Wiki yenye utata: Tulianza na Dr Kigwangalla akaja Kangi Lugolla akafuatia Zitto halafu RC Makonda na sasa ni Mtume na nabii Mwamposya aliyekamatiwa !

Wiki yenye utata: Tulianza na Dr Kigwangalla akaja Kangi Lugolla akafuatia Zitto halafu RC Makonda na sasa ni Mtume na nabii Mwamposya aliyekamatiwa !

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubaliana sana na wewe. Watu wenye elimu yao wanajua fika ukiumwa nenda kamuone Daktari. Walijua Ukimwi haukua umepata dawa ya kuutibu. Wanapanda maVX yao na hata helikopta kwenda kunywa kikombe cha Babu kule Loliondo! Kweli elimu bila maarifa ni sifuri.
 
Makonda atawakondesha ,bado hamjasema
Kufa kila mtu atakufa. Nimehuzunishwa na wenzetu waliokufa kwa kukosa maarifa.

Lakini lililohuzunisha, kusikitisha na kutia hasira kuliko yote, ni hili la Makonda.

Wakati tunahangaika kujua ni nani anawaua watanzania wenzetu, ni nani anawapoteza watanzania wenzetu, ndipo tunaletewa taarifa inayosema kuna uhakika mkubwa kuwa Makonda amekuwa akiwadhulumu watu haki ya kuishi. Hili limekuwa jambo kubwa kuliko yote tangu mwaka uanze.

Yaani aliyefikiriwa kuwa ni kiongozi, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, aliyestahili kulinda uhai wa kila mtu, ndiye anayewaondolea watu haki ya kuishi!! Kwa hili tushirikiane kupaza sauti zetu ndani ya mipaka ya nchi yetu hata mpaka kingo za Dunia.

Unaweza kumkwepa adui anayejulikana ni adui. Lakini mtoto utamkwepa vipi mzazi ambaye amepanga kukuondolea haki ya kuishi?

Huyu mtu amewaondolea watu wangapi haki ya kuishi? Alikuwa anawaondolea akiwa na akina nani? Anatumwa na nani? Ameruhusiwa na nani? Watekelezaji ni nani? Ni maswali yanayoumiza japo hisia tunazo za majibu kwa haya maswali yote.

Tunajua Mungu wewe ni mwenye huruma. Tunaomba uwahurumie waliodhulumiwa haki yao ya kuishi uliyowapa. Laana kubwa izidiyo zote, na ikawe kwa mdhulumaji huyu, na hata na vizazi vyake vingi vijavyo.

Muumba wetu uendelee kutusamehe sisi sote maana kila siku tunakukosea lakini usitupatie msamaha wowote pale tunapodhulumu haki ya watu wengine kuishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom