Uchaguzi 2020 Why Bernard Membe is not a presidential material, at all!

Uchaguzi 2020 Why Bernard Membe is not a presidential material, at all!

Mkuu, unaweza kunieleza ni kwa namna gani Membe alimfitini Mudhihiri? Ninachojua ni kwamba Mudhihiri alishindwa kwenye siasa za ushindani na kijana Mtanda akatwaa jimbo na Mchinga

Mimi nipo Kinyope, walipishana kwa ujenzi wa kiwanda cha cementi, Mudhihiri alitaka ijengwe kwenye jimbo lake Hon Membe hataki, ..etc
 
Yeriko Nyerere nani anayekutuma kuandika hayo?

Bio data za Namupa unazo ndugu Y Nyerere? Kwa hili sijajua kama Y N alisoma nae au vipi.

Pili kinadharia kusini na kanda ya ziwa wapi na wapi?
 
Matusi ya nini mkuu, jenga hoja ama jibu hoja kwakutuliza moyo na akili

Umetusaidia kutuonyesha kwamba licha ya kukatishwa tamaa na siasa zetu za hovyo lakini nchi yetu bado tunao Watanzania wasafi na wenye heshima kama Balozi Mahiga. Ni jukumu la wazalendo wote tuanzishe movement bila kujali vyama,itikadi,dini na ukanda tuwashawishi watu wa aina wajitokeze na kugombea uongozi wa nchi yetu.

Wana UKAWA wakati ndio huu. Wanaccm asili akina mzee Warioba,Salim,Butiku,nk mtasaidia Tanzania kwa kuwaunga mkono watu aina ya Mahiga hata kama hawatasimama kwa ticket ya CCM. Mtalitendea haki taifa letu na mtakumbukwa kwa vizazi vingi vijavyo.
 
Mgojwa wao hata kushika karatasi hawezi,report ya kamati anakaimisha,mama dk zaidi ya 30 kusimama hawezi

Tulia wewe mama Lowasa level nyngne kazi za kuhangaika na.makaratas ni za kna membe na kna January ....lowasa asubiri kuapishwa kua rais 2015 tutampa urais ata kuptia tketi ya familia yake ata ccm itafia mbali ismpomptsha......our president is lowasa. .porojo za afya hzo ni propaganda za team mdmu a.k.a waftn au waweza kuwaita wazee wa wama
 
The truth, I don't know mate, issue ni ni nyie kwa kura zenu kuamua...

Pamoja sana mkuu.

Lakini hii ni nchi yetu sote, na tukikosea tunaliwa pamoja.

Bahati mbaya sana siasa yetu imekuwa kama mchezo wa kuigiza tu, watu wanatumika tu bila na matokeo yake tunachagua viongozi based on vitu vidogovidogo sana visivyo na mashiko.

Wagombea badala ya kuangalia kupanga nin watafanya kwa nchi, wanawekeza kwenye kununua watu na kununua waandishi na vyombo vya habari, nampongeza Makamba na Kigwagwala vyovyote utakavyowatafsiri lakin wamejitokeza kwa hoja, hii ndio namna ya kuanza safari ya ikulu, wengine wanaanza kuhonga na kuahidi kulipa fadhira kwa watu, ole kwa nchi yetu.

Mwaka 2015, vyombo vya habari vyote vilikuwa na muelekeo mmoja tu Kikwete Ndiye Chaguo la Mungu...Mgombea Asiye na Kasoro...Anayekuja Kuwakomboa Watanzania.

Wagombea wengine wote, ukisoma byombo vya habari ilijaa tu mabaya yao ata yasiyokuwepo yaliungwaungwa ata kwa kamba ya katani.Baada ya uchaguzi tukajagundua tukiwa tumechelewa kuwa kumbe tulikuwa tunachezewa comedy tu.

Nakumbuka Sumaye alienda kuchukua fomu, na kwa jinsi alivyochafuliwa, siku ile ya kuchukua fomu badala ya kueleza sera ilibidi hotuba yake nzima ijae kujibu kashfa 11 zilizoelekezwa kwake, tuliamimishwa hakuna fisadi kama Sumaye, baada ya uchaguzi hatumuoni kwemye ufisadi tulioambiwa.

Tuliambiwa Salim Ahmed Salim ni sio Mtanzania, kaja kufuata urais tu, tukimpa tutakuwa tumempa mgeni, tukaambiwa SalimAhmed Salim hafai kwa lolote, ni Mhizbu wa kutupwa, baada ya uchaguzi kama kawaida kashfa zote zikafa, Salim akachaguliwa tena kuingia kamati kuu ya chama ambacho eti hakipendi maana ni Hizbu.

Na sasa vyombo karibu vyote vya habari na waandishi wameshikwa na Lowassa, mabaya yake hayasikiki tena bali wapinzani wake kama akina Membe huyasikii mazuri yao kwenye vyombo vya habari, ni mabaya tu, ata wakitoa speech au taarifa namna inavyoandikwa ni kwa namna ya kuonyesha waliongea ni kitu cha kijinga kisicho na mantiki.Lakin Lowassa ata akiongea kitu kidogo tu, kitakavyopambwa utaona kwenye huyu ndiye haswa, hofu yangu hatujajifunza kwa yaliyotokea 2015.

Ndio maana namsifu Membe kwamba kwa nafasi yake, kwa connections zake, angeweza kabisa nae kupata wafadhiri wa kimnunulia waandishi na vyombo vya habari vikawa vinamuuza na kuimba sifa zake, ila sijaona chombo chochote cha habari ambacho kinamuuza.Kwa hili namsifu na inanipa imani ya kuona yawezekana ni mtu safi.
 
Tulia wewe mama Lowasa level nyngne kazi za kuhangaika na.makaratas ni za kna membe na kna January ....lowasa asubiri kuapishwa kua rais 2015 tutampa urais ata kuptia tketi ya familia yake ata ccm itafia mbali ismpomptsha......our president is lowasa. .porojo za afya hzo ni propaganda za team mdmu a.k.a waftn au waweza kuwaita wazee wa wama
Unawaona ndio hawa....wanachukulia kutafuta Rais wa nchi kama mchezo wa kuigiza..
 
Athari kubwa ya majasusi kujiingiza kwenye nafasi za uongozi ni pamoja na kuendelea kulindana na viongozi wote walopita na serikali yote ambayo siku zote inaeekezwa tuhuma za UFISADI.

Ili kuelewa zaidi juu ya hali hii inabidi uangalie historia ya majasusi wote wale maarufu kama Mabere Marandu, Bernard Membe, Eliakim Maswi, Augustine Mrema ambae baadhi ya majasusi waliwahi kuwa wanafunzi wake alipokuwa mwalimu na hata Masumbuko Lamwai ambao walipewa kazi ya kumdhibiti Mrema, alipotaka uraisi mwaka 1995.

Ni kazi ngumu sana kwa Membe kama atajaribu kutaka kuwania uraisi lakini jaribu kuangalia historia ya raisi Putin wa Russia tangu awe jasusi na baadae mkuu wa KGB, waziri mkuu na sasa raisi wa nchi hiyo kubwa huko Urassia lakini ni mtu hatari sana.

Mambo aloyafanya mpaka sasa ni mazito sana kuanzia kunyang'anya baadhi ya watu mali zao, kugawa mali za nchi kwa marafiki zake na genge lote la ilokuwa KGB ya zamani (maana hawa ndio wanaomlinda), kuwafukuza wale wote ambao wamejaribu kupinga yale anayoyafanya ) mfano Litvinenko alieuawa nchini Uingereza na majasusi wenzie) na mambo mengine mengi tu ya ajabu.
 
Labda hufahamu kuwa ni Jasusi Membe ndiye aliyepeleka hoja Bungeni ya kumtoa Jasusi mwenzake Hans Kitine kwenye uwaziri.Hivyo hoja yako hiyo haina nguvu kwa mfano wa Membe mwenyewe ata kabla hatujatafuta mifano ya wengine.

Wakati huo Membe akiwa Mbunge wa kawaida namkumbuka kama miongoni mwa Wabunge makini waliokuwepo, alikuwa akikomaa na mawaziri kama tunavyowaona leo akina Kangi Lugola, na nadhani ni Uwaziri ndio unamzuia kuwa vile alivyokuwa.

Raia Mwema - Mafanikio na utata wa Membe kidiplomasia
.................................................................................................................................................................
Taswira ya Membe katika uadilifu

Bernard Membe ni kati ya viongozi wachache katika serikali ya CCM wanaojitutumua kwamba ni waadilifu.

Msingi wa uadifu wa Membe unajengwa katika maeneo mawili makubwa. Eneo la kwanza ni kazi aliyoifanya kuokoa fedha za umma kwa kutumia nafasi aliyoishika katika ubalozi wa Canada.

Mapema katika Bunge la mwaka 2001/2002, paliibuka kashfa kubwa ikimhusisha aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Dk. Hans Kitine. Katika kashfa hiyo ilidaiwa kwamba Dk. Kitine alikuwa ametumia fedha za serikali kwa kumtibu mke wake, Saada Mkwawa Kitine, nje ya nchi kwa kiwango cha dola za kimarekani 63,000.

Hata hivyo, uchunguzi wa Serikali haukuonyesha ushahidi wowote kwamba mke wa Dk. Kitine alitibiwa nje ya nchi wala kuumwa. Kashfa hii ikasababisha Dk. Kitine kujiuzulu nafasi yake na mke wake kuamriwa kulipa fedha zote alizokuwa amechukua kwa matibabu hewa.

Hata hivyo, mwezi Julai 2002, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), chini ya Mbunge Richard Ndasa aliyekuwa anakaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, iliandika barua Wizara ya Afya ikiiagiza wizara hiyo kumrudishia mke wa Kitine pesa ambazo alikuwa ameshalipa kiasi cha dola 15,000. Kamati hiyo ilidai kugundua kwamba Mama Kitine alikuwa kweli anaumwa na alitibiwa nje ya nchi kwa kufuata utaratibu.

Haraka haraka Dk. Kitine akaitisha mkutano na waandishi wa habari na kujigamba kwamba yeye ni mwadilifu na kilichotokea ilikuwa ni majungu tu na hivyo Bunge limemsafisha.

Ni katika hatua hii ambapo Bernard Membe alisimama Bungeni kueleza kwamba alikuwa na ushahidi bayana kuhusu ufisadi uliofanywa na Dk. Kitine kwa jina la matibabu ya mke wake.

Alipopewa nafasi, Membe akamwaga nyaraka muhimu zilikuwa zinaonyesha jinsi fedha zilivyotumwa kwenye akaunti binafsi ya mama Kitine badala ya kutumwa katika akaunti ya ubalozi. Membe akiwa ubalozini Canada ndiye aliyepewa jukumu la kuchunguza uhalali wa matibu na malipo kwa ajili ya mama Kitine.

Katika hospitali zote zilizodaiwa kumtibu mama Kitine hawakupata ushahidi wowote kwamba aliwahi hata kufika huko, achilia mbali kutibiwa.

Kufuatia kuthibitika kwa kashfa ya Dk. Kitine, ilionekana wazi kwamba Kamati ya Bunge ilikuwa imetumika kujaribu kumsafisha Dk. Kitine na familia yake kwa njia za giza. Kwa sababu hii wajumbe watatu wa Kamati hii walifungiwa miezi miwili kihudhuria vikao vya Bunge. Wajumbe hawa walikuwa ni Richard Ndasa, Dk. Amani Kaborou na Dk. Hans Kitine mwenyewe.

...................................
........................................................................................................................
 
Mimi kama ningepewa nafasi ya kumhoji mheshimiwa Membe ningemuuliza masuali mawili tu.

Kwanza, kwanini kwa niaba ya serikali ya Tanzania alikataa pesa ilokuwa inarudishwa na BAE systems paundi milioni 29.5 ya Uingereza isipitie kwenye mashirika ya kujitolea maana ingesaidia hata kununua madawati mashuleni.

BAE Systems walisema kwa kuwa kuna kila dalili ya rushwa kutendwa katika manunuzi ya mtambo wa kuongozea ndege wao hawakutaka kuona pesa hiyohiyo inarudi katika mikono ya serikali.Je yeye kwa mawazo yake aliona ni sawa pesa ile irudi serikalini na mpaka sasa pesa ile imefanya kazi gani?

Suali la pili, ni kwamba je yeye mheshimiwa Membe akiwa ofisa katika idara ya usalama mwaka 1977 alifahamu kuwepo kazi na kikosi kazi kwa ajili ya kuiondoa serikali ya Shelisheli ya raisi Mancham ili kummweka France Albert Rene ambae alikuwa mjamaa?

Je kama alifahamu kuwepo kwa kazi hiyo je leo hii anafikiria vipi uhusiano wa nchi moja na ingine kama Tanzania na Marekani au Ghana.

Nauliza hivyo kwasababu mapema mwaka huu kulikuwa na jaribio la kuipindua serikali ya Gambia lililofanzwa na baadhi ya raia wa nchi hiyo waishio nchini Marekani na serikali ya Marekani ikawakamata wote na kuwafungulia mashtaka kwa kutaka kuipindua serikali halali ya nchi rafiki.
 
View attachment 224363

Bernard Kamilius Membe ni waziri wa Mashauri ya Kigeni nchini Tanzania, ni mwanachama wa chama cha mapinduzi,

Historia ya Membe inaanzia mbali kidogo toka kusini mwa Tanzania katika mikono salama ya upadre, chini ya ukasisi wa Namupa Seminari.

Bernard Kamilius Membe kijana wa kati mwenye uso angavu akiketi dawati la Tatu kutoka kulia, alikuwa mtoto mwenye akili ya kawaida akiwa nyuma ya watoto wenye vipaji shuleni hapo, Kasisi Mariano anamueleza kama Bernard mvivu wakusimamiwa kila jambo,

Hayo ni ya Namupa Seminari na Itaga Seminari katika mapito yake kielimu. Bernard Membe kutoka Darasa la awali hadi High School yani kidato cha sita, hakuna mahali panapotaja uimara wake kiakili darasani wala hakuna tukio lolote la kishujaa la kukumbukwa, iwe katika mitiahani, michezo, uongozi shuleni ama sifa yoyote toka kwa wakufunzi wake.
Kwaujumla alikuwa ni mwanafunzi wa kawaida kabisa ambae hawezi kusonga mbele bila usimamizi wa walimu wake kinyume na wanafunzi wengine,

Mwaka 1978 Membe aliingia kwenye ajira ya serikali akihudumu Ofisi ya Rais Idara ya Usalama wa Taifa kitengo cha uchambuzi wa taarifa za kijasusi, Kazi hiyo amehudumu kwa mika kumi na mbili tu (KISHA AKAFUKUZWA) akahamishiwa Wizara ya Mashauri ya Kigeni na kwenda Ottawa Canada kuwa mshauri wa Kibalozi kutoka 1992-2000,

Utumishi wake ndani ya Idara ya Usalama haukuwa wa kutukuka na hakuna kumbukumbu lake na la mfano ndani ya idara kwa ujumla zaidi ya kuwa mmoja ya majasusi wa Tanzania waliopata mafunzo ya mda kuke Scotland Uk, Hakuna mission yoyote aliyowahi kupewa na akaifanya kwa ufanisi wenye kukubalika ndani ya Idara, anamshinda hata Eliamkim Maswi yule wa Escrow ambae yeye alipewa mission ya kuiua NCCR ya Mrema na akafanikiwa kwakujipenyeza mpaka kuwa mbeba mikoba wa Mrema enzi zile na kuizika NCCR MAGEUZI kabisa,

Mwaka 2000 aliingia kwenye siasa akawa Mbunge wa Jimbo la Mtama, nakisha tarehe 17/10/2006 hadi 1/11/2007 aliteuliwa kuwa naibu Waziri wa Nishati na Madini, na kisha 1/12/2007 mpaka sasa ni Waziri kamili wa Mashauri ya Kigeni,

Kulegalega kwa Diplomasia ya Tanzania kunatokana na udhaifu wa Bernard Membe katika wizara hii ya mashaiuri ya Kigeni, Diplomasia ya nchi imeshuka na sasa sio Tanzania ile yenye sauti ya UTU.

Katika kipiti cha utmishi wa Bernard Membe ndani ya Wizara taifa limeshuhudia migogoro mikubwa ya Kidiplomasia na mataifa ya kigeni, ambayo kimsingi ni ufinyu wa maarifa wa Bernard Membe katika kukabiliana nayo,

Mathalani Mgogoro na Malawi wa Ziwa Nyasa, Mgogoro na Rwanda, Mgogoro na Kenya, Mgorogoro na Uingeraza, Mgogoro na ummoja wa nchi wa Hisani wa Maendeleo za Ulaya,

Haya yote yametukia katika uongozi wa Bernard Membe katika wizara inayohusika na mashauri ya Kigeni, lakini hili linatokana na historia ya mtumishi huyu ambaye hajawahi kuwa kiongozi wala hajawahi kujiongoza yeye mwenyewe,

Je dhamana kubwa kabisa ya Urais wa Jamhuri anaweza ikiwa Wizara tu imemshinda?

Zingatia, Bernard Membe hajawahi kuwa kiongozi wa umma tangu AZALIWE 1953 mpaka 2000 alipoingia kwenye siasa, hivyo uongozi sio kipaji chake!

Edited....
 
Mkuu, unaweza kunieleza ni kwa namna gani Membe alimfitini Mudhihiri? Ninachojua ni kwamba Mudhihiri alishindwa kwenye siasa za ushindani na kijana Mtanda akatwaa jimbo na Mchinga
Mini natoka jimbo la Mchinga, jimbo ambalo Mudhihir alikuwa anahudumu! Ni kichekesho mtu kusema kwamba eti Membe alim-fitini Mudhihiri! Anyway, sehemu ninayotoka wanamuheshimu sana Membe... usiniulize kwanini! Nina uhakika kwa 100% kwamba sehemu ninayotoka walikuwa wanampigia kura Mudhihiri kwa sababu ya Membe tu, nothing else... Mudhihiri kama Mudhihir alikuwa hapendwi kabisa! Mtu kama Marehemu Mama wa Tondowa alikuwa anapendwa kuliko Mudhiri lakini nadhani CCM wilaya ama mkoa walikuwa wanambeba tu Mudhihir kuwakilisha chama hadi pale ilipoonekana habebeki tena!

Uhasama wa Mudhiri na Membe, ambao RockSpider anataka kuaminisha watu ulitokana na fitina za Membe ulisbabishwa na ujenzi wa kiwanda cha saruji! Kutokana na ubinafsi, Mudhiri alitaka kiwanda kijengwe Mchinga... kijiji anachotoka Mudhihir! Membe hakukubaliana na jambo hili badala yake akataka kijengwe Lindi! Anayeufahamu Mkoa wa Lindi, kijiji cha Mchinga kimekaa kushoto sana! Membe kwa kuona kwamba Mkoa wa Lindi hakuna kiwanda chochote, akaona busara kiwanda hicho kijengwe Lindi ambayo ni rahisi kufikika kutoka kila sehemu ya mkoa tofauti na Mchinga! Hata busara ya kawaida inashawishi best location ingekuwa Lindi na sio Mchinga! Tusisahau... watu wengi huwa hawapendi kufanya kazi mikoa ya kusini... sasa ikiwa watu wanaenda kwa shingo upande au kukataa kwenda mahali kama Lindi Mjini au Mtwara, sijui huko Mchinga ingekuwaje... Mchinga ni kijiji... narudia, ni kijiji! Idadi ya wakazi wake haifikii hata ile ya wakazi wa kijiji chetu.. lakini Mudhihir akataka kiwanda kiwe huko kwa sababu tu ni kijijini kwao!

Kutokana na hilo, ndipo Mudhihiri akaibuka bungeni na msamiati wa Joka La Mdimu... kwa maana kwamba, Membe kutoka jimbo la Mtama yanamuhusu vipi mambo ya Jimbo la Mchinga huku akisahau kwamba Mtama na Mchinga ni mkoa mmoja na ni wilaya moja! Wakati Lindi inafikika kirahisi kutoka Mtama na Mchinga, Mchinga inafikika kirahisi kutoka Kilwa kuliko kutoka sehemu zingine za wilaya ya Lindi! Wapenda kurukia mada, wakachukua nahau za kichuki za Mudhihir bila kufahamu chanzo cha mzozo ni ubinafsi wa Mudhiri... wa kutaka kiwanda kikajengwe kijijini kwao!
 
Last edited by a moderator:
Kulegalega kwa Diplomasia ya Tanzania kunatokana na udhaifu wa Bernard Membe katika wizara hii ya mashaiuri ya Kigeni, Diplomasia ya nchi imeshuka na sasa sio Tanzania ile yenye sauti ya UTU.

Katika kipiti cha utumishi wa Bernard Membe ndani ya Wizara taifa limeshuhudia migogoro mikubwa ya Kidiplomasia na mataifa ya kigeni, ambayo kimsingi ni ufinyu wa maarifa wa Bernard Membe katika kukabiliana nayo,

Mathalani Mgogoro na Malawi wa Ziwa Nyasa, Mgogoro na Rwanda, Mgogoro na Kenya, Mgorogoro na Uingeraza, Mgogoro na ummoja wa nchi wa Hisani wa Maendeleo za Ulaya,
Yericko Nyerere nisaidie haya machache ili nifahamu kinyume na vile ninavyofahamu!

Mosi, Kumbukumbu zangu kuhusu mgogoro wa Ziwa Nyasa, mgogoro ulianza pale ex-Malawian President, Joyce Banda, au mtu kutoka serikali yake aliposema kwamba Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kwa 100%! Membe akasimama kidete na kusema hakuna kitu kama hicho na akatamka hadharani kwamba mpaka wa Ziwa Nyasa ni kati kati ya ziwa hilo! Kwa kutumia diplomasia, shauri hilo limo mikononi mwa Rais Mstaafu wa Msumbiji! Swali: Unadhani Membe alikuwa na control ya nini Rais au mtu kutoka serikali ya Malawi angeweza kusema kuhusu ziwa Nyasa? Rais Joyce Banda hakuwa wa kwanza kutoka Malawi ku-claim kwamba Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kwa 100%! Rais Kamuzu Banda hadi anatoka madarakani hii ilikuwa ni hoja yake... tena aliisema wazi wazi wakati wa utawala wa Hayati Mwalimu Nyerere! Unataka kusema kwamba hata enzi za Mwalimu hakukuwa na diplomasia iliyokamaa hadi vichaa kama akina Kamuzu Banda kufikia ku-claim kwamba Ziwa Nyasa ni lao kwa 100%? Hivi si ndo hao hao ambao waliwahi ku-claim kwamba hata sehemu y Mkoa wa Mbeya ni yao? Unataka kusema kwamba enzi hizo nazo utawala wa Mwalimu ulikuwa na diplomasia dhaifu!

Pili, tuje hili la Kagame! Kila mwenye akili yake anafahamu kwamba mgogoro wetu na Kagame ulianza pale JK alipotoa ushauri wa serikali ya Rwanda kukaa meza moja na FDLR! Kagame akaja juu na kuanza kashifa dhidi ya JK! Wale wanaopenda kutetea ujinga wakadai eti JK angetoa ushauri huo kwa siri!!! Niambie ewe mwana-diplomasia ulietukuka! Hivi ushauri ule wa JK iliosababisha mtafuruku wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Tanzania na wewe kutaka kumbebesha mzigo huo Membe; ulikuwa na kitu gani very special hadi ushauri ule uonekane haukutolewa hadharani? Tangu lini mambo ya kusaka amani kwa mazungumzo yakawa siri? Membe anahusikaje katika hili? Au ulitaka amuunge Mkono Mbunge wa CHADEMA ambae bila aibu wala haya alisimama bungeni kuwatetea M23 wakati kila mwenye akili yake anafahamu kwamba M23 walikuwa ni tatizo? Wale wanaopenda kutetea upuuzi wanafikia kusema kwamba eti dharau za Kagame kwa Tanzania zinatokana na udhaifu wa JK! Watu hawa, na kama nawe Yericko ni mmoja wao niwajuze tu kwamba mtu kama Kagame hawezi kusubiria kiongozi awe dhaifu ili aweze kumkashifu provided unaingilia maslahi yake! Kwa wenye akili zao wanafahamu wazi kwamba, Mwalimu Nyerere pamoja na heshima kubwa ambayo alikuwa nayo Afrika na duniani kwa ujumla lakini hakuepeka kashifa za hadharani kutoka kwa Idd Amin! Hivi kuna kashfa kama kiongozi wa nchi moja anapomuambia kiongozi wa nchi nyingine kama kweli yeye ni mwanaume basi wakutane kwenye ulingo wa masumbwi? Ina maana wakati Idd Amin anatamka haya diplomasia kwenye utawala wa Nyerere ilikua dhaifu au kiongozi mwendawazimu anachohitaji ni kuingiliwa tu maslahi yake ili nae aanze kumwa kashfa hadharani bila kujali hadhi ya yule anayekashifiwa?

Tatu, tuje suala la Mgogoro na Kenya! Unazungumzia mgogoro upi? Ninachokumbuka mimi "mgogoro" wetu na Kenya ulianzia pale JK alipotamka hadharani kwamba kufanyika kwa vikao CoW bila kutoa taarifa kwa other member states isn't right na iwe iwavyo, kama lengo ni kui-frustrate Tanzania, basi Tanzania haiwezi kujitoa EAC! Kutokana na kauli ya JK ambayo hakukupesa macho wala kuuma meno, siku chache baadae, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya akaja Tanzania na katika hali isiyotarajiwa akatamka hadharani tena bila aibu kwamba Kenya haikufahamu kwamba inachofanya hakikuwa sawa... as if hawakusoma muongozo wa EAC! Ni mgogoro huu unaosema unathibitisha udhaifu wa Membe au kuna mgogoro mwingine? Assume wewe ndie Waziri wa Mashauri ya Nje wa Tanzania... nipe outiline ya namna gani ungeweza kutatua mgogoro huu; sio mbaya unipe outiline ya namna gani ungeweza ku-handle issue ya Ziwa Nyasa! Sina shaka kabisa, moja ya solution zako ingekuwa ni Tanzania kuridhia kila kitu kinachotakiwa na EAC Member states bila kujali kwamba kina maslahi kwa Tanzania au hapana! Sina shaka vile vile kwamba, kwa issue ya Ziwa Nyasa solution yako wala isingekuwa tukubali yaishe, tuwaachie Malawi ziwa lao!
 
1. Mgogoro wa Ziwa Nyasa ni wa Tangu kabla ya Uhuru,

Serikali zilizopita zilitumia kwa kiwango kikubwa diplomasia tuli kuutatua ndiomaana hatukuona sauti za juu za utatuzi wake zaidi lile shambulizi la kijeshi la Julius Nyerere dhidi ya boti za kijeshi za Kamuzu Banda 1970+.

Mwenendo wa diplomasia TULI ulikuwa ni mjarabu zaidi kuli hizi diplomasia kichaa za Bernard Membe (Radical Diplomatic)

2.Suala la Rwanda kimsingi kama ni ushauri ulitakiwa utoleww kuwakufuata utaratibu wa kidiplomasia na sio kuutolea popote tu na na mkuu wa nchi, Membe alitakiwa kuufikisha kwa waziri mwenzie wa Mashauri ya Kigeni wa Rwanda na sio Jk kukurupuka na kusema hadharani tu,hiyo sio diplomasia bali ni uchochezi.

3. Suala la Kenya kwakiasi kikubwa mgogoro wetu unatokana na chembe za mgogoro na Rwanda, Wenzetu Wanyarwanda wameweza kuubadili mgogoro huu kuwa wa Afrika Mashariki badala ya Tz na Rw, ijapokuwa kiini halisi cha mgogoro wa Tanzania na Rwanda au Jk na PK ni mkataba wa Lemera wa kuimega na kuiuza Kongo nakuunda taifa imara la Watusi uliosainiwa kati ya Laurant, Yower Mseven na Paul Kagame.
 
Last edited by a moderator:
Mimi kama ningepewa nafasi ya kumhoji mheshimiwa Membe ningemuuliza masuali mawili tu.

Kwanza, kwanini kwa niaba ya serikali ya Tanzania alikataa pesa ilokuwa inarudishwa na BAE systems paundi milioni 29.5 ya Uingereza isipitie kwenye mashirika ya kujitolea maana ingesaidia hata kununua madawati mashuleni.

BAE Systems walisema kwa kuwa kuna kila dalili ya rushwa kutendwa katika manunuzi ya mtambo wa kuongozea ndege wao hawakutaka kuona pesa hiyohiyo inarudi katika mikono ya serikali.Je yeye kwa mawazo yake aliona ni sawa pesa ile irudi serikalini na mpaka sasa pesa ile imefanya kazi gani?

Suali la pili, ni kwamba je yeye mheshimiwa Membe akiwa ofisa katika idara ya usalama mwaka 1977 alifahamu kuwepo kazi na kikosi kazi kwa ajili ya kuiondoa serikali ya Shelisheli ya raisi Mancham ili kummweka France Albert Rene ambae alikuwa mjamaa?

Je kama alifahamu kuwepo kwa kazi hiyo je leo hii anafikiria vipi uhusiano wa nchi moja na ingine kama Tanzania na Marekani au Ghana.

Nauliza hivyo kwasababu mapema mwaka huu kulikuwa na jaribio la kuipindua serikali ya Gambia lililofanzwa na baadhi ya raia wa nchi hiyo waishio nchini Marekani na serikali ya Marekani ikawakamata wote na kuwafungulia mashtaka kwa kutaka kuipindua serikali halali ya nchi rafiki.

Umejenga hoja mhimu sana na nzito, sidhani wapambe wake wataweza kujibu
 
Cheo anacho ringia Yericko
Groupie:The term originates from the female attaching herself to a band. A groupie is considered more intense about her adored celebrities than a fan and tends to follow them from place to place. A groupie will attempt to have a connection with the band and may seek sexual or intimate contact. Obsessive groupies will almost certainly involve themselves sexually with any members of the band
 
Membe hovyo kabisa! anachokiweza ni kuwafitinisha wenzake tu! alianza kuwafitinisha akina Mudhihir na jamaa zake wote wa kusini waliokuwepo kwenye system! kwa kushirikiana na Sitta wameweza kupenyeza fitna ya kumchafua Lowassa ile mbaya! ilifikia mahla wakamwambia JK eti atatawala kwa kipindi kimoja tu kwani Edo amejiandaa kumvua madaraka 2010 kwa sababu za kiafya! Sendeka aliingizwa mkenge na sasa amekuwa mbogo ile mbaya! Membe amekuwa akiwashauri CCM mikakati ya kuidhoofisha UKAWA! Operesheni za kijinga za kukamata na kutesa wananchi ameziasisi yeye , wassira na Pinda! Jitihada za kuboresha Daftari la Wapiga kura siku zote zimekuwa zikififishwa na mikakati yake ya kijinga ... Membe si Mwanadplomasia mzuri kwani wataalam wanaweza kumsoma paji lake la uso kirahisi sana! No wonder sasa hivi tunapigwa bit kila upande ... Membe hafai kuwa kiongozi zaidi ya kusaidia kugawa Juice ....

Membe ni mtu Hatari sana alikula njama na Balozi wa Libya wakapora Mapesa ya Gadafi akaenda kuyafucha kwenye Handaki nyumbani kwake kisha akala njama Balozi wa Libya akauawa na kushikishwa Bunduki mkononi kuzuga kama amejiua mwenyewe, huu Unyama aliutenda ili kuficha Ushahidi juu ya hizo fedha za Marehemu Gadafi, membe kapiga Ufisadi mkubwa kwenye Ununuzi wa nyumba za Ubalozi huko ulaya kila nyumba iliyonunuliwa kuna percent zake, Membe kaweka mtu wake pale Ubalozi wa Uingereza ( UK) ambaye anawalipisha watu wengi Ada za viza na pesa wanagawana hivyo watu kukosa viza kwa visingizio vya kijinga jinga huku pesa zao zikiliwa na Membe na watu wake, Membe ni Mwizi anapenyeza wizi wake hadi kwenye balozi za nje hafai hata kuwa Mwenyekiti wa kijiji.
 
Back
Top Bottom