Sehemu yoyote ambayo haina matumaini ni rahisi sana kuingiliwa na wimbi la ugaidi.
Tusijidanganye kwamba tunaweza kuyafumbia macho matatizo ya watu wengi sana ya kiuchumi, halafu tubakie salama tu kwenye mambo kama ugaidi.
Vijana ambao hawana ajira, hawana elimu na hawana matumaini ni rahisi sana kurubuniwa au hata kujirubuni wenyewe kwamba ugaidi ni kitu sahihi cha kufuata.
Nakumbuka mwaka 1990 wakati nakatiza Upanga hapa Kanisa la Immaculata, mkabala na ubalozi wa Iraq, barabara ya Umoja wa Mataifa, karibu na daraja la Salender, nilikuwa naona watu wengi sana wamejipanga nje ya ubalozi, walikuwa wanafuatilia namna ya kwenda vitani (siku hizo vita ilikuwa imeanza kati ya Marekani na Iraq).
Wale masela wengi walikuwa wanasema wanatafuta njia ya kutoka nje ya Tanzania tu waende kutafuta maisha nje. Yani katika akili zao, waliona ni bora kwenda vitani ili kutoka Tanzania, kuliko kukaa Tanzania.
Na mpaka leo, ingawa kuna wengi wamehubiriwa mahubiri ya ugaidi, kimsingi inakuwa rahisi kuwapata kwa sababu nchi yao wenyewe haijawapa matumaini, elimu wala kazi.
Kibaya zaidi, wanaona wenzao ambao wana connections mambo yao yanaenda poa, hata kama hawana qualifications.
Watu wanaona bora wajilipue tu.
Na ikifikia sehemu serikali yenyewe haikubaliki na wananchi, mara imeharibu ununuzi wa korosho, mara imenyanyasa wapinzani, hata baadhi ya wananchi wanaweza kuona hao magaidi wana point, ni kama freedom fighters.
Siwatetei, naeleza hali inayosababisha mtu kujiingiza katika vikundi hivi, na tatizo hili kukua zaidi.