jebs2002
JF-Expert Member
- Sep 3, 2008
- 9,604
- 8,812
Ebu twambie wewe unadhan nani anafaa?
The truth, I don't know mate, issue ni ni nyie kwa kura zenu kuamua...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ebu twambie wewe unadhan nani anafaa?
Yeriko Nyerere nani anayekutuma kuandika hayo?
Mkuu, unaweza kunieleza ni kwa namna gani Membe alimfitini Mudhihiri? Ninachojua ni kwamba Mudhihiri alishindwa kwenye siasa za ushindani na kijana Mtanda akatwaa jimbo na Mchinga
Ebu twambie wewe unadhan nani anafaa?
we umetumwa na nani kuuliza
Yeriko Nyerere nani anayekutuma kuandika hayo?
Matusi ya nini mkuu, jenga hoja ama jibu hoja kwakutuliza moyo na akili
Mgojwa wao hata kushika karatasi hawezi,report ya kamati anakaimisha,mama dk zaidi ya 30 kusimama hawezi
The truth, I don't know mate, issue ni ni nyie kwa kura zenu kuamua...
Unawaona ndio hawa....wanachukulia kutafuta Rais wa nchi kama mchezo wa kuigiza..Tulia wewe mama Lowasa level nyngne kazi za kuhangaika na.makaratas ni za kna membe na kna January ....lowasa asubiri kuapishwa kua rais 2015 tutampa urais ata kuptia tketi ya familia yake ata ccm itafia mbali ismpomptsha......our president is lowasa. .porojo za afya hzo ni propaganda za team mdmu a.k.a waftn au waweza kuwaita wazee wa wama
Athari kubwa ya majasusi kujiingiza kwenye nafasi za uongozi ni pamoja na kuendelea kulindana na viongozi wote walopita na serikali yote ambayo siku zote inaeekezwa tuhuma za UFISADI.
Ili kuelewa zaidi juu ya hali hii inabidi uangalie historia ya majasusi wote wale maarufu kama Mabere Marandu, Bernard Membe, Eliakim Maswi, Augustine Mrema ambae baadhi ya majasusi waliwahi kuwa wanafunzi wake alipokuwa mwalimu na hata Masumbuko Lamwai ambao walipewa kazi ya kumdhibiti Mrema, alipotaka uraisi mwaka 1995.
Ni kazi ngumu sana kwa Membe kama atajaribu kutaka kuwania uraisi lakini jaribu kuangalia historia ya raisi Putin wa Russia tangu awe jasusi na baadae mkuu wa KGB, waziri mkuu na sasa raisi wa nchi hiyo kubwa huko Urassia lakini ni mtu hatari sana.
Mambo aloyafanya mpaka sasa ni mazito sana kuanzia kunyang'anya baadhi ya watu mali zao, kugawa mali za nchi kwa marafiki zake na genge lote la ilokuwa KGB ya zamani (maana hawa ndio wanaomlinda), kuwafukuza wale wote ambao wamejaribu kupinga yale anayoyafanya ) mfano Litvinenko alieuawa nchini Uingereza na majasusi wenzie) na mambo mengine mengi tu ya ajabu.
View attachment 224363
Bernard Kamilius Membe ni waziri wa Mashauri ya Kigeni nchini Tanzania, ni mwanachama wa chama cha mapinduzi,
Historia ya Membe inaanzia mbali kidogo toka kusini mwa Tanzania katika mikono salama ya upadre, chini ya ukasisi wa Namupa Seminari.
Bernard Kamilius Membe kijana wa kati mwenye uso angavu akiketi dawati la Tatu kutoka kulia, alikuwa mtoto mwenye akili ya kawaida akiwa nyuma ya watoto wenye vipaji shuleni hapo, Kasisi Mariano anamueleza kama Bernard mvivu wakusimamiwa kila jambo,
Hayo ni ya Namupa Seminari na Itaga Seminari katika mapito yake kielimu. Bernard Membe kutoka Darasa la awali hadi High School yani kidato cha sita, hakuna mahali panapotaja uimara wake kiakili darasani wala hakuna tukio lolote la kishujaa la kukumbukwa, iwe katika mitiahani, michezo, uongozi shuleni ama sifa yoyote toka kwa wakufunzi wake.
Kwaujumla alikuwa ni mwanafunzi wa kawaida kabisa ambae hawezi kusonga mbele bila usimamizi wa walimu wake kinyume na wanafunzi wengine,
Mwaka 1978 Membe aliingia kwenye ajira ya serikali akihudumu Ofisi ya Rais Idara ya Usalama wa Taifa kitengo cha uchambuzi wa taarifa za kijasusi, Kazi hiyo amehudumu kwa mika kumi na mbili tu (KISHA AKAFUKUZWA) akahamishiwa Wizara ya Mashauri ya Kigeni na kwenda Ottawa Canada kuwa mshauri wa Kibalozi kutoka 1992-2000,
Utumishi wake ndani ya Idara ya Usalama haukuwa wa kutukuka na hakuna kumbukumbu lake na la mfano ndani ya idara kwa ujumla zaidi ya kuwa mmoja ya majasusi wa Tanzania waliopata mafunzo ya mda kuke Scotland Uk, Hakuna mission yoyote aliyowahi kupewa na akaifanya kwa ufanisi wenye kukubalika ndani ya Idara, anamshinda hata Eliamkim Maswi yule wa Escrow ambae yeye alipewa mission ya kuiua NCCR ya Mrema na akafanikiwa kwakujipenyeza mpaka kuwa mbeba mikoba wa Mrema enzi zile na kuizika NCCR MAGEUZI kabisa,
Mwaka 2000 aliingia kwenye siasa akawa Mbunge wa Jimbo la Mtama, nakisha tarehe 17/10/2006 hadi 1/11/2007 aliteuliwa kuwa naibu Waziri wa Nishati na Madini, na kisha 1/12/2007 mpaka sasa ni Waziri kamili wa Mashauri ya Kigeni,
Kulegalega kwa Diplomasia ya Tanzania kunatokana na udhaifu wa Bernard Membe katika wizara hii ya mashaiuri ya Kigeni, Diplomasia ya nchi imeshuka na sasa sio Tanzania ile yenye sauti ya UTU.
Katika kipiti cha utmishi wa Bernard Membe ndani ya Wizara taifa limeshuhudia migogoro mikubwa ya Kidiplomasia na mataifa ya kigeni, ambayo kimsingi ni ufinyu wa maarifa wa Bernard Membe katika kukabiliana nayo,
Mathalani Mgogoro na Malawi wa Ziwa Nyasa, Mgogoro na Rwanda, Mgogoro na Kenya, Mgorogoro na Uingeraza, Mgogoro na ummoja wa nchi wa Hisani wa Maendeleo za Ulaya,
Haya yote yametukia katika uongozi wa Bernard Membe katika wizara inayohusika na mashauri ya Kigeni, lakini hili linatokana na historia ya mtumishi huyu ambaye hajawahi kuwa kiongozi wala hajawahi kujiongoza yeye mwenyewe,
Je dhamana kubwa kabisa ya Urais wa Jamhuri anaweza ikiwa Wizara tu imemshinda?
Zingatia, Bernard Membe hajawahi kuwa kiongozi wa umma tangu AZALIWE 1953 mpaka 2000 alipoingia kwenye siasa, hivyo uongozi sio kipaji chake!
Mini natoka jimbo la Mchinga, jimbo ambalo Mudhihir alikuwa anahudumu! Ni kichekesho mtu kusema kwamba eti Membe alim-fitini Mudhihiri! Anyway, sehemu ninayotoka wanamuheshimu sana Membe... usiniulize kwanini! Nina uhakika kwa 100% kwamba sehemu ninayotoka walikuwa wanampigia kura Mudhihiri kwa sababu ya Membe tu, nothing else... Mudhihiri kama Mudhihir alikuwa hapendwi kabisa! Mtu kama Marehemu Mama wa Tondowa alikuwa anapendwa kuliko Mudhiri lakini nadhani CCM wilaya ama mkoa walikuwa wanambeba tu Mudhihir kuwakilisha chama hadi pale ilipoonekana habebeki tena!Mkuu, unaweza kunieleza ni kwa namna gani Membe alimfitini Mudhihiri? Ninachojua ni kwamba Mudhihiri alishindwa kwenye siasa za ushindani na kijana Mtanda akatwaa jimbo na Mchinga
Yericko Nyerere nisaidie haya machache ili nifahamu kinyume na vile ninavyofahamu!Kulegalega kwa Diplomasia ya Tanzania kunatokana na udhaifu wa Bernard Membe katika wizara hii ya mashaiuri ya Kigeni, Diplomasia ya nchi imeshuka na sasa sio Tanzania ile yenye sauti ya UTU.
Katika kipiti cha utumishi wa Bernard Membe ndani ya Wizara taifa limeshuhudia migogoro mikubwa ya Kidiplomasia na mataifa ya kigeni, ambayo kimsingi ni ufinyu wa maarifa wa Bernard Membe katika kukabiliana nayo,
Mathalani Mgogoro na Malawi wa Ziwa Nyasa, Mgogoro na Rwanda, Mgogoro na Kenya, Mgorogoro na Uingeraza, Mgogoro na ummoja wa nchi wa Hisani wa Maendeleo za Ulaya,
Yericko Nyerere nisaidie haya machache ili nifahamu kinyume na vile ninavyofahamu!
Mosi, Kumbukumbu zangu kuhusu mgogoro wa Ziwa Nyasa, mgogoro ulianza pale ex-Malawian President, Joyce Banda, au mtu kutoka serikali yake aliposema kwamba Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kwa 100%! Membe akasimama kidete na kusema hakuna kitu kama hicho na akatamka hadharani kwamba mpaka wa Ziwa Nyasa ni kati kati ya ziwa hilo! Kwa kutumia diplomasia, shauri hilo limo mikononi mwa Rais Mstaafu wa Msumbiji! Swali: Unadhani Membe alikuwa na control ya nini Rais au mtu kutoka serikali ya Malawi angeweza kusema kuhusu ziwa Nyasa? Rais Joyce Banda hakuwa wa kwanza kutoka Malawi ku-claim kwamba Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kwa 100%! Rais Kamuzu Banda hadi anatoka madarakani hii ilikuwa ni hoja yake... tena aliisema wazi wazi wakati wa utawala wa Hayati Mwalimu Nyerere! Unataka kusema kwamba hata enzi za Mwalimu hakukuwa na diplomasia iliyokamaa hadi vichaa kama akina Kamuzu Banda kufikia ku-claim kwamba Ziwa Nyasa ni lao kwa 100%? Hivi si ndo hao hao ambao waliwahi ku-claim kwamba hata sehemu y Mkoa wa Mbeya ni yao? Unataka kusema kwamba enzi hizo nazo utawala wa Mwalimu ulikuwa na diplomasia dhaifu!
Pili, tuje hili la Kagame! Kila mwenye akili yake anafahamu kwamba mgogoro wetu na Kagame ulianza pale JK alipotoa ushauri wa serikali ya Rwanda kukaa meza moja na FDLR! Kagame akaja juu na kuanza kashifa dhidi ya JK! Wale wanaopenda kutetea ujinga wakadai eti JK angetoa ushauri huo kwa siri!!! Niambie ewe mwana-diplomasia ulietukuka! Hivi ushauri ule wa JK iliosababisha mtafuruku wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Tanzania na wewe kutaka kumbebesha mzigo huo Membe; ulikuwa na kitu gani very special hadi ushauri ule uonekane haukutolewa hadharani? Tangu lini mambo ya kusaka amani kwa mazungumzo yakawa siri? Membe anahusikaje katika hili? Au ulitaka amuunge Mkono Mbunge wa CHADEMA ambae bila aibu wala haya alisimama bungeni kuwatetea M23 wakati kila mwenye akili yake anafahamu kwamba M23 walikuwa ni tatizo? Wale wanaopenda kutetea upuuzi wanafikia kusema kwamba eti dharau za Kagame kwa Tanzania zinatokana na udhaifu wa JK! Watu hawa, na kama nawe Yericko ni mmoja wao niwajuze tu kwamba mtu kama Kagame hawezi kusubiria kiongozi awe dhaifu ili aweze kumkashifu provided unaingilia maslahi yake! Kwa wenye akili zao wanafahamu wazi kwamba, Mwalimu Nyerere pamoja na heshima kubwa ambayo alikuwa nayo Afrika na duniani kwa ujumla lakini hakuepeka kashifa za hadharani kutoka kwa Idd Amin! Hivi kuna kashfa kama kiongozi wa nchi moja anapomuambia kiongozi wa nchi nyingine kama kweli yeye ni mwanaume basi wakutane kwenye ulingo wa masumbwi? Ina maana wakati Idd Amin anatamka haya diplomasia kwenye utawala wa Nyerere ilikua dhaifu au kiongozi mwendawazimu anachohitaji ni kuingiliwa tu maslahi yake ili nae aanze kumwa kashfa hadharani bila kujali hadhi ya yule anayekashifiwa?
Tatu, tuje suala la Mgogoro na Kenya! Unazungumzia mgogoro upi? Ninachokumbuka mimi "mgogoro" wetu na Kenya ulianzia pale JK alipotamka hadharani kwamba kufanyika kwa vikao CoW bila kutoa taarifa kwa other member states isn't right na iwe iwavyo, kama lengo ni kui-frustrate Tanzania, basi Tanzania haiwezi kujitoa EAC! Kutokana na kauli ya JK ambayo hakukupesa macho wala kuuma meno, siku chache baadae, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya akaja Tanzania na katika hali isiyotarajiwa akatamka hadharani tena bila aibu kwamba Kenya haikufahamu kwamba inachofanya hakikuwa sawa... as if hawakusoma muongozo wa EAC! Ni mgogoro huu unaosema unathibitisha udhaifu wa Membe au kuna mgogoro mwingine? Assume wewe ndie Waziri wa Mashauri ya Nje wa Tanzania... nipe outiline ya namna gani ungeweza kutatua mgogoro huu; sio mbaya unipe outiline ya namna gani ungeweza ku-handle issue ya Ziwa Nyasa! Sina shaka kabisa, moja ya solution zako ingekuwa ni Tanzania kuridhia kila kitu kinachotakiwa na EAC Member states bila kujali kwamba kina maslahi kwa Tanzania au hapana! Sina shaka vile vile kwamba, kwa issue ya Ziwa Nyasa solution yako wala isingekuwa tukubali yaishe, tuwaachie Malawi ziwa lao!
Mimi kama ningepewa nafasi ya kumhoji mheshimiwa Membe ningemuuliza masuali mawili tu.
Kwanza, kwanini kwa niaba ya serikali ya Tanzania alikataa pesa ilokuwa inarudishwa na BAE systems paundi milioni 29.5 ya Uingereza isipitie kwenye mashirika ya kujitolea maana ingesaidia hata kununua madawati mashuleni.
BAE Systems walisema kwa kuwa kuna kila dalili ya rushwa kutendwa katika manunuzi ya mtambo wa kuongozea ndege wao hawakutaka kuona pesa hiyohiyo inarudi katika mikono ya serikali.Je yeye kwa mawazo yake aliona ni sawa pesa ile irudi serikalini na mpaka sasa pesa ile imefanya kazi gani?
Suali la pili, ni kwamba je yeye mheshimiwa Membe akiwa ofisa katika idara ya usalama mwaka 1977 alifahamu kuwepo kazi na kikosi kazi kwa ajili ya kuiondoa serikali ya Shelisheli ya raisi Mancham ili kummweka France Albert Rene ambae alikuwa mjamaa?
Je kama alifahamu kuwepo kwa kazi hiyo je leo hii anafikiria vipi uhusiano wa nchi moja na ingine kama Tanzania na Marekani au Ghana.
Nauliza hivyo kwasababu mapema mwaka huu kulikuwa na jaribio la kuipindua serikali ya Gambia lililofanzwa na baadhi ya raia wa nchi hiyo waishio nchini Marekani na serikali ya Marekani ikawakamata wote na kuwafungulia mashtaka kwa kutaka kuipindua serikali halali ya nchi rafiki.
Membe hovyo kabisa! anachokiweza ni kuwafitinisha wenzake tu! alianza kuwafitinisha akina Mudhihir na jamaa zake wote wa kusini waliokuwepo kwenye system! kwa kushirikiana na Sitta wameweza kupenyeza fitna ya kumchafua Lowassa ile mbaya! ilifikia mahla wakamwambia JK eti atatawala kwa kipindi kimoja tu kwani Edo amejiandaa kumvua madaraka 2010 kwa sababu za kiafya! Sendeka aliingizwa mkenge na sasa amekuwa mbogo ile mbaya! Membe amekuwa akiwashauri CCM mikakati ya kuidhoofisha UKAWA! Operesheni za kijinga za kukamata na kutesa wananchi ameziasisi yeye , wassira na Pinda! Jitihada za kuboresha Daftari la Wapiga kura siku zote zimekuwa zikififishwa na mikakati yake ya kijinga ... Membe si Mwanadplomasia mzuri kwani wataalam wanaweza kumsoma paji lake la uso kirahisi sana! No wonder sasa hivi tunapigwa bit kila upande ... Membe hafai kuwa kiongozi zaidi ya kusaidia kugawa Juice ....