Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #32,961
Rafiki yangu,
Tufunge mwana 2020 na kufungua na kuishi katika mwaka 2021 tukitafakari maneno ya Kristo kupitia Nabii na Mfalme Solomoni (Suleimani):
Katika Mithali 6 anasema:
1. “‘Ewe mvivu, mwendee chungu (au sisimizi) zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana kiongozi, wala msimamizi, wala mkuu, lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua;
Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hadi lini?
Utaondoka lini katika usingizi wako? Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,
Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silah” (Mithali 6:6-11)
2. “Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA;
Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake:?
i) Macho ya kiburi,
ii) Ulimi wa uongo,
iii) Mikono imwagayo damu isiyo na hatia,
iv) Moyo uwazao mawazo mabaya,
v) Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu,
vi) Shahidi wa uongo asemaye uongo;
vii) Apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu” (Mithali 6:16-19)
3. “Mwanangu, shika maagizo ya baba yako,
Wala usiiache sheria ya mama yako. Yafunge hayo katika moyo wako daima;
Jivike hayo shingoni mwako.
Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda, Na uamkapo yatazungumza nawe. Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru,
Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima” (Mithali 6:20-23).
Tunda la Roho: Upendo, Amani, Hekima, Uvumilivu, Maarifa, Uelewa, Uaminifu, Kuwa na Kiasi, nk liwe nawe katika mwaka 2021 na kwenda mbele.
Wasalaam
Charles Ndyetabula
31 Disemba 2020