Jana Jumamosi Februari 19, 2022 Wilayani Iramba Mkoani Singida pamefanyika Kongamano kubwa sana la Madini lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Suleiman Mwenda na kuhudhuriwa na Wadau mbalimbali wa Madini wa ndani ya Wilaya na kutoka Makao Makuu huku Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Lemomo Kiruswa akiwa Mgeni rasmi akimuwakilisha Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko.
Naibu Waziri Kiruswa alisema "Kwa mara ya kwanza Mimi ndo nimesikia suala hili kwa Mkuu wa Wilaya kuandaa Kongamano kubwa kama hili la Madini. Kwakweli niwe mkweli, Wewe (DC Mwenda) ni DC pekee ndani ya mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla kuandaaa kongamano la Madini. Sijawahi kusikia Mimi. Kwakweli katika hili nikupongeze sana Mkuu wa Wilaya hii ya Iramba kwa ubunifu huu. Kongamano hili litasaidia sana kuona fursa na changamoto zilizopo kwenye Sekta yetu ya Madini kwenye Wilaya ya Iramba."
"Lakini Kongamano hili limekuwa na mafanikio makubwa sana, natarajia litafanyika Kongamano kubwa kama hili kwa ngazi ya Mkoa na litasaidia sana."