MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Mzee huwa unajichanganya sana, Mbona umesema Al shabaab hawana Ugomvi na Tanzania, mnatukingia Kifua dhidi ya Nani?
Mashababi hawana ugomvi na nyie maana hamjahusika kwenye kuwazuia kutanua, hampo kwenye kundi linalowanyima usingizi, lakini ikitokea tuwaache wafanye yao na kuanza kutanua, utawaskia hadi Kigoma. Wao wako kama ISIS, yaani wakipata fursa ya kutoka, hutoka na kuzagaa kote.
Hapa tu hamjahusika na ugomvi wao lakini vijana wenu wanakuja kujilipua Kenya na kwenda kufanya ugaidi Msumbiji, inaonyesha hapo kwenu jinsi vijana wanatamani sana kinuke, siku mtie guu wapate sababu. Acheni kukejeli juhudi zetu za kudhibiti haya mazombi maana siku tukishindwa na kuachia, mtatamani dunia ipasuke.
Ukipata fursa kaitazame hii movie