Why should I confess?

Why should I confess?

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Utadangishwa na usipokuwa makini wanakugeuza punda, sasa hivi director anatembelea gari ya million 600 sio mchezo, na ilo jina la director alipewaga kwa sababu hiyo. Kamdangisha sana wema ๐Ÿ˜‚
Ila director yule mama namuinulia mikono juu๐Ÿ™Œ ana pesa nyingi kuliko anazozionyesha watoto wake wanaspend kama watoto wa Bakhresa๐Ÿฅน
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Utadangishwa na usipokuwa makini wanakugeuza punda, sasa hivi director anatembelea gari ya million 600 sio mchezo, na ilo jina la director alipewaga kwa sababu hiyo. Kamdangisha sana wema ๐Ÿ˜‚
Hatari Sana, nawa onaga vibinti vya chuo. Vina hangaika kwenye ma status.

Kuna saloon ya kike karibu na home, basi kutwa Wana shinda humo.
wame wekewa mpaka masofa ๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ
 
Nashindwa kufunguka kila kitu,.
Anyways... hata mimi sielewei ni nini kimeniconfuse๐Ÿ˜‘
Funguka bhana ndio utapata ufumbuzi, mbona Mimi kuna siku nilifunguka jambo humu na nikapata na ufumbuzi japo watesi wangu ni watu wenye mamlaka lakini kwa sababu nilishapata ufumbuzi napambana hivyo hivyo kwa msaada wa Mungu na watu wema wenye kunitakia mema.
 
We Umesha sema wapaka bleach, Wana tattoo, vipindi.

Mara vipato vyao na biashara havi endani, hao ni street retailers ๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ
YEah ni kweli,. Sema ni watu ambao wanajuana na watu wengi na wako very supportive kwenye chochote nitakachotaka kufanya wananisapoti kwa asilimia zote mia moja

Kwa namna fulani hii ndio sababu ya kwanini bado huwa niko nao
 
Tatizo watu wa humu watatumia kama fimbo siku isiyo na jina..
Biashara zao ni hizihizi tu za kawaida maduka ya nguo viatu. Vipodozi mwingine home decorations na vitu kama hivyo

Sijui nisemeje lakini huwa wananishawishi kufanya vitu vya kijinga japo kwa akili sana,.
Lakini hawajafanikiwa
Vitu gani??๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
 
Sio rahisi kuacha kupokea vitu kutoka kwao ukizingatia umepokea since 2022 umesema tena vitu vya gharama na pesa.
Pia mmeshajenga na mazoea kabisa kama ndugu kabisa japo tabia zao huzielewielewi
Punguza mazoea na kuwa too available wakikuhitaji punguza kupokea vitu kutoka kwao punguza mdogomdogo, kama ni mawasiliano punguza mpaka uwe kimya watatazoea na kujiongeza kuwa hutaki mambo zao
Otherwise, ukiendelea utaishia kuwa kama wao kitabia
 
Tuendeleee

BAsi buana mdogo wenu nikaanza napendwa pekeyangu,. Mie ni mtu ambaye sio mtokaji kabisa yaani sijawahi kuhudhuria hata mtu wangu wa karibu awe anafanya birthday Party sijui nini mie sijawahi kuhudhuria huwa naagizaga tu zawadi,. Au labda niwe naenda na mama labda kuwe na harudi kitchen party na shughuli kama hizo mama akiniomba nimpeleke ndio huwa tunaenda wote,.
Lakini hawa wadada walinifanya nianze kwenda kwenye party za watu usiku, Yaani utakuta nimekaa tu sina hili wala lile napigiwa simu "Lee kuna namba nimekutumia hapo ya fundi uende akupime gauni Utalivaa Jumamosi kuna party mie nitakuletea kadi na viatu".. Kwa Approach kama hiyo jamani ningeweza kuchomoa kweli? Baasi nikawa naenda na nikifika kule kila mtu atatamani akae na mimi yaani nakeiwa kwelikweli hadi chooni nikitaka kwenda napelekwa๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„,.


Hawakuishia hapo,. Kuna siku alinipigia simu mmoja akasema nimepita ofisini kwenu nimeambiwa haupo uko wapi nikamwambia sijafika leo niko kwenye graduation ya mdogo wangu,. Akaniuliza tu wa kike au wa kiume nikamwambia wakike akasema nimwelekeze aje na zawadi basi akaja yeye na wenzie tunasherekea pale mda wa kutoka mie nikaondoka na kina mama na wao wakaondoka zao,.

Kuna siku nlikuwaga niko na stress zangu tu wateja walinivuruga sijui akili yangu iliwaza nini nikasema nimpigie huyu mdada tumwite "Tina " nikawa nimeongea nae tu akanotice kama siko sawa akaniambia nakuja kukuchukua,. Hii ndio siku ambayo nilikunywa pombe mwenzenu na nilikuja kustuka asubuhi,. Mama yangu alipiga simu missed calls sijui zaidi ya ngapi hata sikumbuki, dada na baba ndio kabisa maneno ambayo sikuwahi waza kama nitaambiwa na baba yangu basi siku hiyo niliambiwa kwenye meseji... Lakini cha ajabu huyu Tina wala hata hakustuka aliniambia tu Jiandae twende peramiho Hospitali,. Nikafika kule nikakata kadi nikapimwa malaria, na vihoma vingine vingine nikapewa na dawa halafu ndio akaniambia niwapigie simu nyumbani waje Hospitali halafu sisi tuanze kutoka tukutane njiani, Kwa jinsi nlivyokua nimechoka na ile midawa nliyokuwa nayo moto wote ulizimika waliamini tu labda nilizidiwa njiani nikasaidiwa๐Ÿ˜ฅ๐Ÿ˜“๐Ÿ˜‚

Story zisiwe nyingi jamani maana scenarios ni zilezile .......
Ila tu Kiukweli ni watu ambao wamekuwa wamenizoea sana naweza kusema wamenizoea kupitiliza na ndio cycle yangu ya sasa,. Na ninaweza kusema wameniharibu mnoo yaani mimi najiona kabisa sio yule Lee ambaye kila mtu anamjua japo najitahidi sana kuficha nyumbani wasigundue chochote,.

Nashindwa namna ya kuwaepuka jamani maana saizi ndio kabisa wananichukulia kama mwenzao tu,. Yaani wananiona mdogo wao kwenye kazi zao Japo sijawahi kufanya nao chochote kibaya zaidi ya Pombe.. Vishawishi vyao vyote niliweza, nimeweza na ninaweza kuvipangua ( Japo hii huwa naamini ni nguvu ya maombi ya mama yangu) .. Maana mda mwingine mmmh


Kwa namna ambavyo naishi nao saizi ni ngumu sana gafla kusema nipotezane nao,. Nimejaribu mbinu zote hadi kubadili namba za simu lakini ilisaidia nini unadhani?,. Watu wanakujua nyumbani hadi nakofanyia kazi zangu.. Natamani kuwatema moja kwa moja lakini kwa upande mwingine jinsi walivyo Supportive naona kama nitapoteza watu wazuri,. Lakini hapohapo nawaza isije wakaniingiza kwenye matatizo ukizingatia ni watu ambao najioneaga aibu hata kusimama nao njiani isije watu wanaoniheshimu wakaniona nao wakanidharau,.
Sijui nifanye nini kwakweli ila ndio hivyo buana

Mwishooo,.
Mpaka sasa miaka miwili ni kipi kibaya wamekufanya?

Mambo gani umeyaepuka?
 
Binafsi umenichanganya kwenye title ya uzi tu...huko kwingine kwenye hadithi yako unaeleweka

Au ulivyoandika "why should i confess? "ulitaka kumaanisha nini kwa kiswahili chake?
Nilimaanisha kwanini nikiri kwamba niko nao?,. Ningeweza kuwa nao tu hivihivi kimyakimya na maisha yakaendelea lakini naogopa wataniingiza matatizoni,.

ILi labda niweze kusaidika lazima niconfess kwanza am occupied,. But why?๐Ÿ˜‘๐Ÿ˜ƒ
 
Nilimaanisha kwanini nikiri kwamba niko nao?,. Ningeweza kuwa nao tu hivihivi kimyakimya na maisha yakaendelea lakini naogopa wataniingiza matatizoni,.

ILi labda niweze kusaidika lazima niconfess kwanza am occupied,. But why?๐Ÿ˜‘๐Ÿ˜ƒ

Hapo hakuna unachokunywa Leejay49 ?๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
Manake kwenye uzi wako umekiri kuwa una vijitabia vya pombee kutoka kwa hao mashangazi ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Back
Top Bottom