La hasha. Huyo mwandishi ndiye hakuchagua maneno yake ipasavyo, angesema wenye degree hawalipwi pesa kulingana na tajriba/elimu yao. Hapo ni sawa kabisa, na sote tunakubali. Lakini kuwaita poor.....hapo kidogo kapitiliza kabisa.
Mtu mwenye kipato kiwangi hicho kwenye nchi zinazoendelea kama Kenya, Tanzania hata kule SA wanaorodheshwa kama "middle- class".
Umaskini wa mtu kama utatokana na anavyotumia hela hizo, hasa kuamua ato kwenda kubughia "ice bucket", maisha kama haya hatayaweza. Itakuwa ni lazma ajipange vyema.