Wiki mbili zitanitosha kujua gari?

Wiki mbili zitanitosha kujua gari?

zinakutosha, pia nikukumbushe kujua kuendesha gari ni pamoja na kujua sheria na alama za barabarani, Kila la heri
plus basic knowledge ya matatzo madogo madogo, mfano kuchek oil kwa enjine, brake fluids maji kwa rejeta na vingne
 
Ahsanteni wapenzi wangu. Leo nimeanza rasmi mafunzo ya driving.

Darasa linaenda vizuri.
 
Zinatosha kujua kuendesha,hazitoshi kujua alama barabarani na manuva,kuendesha sehem km Dar na ubabe nao unahitajika,..
 
Kasheshe la kubadili gia lol
Sio kazi,kama unafahamu auto,manual lisaa limoja tu unatambaa,muhimu ufahamu gia gani iko sehemu gani na ui ngage Kwa mtiririko wake.
Gear lever yenyewe inaonyesha mtiririko ulivyo
220px-Manual_Layout.svg.png
 
Tatizo sio kujua sheria na alam za barabarani,
Tatizo ni kujiamini na kutokuwa na woga uwapo barabarani.
Umenigusa mkuu mpaka kesho siendeshi gari sababu naogopa mnoo yaan kitendo cha kukaa kwenye usukani presha inapanda...... natetemeka mwisho naamua kuacha ila natamani kweli.
 
Umenigusa mkuu mpaka kesho siendeshi gari sababu naogopa mnoo yaan kitendo cha kukaa kwenye usukani presha inapanda...... natetemeka mwisho naamua kuacha ila natamani kweli.

Fanyia kazi hiyo kitu, jiamini, usiogope as long as upo upande wako. Ukijiamini na kutokuwa na uwoga gari kwako itakuwa rahisi, ila ukikosa hivyo hata nguvu ya kusoma vibao/alama za barabarani utashindwa.
 
Katika kuendesha gari wanashauri kuondoa hofu (driving phobia) , ndiyo chanzo cha kupata matatizo ya wakati wa kujifunza udereva , mfano Mimi wakati najifunza miaka 15 iliyopita na auto zilikuwa si nyingi sana , nilikuwa nikiona gari linakuja kasi Mimi nawaza kupaki pembeni apite kwanza ,sasa kwa style hiyo yangu ningeweza kufika kweli kwenye udereva makini
 
Back
Top Bottom