Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425

Bernard Kamilius Membe ni waziri wa Mashauri ya Kigeni nchini Tanzania, ni mwanachama wa chama cha mapinduzi,
Historia ya Membe inaanzia mbali kidogo toka kusini mwa Tanzania katika mikono salama ya upadre, chini ya ukasisi wa Namupa Seminari.
Bernard Kamilius Membe kijana wa kati mwenye uso angavu akiketi dawati la Tatu kutoka kulia, alikuwa mtoto mwenye akili ya kawaida akiwa nyuma ya watoto wenye vipaji shuleni hapo, Kasisi Mariano anamueleza kama Bernard mvivu wakusimamiwa kila jambo,
Hayo ni ya Namupa Seminari na Itaga Seminari katika mapito yake kielimu. Bernard Membe kutoka Darasa la awali hadi High School yani kidato cha sita, hakuna mahali panapotaja uimara wake kiakili darasani wala hakuna tukio lolote la kishujaa la kukumbukwa, iwe katika mitiahani, michezo, uongozi shuleni ama sifa yoyote toka kwa wakufunzi wake.
Kwaujumla alikuwa ni mwanafunzi wa kawaida kabisa ambae hawezi kusonga mbele bila usimamizi wa walimu wake kinyume na wanafunzi wengine,
Mwaka 1978 Membe aliingia kwenye ajira ya serikali akihudumu Ofisi ya Rais Idara ya Usalama wa Taifa kitengo cha uchambuzi wa taarifa za kijasusi, Kazi hiyo amehudumu kwa mika kumi na mbili tu akahamishiwa Wizara ya Mashauri ya Kigeni na kwenda Ottawa Canada kuwa mshauri wa Kibalozi kutoka 1992-2000,
Utumishi wake ndani ya Idara ya Usalama haukuwa wa kutukuka na hakuna kumbukumbu lake na la mfano ndani ya idara kwa ujumla zaidi ya kuwa mmoja ya majasusi wa Tanzania waliopata mafunzo ya mda kuke Scotland Uk, Hakuna mission yoyote aliyowahi kupewa na akaifanya kwa ufanisi wenye kukubalika ndani ya Idara, anamshinda hata Eliamkim Maswi yule wa Escrow ambae yeye alipewa mission ya kuiua NCCR ya Mrema na akafanikiwa kwakujipenyeza mpaka kuwa mbeba mikoba wa Mrema enzi zile na kuizika NCCR MAGEUZI kabisa,
Mwaka 2000 aliingia kwenye siasa akawa Mbunge wa Jimbo la Mtama, nakisha tarehe 17/10/2006 hadi 1/11/2007 aliteuliwa kuwa naibu Waziri wa Nishati na Madini, na kisha 1/12/2007 mpaka sasa ni Waziri kamili wa Mashauri ya Kigeni,
Kulegalega kwa Diplomasia ya Tanzania kunatokana na udhaifu wa Bernard Membe katika wizara hii ya mashaiuri ya Kigeni, Diplomasia ya nchi imeshuka na sasa sio Tanzania ile yenye sauti ya UTU.
Katika kipiti cha utmishi wa Bernard Membe ndani ya Wizara taifa limeshuhudia migogoro mikubwa ya Kidiplomasia na mataifa ya kigeni, ambayo kimsingi ni ufinyu wa maarifa wa Bernard Membe katika kukabiliana nayo,
Mathalani Mgogoro na Malawi wa Ziwa Nyasa, Mgogoro na Rwanda, Mgogoro na Kenya, Mgorogoro na Uingeraza, Mgogoro na ummoja wa nchi wa Hisani wa Maendeleo za Ulaya,
Haya yote yametukia katika uongozi wa Bernard Membe katika wizara inayohusika na mashauri ya Kigeni, lakini hili linatokana na historia ya mtumishi huyu ambaye hajawahi kuwa kiongozi wala hajawahi kujiongoza yeye mwenyewe,
Je dhamana kubwa kabisa ya Urais wa Jamhuri anaweza ikiwa Wizara tu imemshinda?
Zingatia, Bernard Membe hajawahi kuwa kiongozi wa umma tangu AZALIWE 1953 mpaka 2000 alipoingia kwenye siasa, hivyo uongozi sio kipaji chake!