Wikiendi Njema: Maombi yangu kwa wanawake wote wa JF wawe wenye kutenda haki na kuwa kwenye unyoofu

Wikiendi Njema: Maombi yangu kwa wanawake wote wa JF wawe wenye kutenda haki na kuwa kwenye unyoofu

ndio,,, mbona kushangaa ni ajabu😳au ulitaka uje utupe ndoano 😂😂mana nmeona likes zako kwangu unabidii😆😆
Hahahah nilitaka niteke attention yangu kwako ila kama una mtoto basi 🙌.

Uwe na weeknd njema Ms R 😊
 
iba namba za mademu kwenye cm ya mshkaji wako then tupia kamba,, mbon una uandishi mzuri tu.
Hahaha kwenye uandishi nipo vizuri ila face 2 face ndo changamoto 😢.

Sijui nifanyeje 😣 siwezi iba kwenye simu za washkaji maana kuna password huko
 
Hahaha kwenye uandishi nipo vizuri ila face 2 face ndo changamoto 😢.

Sijui nifanyeje 😣 siwezi iba kwenye simu za washkaji maana kuna password huko
basi kaa na shda zako mi ndo huniwezi ivoo imekula kwako.
 
Aaah huu uzi utakuwa umecopy, haiwezekani mwandiko unyooke hivi!
 
Amina,ubarikiwe Kwa ujumbe mujarab! Afisa ubashiri!!
 
BINTI YANGU NJOO NIKUAMBIE HAPA.

Mithali 20:7
[7]Mwenye haki aendaye katika unyofu wake, watoto wake wabarikiwa baada yake.

Haki katika ndoa yako ambayo Mungu amekupa hakikisha unaishi katika haki, wamama wengi siku hizi hasa hawa mabinti wanajivunia watoto wao wakiwa wazuri wa sura, wakiwa na akili darasani, na akivaa nguo inamkaa utasikia wanangu wana damu za nguo jamani.

Yaani ndio imekuwa mada yaani umeona watoto wa wengine ni kama vigengedere tu.

Sasa ni hivi mmeacha kuomboleza, mmeacha kumtumikia Mungu, mmeacha kuheshimu ndoa zenu, yaani mmeacha kuwa wenye haki.

Andiko tajwa hapo juu linazungumzia mzazi atakae kwenda ktk unyofu wa haki hakika watoto wake watabarikiwa badala yake, yaani watoto watarithi nini kutoka kwako?

Natamani Ukue uone jinsi gani Dunia imeharibika nje kumeoza ni kwamba Kama jamii haiko salama basi watoto wako hawako salama.

Acha kujipiga msamba tamani kuwa mama muombolezaji na uwafanye watoto wako wana wa Mungu.

Ni maombi yangu watoto wetu wawe wana wa Mungu.
YESU LUGHA YANGU.
Jadda una lolote la kusema?
 
Back
Top Bottom