Uchaguzi 2020 Why Bernard Membe is not a presidential material, at all!

Uchaguzi 2020 Why Bernard Membe is not a presidential material, at all!

Bernard Kamilius Membe ni waziri wa Mashauri ya Kigeni nchini Tanzania, ni mwanachama wa chama cha mapinduzi,

Historia ya Membe inaanzia mbali kidogo toka kusini mwa Tanzania katika mikono salama ya upadre, chini ya ukasisi wa Namupa Seminari.

Bernard Kamilius Membe kijana wa kati mwenye uso angavu akiketi dawati la Tatu kutoka kulia, alikuwa mtoto mwenye akili ya kawaida akiwa nyuma ya watoto wenye vipaji shuleni hapo, Kasisi Mariano anamueleza kama Bernard mvivu wakusimamiwa kila jambo,

Hayo ni ya Namupa Seminari na Itaga Seminari katika mapito yake kielimu. Bernard Membe kutoka Darasa la awali hadi High School yani kidato cha sita, hakuna mahali panapotaja uimara wake kiakili darasani wala hakuna tukio lolote la kishujaa la kukumbukwa, iwe katika mitiahani, michezo, uongozi shuleni ama sifa yoyote toka kwa wakufunzi wake.
Kwaujumla alikuwa ni mwanafunzi wa kawaida kabisa ambae hawezi kusonga mbele bila usimamizi wa walimu wake kinyume na wanafunzi wengine,

Mwaka 1978 Membe aliingia kwenye ajira ya serikali akihudumu Ofisi ya Rais Idara ya Usalama wa Taifa kitengo cha uchambuzi wa taarifa za kijasusi, Kazi hiyo amehudumu kwa mwaka mmoja tu akahamishiwa Wizara ya Mashauri ya Kigeni na kwenda Ottawa Canada kuwa mshauri wa Kibalozi kutoka 1992-2000,

Utumishi wake ndani ya Idara ya Usalama haukuwa wa kutukuka na hakuna kumbukumbu lake na la mfano ndani ya idara kwa ujumla zaidi ya kuwa mmoja ya majasusi wa Tanzania waliopata mafunzo ya mda kuke Scotland Uk, Hakuna mission yoyote aliyowahi kupewa na akaifanya kwa ufanisi wenye kukubalika ndani ya Idara, anamshinda hata Eliamkim Maswi yule wa Escrow ambae yeye alipewa mission ya kuiua NCCR ya Mrema na akafanikiwa kwakujipenyeza mpaka kuwa mbeba mikoba wa Mrema enzi zile na kuizika NCCR MAGEUZI kabisa,

Mwaka 2000 aliingia kwenye siasa akawa Mbunge wa Jimbo la Mtama, nakisha kuwa naibu waziri wa Mashauri ya Ndani, baadae naibu Waziri wa Nishati na Madini, na kisha naibu waziri wa Mambo ya Kigeni na sasa ni Waziri kamili wa Mashauri ya Kigeni,

Kulegalega kwa Diplomasia ya Tanzania kunatokana na udhaifu wa Bernard Membe katika wizara hii ya mashaiuri ya Kigeni, Diplomasia ya nchi imeshuka na sasa sio Tanzania ile yenye sauti ya UTU.

Katika kipiti cha utmishi wa Bernard Membe ndani ya Wizara taifa limeshuhudia migogoro mikubwa ya Kidiplomasia na mataifa ya kigeni, ambayo kimsingi ni ufinyu wa maarifa wa Bernard Membe katika kukabiliana nayo,

Mathalani Mgogoro na Malawi wa Ziwa Nyasa, Mgogoro na Rwanda, Mgogoro na Kenya, Mgorogoro na Uingeraza, Mgogoro na ummoja wa nchi wa Hisani wa Maendeleo za Ulaya,

Haya yote yametukia katika uongozi wa Bernard Membe katika wizara inayohusika na mashauri ya Kigeni, lakini hili linatokana na historia ya mtumishi huyu ambaye hajawahi kuwa kiongozi wala hajawahi kujiongoza yeye mwenyewe,

Je dhamana kubwa kabisa ya Urais wa Jamhuri anaweza ikiwa Wizara tu imemshinda?

Zingatia, Bernard Membe hajawahi kuwa kiongozi wa umma tangu AZALIWE 1953 mpaka 2000 alipoingia kwenye siasa, hivyo uongozi sio kipaji chake!

Basi kama Membe aliwahi kutumwa kuua demokrasia na hakufanya kama Maswi basi anafaa sana kwa ustawi wa Tanzania. Kama Membe hana akili na kwa shule za seminari ambako hakuna kujuana wala nini alifikaje form six? Kama Membe hajawahi kufanikisha mission ya kijasusi ambazo tunajua wakati wa chama kimoja ilkuwa ni ukandamizaji basi Membe ni mwema kwa wananchi waliokuwa huru kuongea.

Kwa kifupi, huwezi kutegemea treni yaani kichwa na mabahewa yake iende vizuri kama kichwa ni horrible!!! Halafu inaonekana kama hujafurahishwa na maamuzi ya Membe hapo wizarani na kukunyima maslahi fulani ukiwa kama mtumishi wa wizara hiyo!!!
 
Msichafue watu, ni vema ukaacha watanzania wakaamua wenyewe kuliko kuanza kupigia debe hao waliokutuma.
 
Humjui Membe ww peleka hizi njaa zako Monduli ukale buku 7
 
Msichafue watu, ni vema ukaacha watanzania wakaamua wenyewe kuliko kuanza kupigia debe hao waliokutuma.
Yericko ye ni Mkenya??!!ndo ameamua hivyo,labda useme kwa nini maamuzi yake kayaanika,hata hivo katiba imemruhusu
 
Yes hana uwezo na dhamira kama walivyo CCM wote,sasa isionekane bwana ako kapata uchochoro.hatujaja kumtawaza Lowasa hapa

Mkuu we waache hawa vijana waneng'eneke, hapa tutawapia wote kwakuwa huko ccm hata angejitokeza Mtume au Yesu basi hafai kuwa rais wa Tanzania, kuichagua ccm ni laana
 
Basi kama Membe aliwahi kutumwa kuua demokrasia na hakufanya kama Maswi basi anafaa sana kwa ustawi wa Tanzania. Kama Membe hana akili na kwa shule za seminari ambako hakuna kujuana wala nini alifikaje form six? Kama Membe hajawahi kufanikisha mission ya kijasusi ambazo tunajua wakati wa chama kimoja ilkuwa ni ukandamizaji basi Membe ni mwema kwa wananchi waliokuwa huru kuongea.

Kwa kifupi, huwezi kutegemea treni yaani kichwa na mabahewa yake iende vizuri kama kichwa ni horrible!!! Halafu inaonekana kama hujafurahishwa na maamuzi ya Membe hapo wizarani na kukunyima maslahi fulani ukiwa kama mtumishi wa wizara hiyo!!!

Mimi ni mkulima wa bamia tu huku Mbutu Kigamboni sio mfanyakazi wa wizara ya membe
 
Jitambue!!
 

Attachments

  • 1423045307616.jpg
    1423045307616.jpg
    9 KB · Views: 193
Kwa kwa kuwa umetumia kigezo cha uwezo wake wa darasani na kwa kuwa kigezo hicho kinahusiana na alivyopata elimu yake.

Basi, ni vyema na haki utupe wasifu wake wa kielimu pia, alipita wapi na alikwama wapi kwenye elimu yake.

Ni kawaida sana kwa miaka ya zamani watu kufeli na kurudia, vip Membe kuna historia hiyo?ukipeleka kwa milengo ya aina hiyo ndipo utakapokuwa na haki kusema hakuwa na uwezo darasani au vipi.

Kuna shule zingine, kama Ilboru na Mzumbe za zamani, ilikuwa ngumu sana kuwika kwemye darasa lako, lakini ata mtu asiye 20 bora huko akienda shule nyingine angeweza kuwa kichwa chao, hivyo sio haki kumpima kwa kuangalia tu darasani kwake kama alikuwa kipanga miongoni kwa wenzake lakin kupitia kigezo cha jumla, pote alipopita kuna matokeo ya jumla.

Kuhusu kutowahi kuwa kiongozi kabla hiyo sio kigezo cha udhaifu wake, kuna suala la malengo na mipango, kwamba kwa wakati fulani unataka ujikite zaidi kwenye jambo fulani hivyo jambo lingime unaliachia lipite kwanza.

Kuna watu wengi waliokuwa wanamichezo wazuri lakin hawakuwa wanashiriki umishumta wala umiseta maana ni distraction kwa walichokuwa busy nacho shule.La pili ni debatable pia je uongozi mtu anazaliwa nao au anajifunza?na wataalamu wengi wanakubali kuwa uongozi kama nyanja zingine zozote unafunzwa.

Lakii kingine Plato Myunani wa kale anayeheshimika sana alipata kusema "Wanafalsafa ndio wanaofaa kutawala maana wanasifa kuu mbili muhimu, kwanza wanaweza kutawala lakin pili hawapendi kutawala" akaendelea kusema ni "wapo tofauti na wanasiasa wa kawaida ambao wanapenda kutawala wakati hawawezi kutawala"akasema Jamii Iwatambue watu hao ni iwafor e wachukue uongozi.Hivyo kigezo cha kuwa kiongozu kila ulipopita jambo ni ishara kuwa unapenda uongozi lakini sio ishara kuwa unaweza uongozi au unafaa kuwa kiongozi, maana wanasiasa wa kaqaisa hutaka tu uongozi japo hawana uwezo wa kuongoza.
 
Hapana pingamizi Bernard Membe ni mfitinishi pengine mwenye wivu na hulka ya fitina chinichini hata anaweza kusababisha maafa.

Mwulizeni kwa nini hayuko karibu na viongozi wa Kanisa Katoliki wakati alikuwa mseminari akisomea upadre Kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne seminari ya Namupa na kisha "A" level huko Itaga, Tabora, hadi kuvaa Kanzu Seminari Kuu ya Peramiho, Songea? Kuna nini nyuma ya pazia?

Kifo cha kutatanisha cha Padre Serapius Komba kwa kuugua ugonjwa wa kufa ubongo polepole kilihuzunisha na hakitasahaulika na wengi, hayati Padre Serapius Komba ambaye alikuwa Gombera wa Seminari Kuu Peramiho, mandishi mahiri na aliyejaliwa akili nzuri na mwenendo mwema wakati huo washiriki wa Bernard Membe akina hayati Padre Sebastina Napachihi waliotaka kushika nafasi ya ugombera hadi kuwa maaskofu walichokifanya kwa Serapius Komba anakijua na pengine kuwa mshauri na mbinu hatimaye mfanikishaji wa tukio.

Akiwa ameshavua kanzu na kufanya kazi Ikulu usalama wa taifa kitengo hicho cha ujasusi hayo yakitokea Seminari Kuu Peramiho Bernard Membe alikovaa kanzu ya useminari na kusomea masomo ya awali ya filosofia yanayotangulia teolojia alivua kanzu na kwenda huko kufanya kazi Ikulu na kisha kutokea hayo pale seminari kuu Peramiho. Hayuko karibu kabisa na kanisa lililomsomesha na kumlea hadi awe alivyo na pengine kuna kinachomsumbua alicholifanyia kanisa na kuambua kukaa mbali kabisa.

Kwa macho yangu nikiwa mdogo nasoma shule tukienda kuangalia mpira nilimshuhudia akiwa na Kanzu seminari Kuu Peramiho alikuwa na mazoea kusafiri na timu ya mpira wa miguu ya waseminari akiwa shabiki wa timu hiyo. Alionekana mtulivu sana kama ilivyo kawaida ya waseminari wengine ila hakuonyesha upekee. Kwa waliokuwa karibu naye huko alikosomea Peramiho alionekana kuwa karibu katika kila tukio na kujua kila kinachojilia seminarini, pengine alishakuwa na kazi maalum pale seminarini bila wakubwa wake kujua hadi walipomshtukia baadaye sana.
 
Mwalimu alisema ukila nyama ya binadamu huwezi kuacha labda ndio sababu kaslimu....naskia cardinal pengo alishamfukuza membe ofsni kwake alipoenda kumuomba kanisa liruhusu Tanzania kujiunga IOC
 
Very petty! acha umbeya
Unauliza and I quote, 'Je dhamana kubwa kabisa ya Urais wa Jamhuri anaweza ikiwa Wizara tu imemshinda?'
Jibu: Kama mtawala na mwanasiasa ANAWEZA
 
Back
Top Bottom