Bahati nzuri nimefanikiwa kupita vijiji vya asili vya wachaga na wapare miaka hii ya karibuni, na kwa uchache ninaweza kusema wazi, japokuwa mpare ni mtu nisiyemkubali kabisa kwa sababu zangu binafsi lakini kwa sasa hatua ya kimaendeleo kijamii huko kwao ni kubwa maradufu ikiwa utamlinganisha na mchaga.
Nimefika maeneo ya wapare niliyoyaona ni haya.
1. Ni kweli barabara kuu ya lami umefika mpaka huko mwisho wa milima ya wapare (usangi) na karibia eneo lote kuelekea upande wa ugweno. Kwenye barabara ni hakika, kwa namna ya jiographia ya eneo husika ilivyo, nisingetegemea kukuta ubora ule.
2. Huduma za umeme, na upatikani wa maji ya uhakika ya bomba nyumba kwa nyumba huenda ni zaidi ya Dar. Wako vizuri.
3. Ubora wa nyumba ni mkubwa mnoo. Kwa mtazamo wangu ni nzuri na bora zaidi kuliko uchagani.
4. Tamaduni za kijadi za kutambika, ushirikina au ulevi hazipo kabisa upareni, haziruhusiwi na jamii yenye hizo tabia hutengwa kijamii. Naona dini (uislamu, ulutheri na usabato) zimeshika kasi zaidi. Vitu ambavyo kwa macho yangu nimevikuta uchagani na wachaga wanajivunia navyo.