuingizia ela ya maana ambayo usingeweza kuifanya kwa ufasaha bila gari.
 
Sisi wapangaji tumekukosea nini baba mwenye nyumba[emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania bana, yaani MTU hata usiyemjua kanunua gari unakasirika, unataka ajenge nyumba, alikwambia yeye shida yake yeye ni nyumba..

Hugo dogo kazi zake asilimia kubwa anafanya usiku, akitoka kwenye show anapata shida ya usafiri, yy kaona anunue gari ili arahisishe kazi zake .....hamtaki..
Duh!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Wavumilie tu, wabongo wana hali ngumu. Vichwa vina stress hatari, wanajifanya hawajui kuwa kwa maisha ya dar gari ni hitaji muhimu sio anasa tena.
 
Wewe ni mke wa whozu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ataachaje kununua gari yake ya kwenda mbinguni ilhali aliachwa na basi la kwenda mbinguni kisa nyoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…