"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza ya Uponyaji kwa Imani. Kila Mtu Anazo!

"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza ya Uponyaji kwa Imani. Kila Mtu Anazo!

Kuberi afunikaye Majini ni kama binadamu tu! Sote tupo duniani kwa ajili ya kumuabudu Mungu! Kiukweli kabisa Majini wananguvu na uwezo zaidi yetu!
Vile vile majini wako wema na wabaya!
...
Wema hawana madhara kwa binadamu, wanamuabudu Mungu, na kufanya kila jambo jema! Wale viumbe wanatabia ya kupenda wanadamu, so, jini mwema akimpenda mwanadamu, humlinda binadamu huyo na maovu either ya kutendewa or anayotenda huyo mwanadamu! Jini hatokosa masharti akimpenda mwanadamu, masharti hayo ukienda kinyume ndio hapooo utakapoona mzuka wa jini!
...
Sasa basi jini mwema kama huyo, hauwezi kumtoa kwa maombi ya bible or Qurani, coz yeye mwenyewe ni mjuzi wa hivo vitu na ANAAMINI anachokifanya sio kibaya! So ukitaka kumfurusha huyu utafute jini aliemzidi nguvu tu! Tena kuna hatari hata usifanikiwe coz anaweza kukublock katikati ya process!
...
Majini mabaya ndio wanadhuru watu bila sababu, wanafanyisha watu vitendo viovu ie sodoma na uovu mwengine!
Majini hawa nawafananisha na majambazi, wizi, walaunga, wavuta bangi, malaya na wengineo!
...
Majini hawa ukiwapiga kisomo cha dini Quran/Bible ni lazima wadhurike na kukimbia mbio nyingi sana, kwa sababu wanajijua wao ni waovu.
...
Sjui nimeeleweka hapa.

nimekuelewa vizuri sana mkuu,thanks a lot for your contribution.Tatizo tu jibu hili linapingana na mafundisho ya imani yangu,ningekuwa muislam isingenisumbua lakini sie wakristo tunaamini majini wote ni evil,ni malaika tu ndio kuna wazuri na wabaya(mashetani).Sina uhakika kama biblia iko detailed na suala la aina za mapepo,majini n.k. labda mwenye ujuzi wa biblia anielekeze.Hata hivyo kuna jambo naligundua kila siku kwenye maisha,kwamba inaelekea ukweli unasimama wenyewe,hautegemei kitu kingine chochote,so unapoutafuta lazima uwe free minded sana ili kuelewa.Ngoja nilifanyie kazi na hili la majini wazuri na wabaya kujua ukweli wake na kama bible inasapoti.Thanks a lot mkuu Mashaxizo
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Pasco nina swali kuhusu mada uliyoleta,je,Mungu anatumia njia gani kuhakikisha binadamu hawa-abuse hizi powers alizowapa?Je,jinsi shetani anavyotudanganya na kutuingiza kwenye uasi,anatumia will powers zake?(maana na yeye ni kiumbe wa Mungu),au anamanipulate will powers zetu,au ana negotiate na will powers zetu?Nauliza hivi kwa vile umesema mtu anaweza kuinvoke hizi nguvu mwenyewe tu,wakati sie wengine tunaamini kuwa kuna path ya kupita(jina la Yesu) ili kuinvoke hizi powers kwa matumizi sahihi anayoyataka aliyezitoa.
 
Last edited by a moderator:
Duh!nimechoka kabisa.umekwenda deep sana mkuu ila hapo kwenye suala la spirit za wafu kuendelea kuishi kama mizimu ni pagumu kweli kwangu kumeza maana mafundisho ya biblia ni contrary na hii belief kabisa unless sijaifahamu tafsiri sahihi ya biblia on this matter.I only consider your answer because so far you are the only person to give me such a logical answer to my question but now another question comes in my mind,does it mean kwamba kuna kasoro kwenye mafundisho ya mainstream religions kuhusu hii dhana ya spirits?naumiza kichwa kwa vile nataka kujua status ya zile spirits zisizo za kawaida zilizompanda ndugu yangu.Unajua kitendo cha mtu mmoja kuamrisha mwingine kuumwa na akaumwa kweli si kawaida,kwa sababu kila mtu ana ulinzi wa Mungu,yaani hapo ndio palinichanganya,how powerful were these spirits?na wametaka mtu awe mcha Mungu,amekuwa hivyo,wameondoka hadi leo hawajarudi,so they were serious about that na si kutuhadaa!sasa jini gani huyu anaamrisha ibada kwa Mungu na utu wema?so far hili ni jibu pekee logical nililopata kwa swali langu in 20 years,ngoja nikalifanyie research mkuu kwenye kipengele hicho cha wafu kugeuka mizimu,halafu ntarudi.Ahsante sana mkuu for a very,very logical and detailed answer.
Mkuu Kerubi, kila kitu kimeelezwa kwenye Biblia, hivi unadhani huo uzima wa milele watu wanaushi vipi?!. Roho ikiisha umbwa, haifi milele, kinachokufa na kuoza ni mwili tuu!, hata watenda maovu, nao pia hawafi milele, wataendelea kuungua na kuteseka kwenye jehanum ya ziwa la moto wa milele.

Kuna vitu vimeelezwa kwenye Bibilia lakini tunavitafsiri vibaya, mfano mbinguni is usumed ni kule juu mbali sana, mawinguni!. I reality, mbinguni ni hapa hapa duniani ila ni kwenye spiritual world. Yesu kabla ya kuteswa kwake alifunga siku 40 na alijaribiwa na shetani!. Kuna wakati katika sala fulani, Petro alimuona Yesu akiomba, na akaoziona taswira za Musa na Eliya!. Hizi zilikuwa spirits!.

Yesu baada ya kukufuka, japo alikuwa na mwili wake, lakini aliishi kwenye spiritual world, alikuwa akiwatokea tuu watumishi wake!. Bikira Maria pia amewahi kuwatokea wale wanawake watatu wa Fatima pale Louders Ufaransa!.

Fuatilia kwa makini vitabu kama Ufunuo wa Yohana, unazungumzia siku za mwisho na mambo mengi ya ulimwengu wa roho!.

Mungu anaeleza yuko popote, ni omniscience, omnipotent, na omnipresence, hizi existance zote za Mungu, zina exist in spiritual form, Roho Mtakatifu ni spirits, na malaika wana exist in spiritual form, hiyo inayoitwa mizimu, ndio malaika wema na wako in spirit form, vivyo hivyo shetani naye ni omnipresent, ana exist in spiritual form, na malaika wake ndio hao wanaoitwa majini, na mapepo wachafu, na mashetani, they exist in spirits!.

Naomba nisizame sana ndani ya dini, wasije wakaja humu wale watu wenye vichwa nazi, akili zao zikiwa ngumu kama jiwe ambao wameaminisha moja na moja ni mbili, ukiwaambia pia moja na moja inaweza kuwa ni moja moja, tutaishia kubishana humu mpaka asubuhi!.
Pasco.
 
nimekuelewa vizuri sana mkuu,thanks a lot for your contribution.Tatizo tu jibu hili linapingana na mafundisho ya imani yangu,ningekuwa muislam isingenisumbua lakini sie wakristo tunaamini majini wote ni evil,ni malaika tu ndio kuna wazuri na wabaya(mashetani).Sina uhakika kama biblia iko detailed na suala la aina za mapepo,majini n.k. labda mwenye ujuzi wa biblia anielekeze.Hata hivyo kuna jambo naligundua kila siku kwenye maisha,kwamba inaelekea ukweli unasimama wenyewe,hautegemei kitu kingine chochote,so unapoutafuta lazima uwe free minded sana ili kuelewa.Ngoja nilifanyie kazi na hili la majini wazuri na wabaya kujua ukweli wake na kama bible inasapoti.Thanks a lot mkuu Mashaxizo

Mkuu mimi ni Muslim na sina elimu ya Bible!
Wacha niwe neutral na nijaribu kukuambia kitu hapo.
...
Hivi vitabu vya dini haviko complete! I mean havijacover mambo yote na vipengele vyote! Hivyo basi, kama unataka upate elimu tofauti tofauti, usiegemee saana kwenye hivyo vitabu! Coz hivo vitabu vyenyewe vinashauri watu kutafuta elimu ktk vyanzo tofauti!
...
Angalia maelezo haya:
Islam inaichukuli bible kama kitabu kisichokamilishwa na kinachakachuliwa! (sorry kwa hili) Yesu aliondoka/ondoshwa/alikufa kabla ya kukamilisha ujumbe, bible iliandikwa na watu tofauti baada ya kundoka Yesu!
Thus why akaletwa Muhamad!
...
Kwa upande wa pili just jiulize kwanini kuna makundi mengi ya kidini wakati wote wanatumia kitabu hiko hiko? Kwa mfano: kuna Lutheran, catholic, Protestarant, na wengineo! Also kuna Sunni, Shia, Ibadh na wengineo!
The logic is that, kama vitabu vingecover angle zote kusingekua na hayo matabaka!
...
Also ukumbuke hivi vitabu viliandikwa zamani na kila leo kunaibuka issue mpya!
...
NB:
SIJAANDIKA KWA LENGO LA KUKASHIFU DINI YOYOTE! Its only matter of logic!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mashaxizo, yesi ukiamini huwezi kupata ukimwi, huupati, ila hizi nguvu ili zifanye kazi, unatakiwa kutenda yalio mema tuu, kuzitumia kutendea uovu, utaadhibiwa!, mimi baada ya kujitambua kuwa nikimtaka mwanamke yoyote, kwa kudhamiria, then lazima nimpate, awe ni demu wa mtu, mke wa mtu haijalishi, hivyo kwenye ujana, niliutumia vibaya, ilipofika muda wa payback, the price is too high!.

Mungu alisema piga hodi, utafunguliwa, tafuta utapata, this means ukiomba chocho utapewa, ila usi fanye abuse of powers!.

Mfano ukiamini mwizi hawezi kuingia nyumbani kwako, ni kweli mwizi hawezi kuingia, lakini usilale mlango wazi, simply tuu eti kwa sababu you have the powers kuwazuia wezi!. Vivyo hivyo, una powers za kuzuia ukimwi, usirande peke peku kwa makusudi simply because you have the powers, hiyo ni abuse, hivyo bakora utazipata!.

Hata hawa wanaotumia faith healing kuponya au kuzua magonjwa, ugonjwa ukikushika very seriously nendo hospitali, jana kuna mtu na mkewe wamefungwa jela kule Marekani kwa kosa la kuua bila kukusudia ambapo mtoto wao wa miezi 8 alipata ugonjwa wa pneumonia, wakampeleka kanisa la wokovu kuombewa badala ya hospitali, mtoto kafariki, wazazi ni jela miaka 8, kwa kukua bila kukusudia!.

Pasco.

Underline:
Mkuu ikiwa hizo nguvu zinatakiwa zitumike kwa mambo mema tu, ni kwa nini hata zikitumika kwa mambo maovu/mabaya zinafanya kazi???
...
Hapo blue unaweza kusema nini ulilipwa?
 
Mkuu Pasco nina swali kuhusu mada uliyoleta,je,Mungu anatumia njia gani kuhakikisha binadamu hawa-abuse hizi powers alizowapa?Je,jinsi shetani anavyotudanganya na kutuingiza kwenye uasi,anatumia will powers zake?(maana na yeye ni kiumbe wa Mungu),au anamanipulate will powers zetu,au ana negotiate na will powers zetu?Nauliza hivi kwa vile umesema mtu anaweza kuinvoke hizi nguvu mwenyewe tu,wakati sie wengine tunaamini kuwa kuna path ya kupita(jina la Yesu) ili kuinvoke hizi powers kwa matumizi sahihi anayoyataka aliyezitoa.
Mkuu Kerubi, kiukweli kuna vitu kwenye maandiko havikusemwa, mfano hakuna popote unapozungumzwa mwanzo wa shetani, ila tuu inaelezwa hapo mwanzo shetani alikuwa ndie malaika mkuu, akiwa na nguvu na mamlaka next to God.

Shetani alipomuasi Mungu, na vikapiganwa vita kati ya malaika watiifu na wale waasi, baada ya kushindwa ndipo yeye na malaika wake wakatupwa duniani(haikuelezwa kwa nini Mungu hakumuangamiza shetani!.

Baada ya uasi wa shetani ndipo Mungu akasemezana na malaika wake, tumuumbe kimbe kwa mfano wetu kitakacho tutii!. Mungu akamuumba Adamu, na haikuelezwa Adamu alikaa muda gani pekeyake ndipo akamuumbia mwanamke.

Kwenye andiko fulani nimesoma, baada ya Mungu kuwaumba binadamu, shetani alikwenda kuzungumza na Mungu na kumwambia utajuaje hawa viumbe kama wanakutii paspo kuwawekea vishawishi?!. Ndipo Mungu akamkubalia kwa kuwawekea kishawishi cha tunda la mti wa katikati wa mema na mabaya!.

Kisha Mungu akawaweka malaika wawili wenye upanga wa moto kwenye geti la kuingia bustanini Aden, ili shetani asiingie!. Shetani alijigeuza nyoka akapenya getini, kule ndani akajigeuza mwanamume mzuri, Eva kumuona akashtuka, ndipo shetani akamuuliza hivi viungo vimewekwa vya nini (tunda), Eva akamjibu tumekatazwa kuvitumia (wamekatazwa kula tunda), akamuuliza kwa nini?, Eva akamwambia alisema tutakufa!.

Ndipo shetani akamwambia Eva ukweli we mambo!, kuwa akimega tunda, atapata rahahaijawahi kutokea, ila pia wakimega "tunda" watakuwa na uwezo sawa na Mungu, kwa kujiumbia viumbe wengine wadogo (kuzaa watoto), na ilielezwa shetani alimega tunda na Eva, kisha Eva akamlazimisha Adamu "kumega" na wakaishia uzingizini, Mungu alipomuita Adamu, ndipo wakajistukia wako uchi, kwa sababu mwanzo hawakujua hivyo ni viungo vya nini?!.

Ikasemekana shetani ndio chanzo cha uasi kwa kuitengeneza tamaa, hivyo kitu kinachoitwa dhambi ya sili ndicho hicho, ili binadamu azaliwe, lazima lile tendo la dhambi ya sili lifanyike!, mtu pekee aliyekingiwa dhambi ya sili ni Bikira Maria, kwa kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu hivyo kumzaa Yesu bila kufanyika kile kitendo!.

Lengo la Mungu ni kwa binadamu kuzitumia hizi powers vizuri, lakini mission ya shetani ni abuse ya hizi powers. Mpaka sasa hakuna solid reasons kwa nini Mungu ameendelea kumuacha shetani akiendelea kuexist, kuwapoteza watu wake, na ndio maana Mungu ametupa utashi kumfuata yeye au kumfuata shetani!.

Unaweza kuinvoke hizi nguvu kwa Jina la Yesu na kuzitumia kufanya yaliyo mema, ukizitumia kufanyia uovu, then utakuwa unamtumikia shetani, ila kwa vile nguvu hizi zipo tangu existance ya mwanadamu, watru wengine wowote, hata wasiomwamini Mungu, wanaweza kuzinvoke na kuenda mema kama uponyaji bila kulitaja jina la Yesu, na bila kumtumikia shetani!.

Kufuati Mungu kuwa na nguvu zaidi ya shetani, ila shetani nae anazo nguvu fulani, unaweza kushangaa kuona baadhi ya watu wanaomtumikia shetani kama freemasons, na secret societies karibu zote, wana mafanikio makubwa, huku watu wa Mungu, wakiishi katika maisha ya dhiki na mateso, hivyo kujiuliza ni kwa nini Mungu hajamuangamiza shetani?!. Mimi jibu ninalo ila hupelekea kuleta ubishani sana, hivyo naomba nilisiseme humu, ukinitembelea kwenye uzi wangu huu [h=3]Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo ,[/h]utayakuta majibu huko.

Pasco
 
Underline:
Mkuu ikiwa hizo nguvu zinatakiwa zitumike kwa mambo mema tu, ni kwa nini hata zikitumika kwa mambo maovu/mabaya zinafanya kazi???
...
Hapo blue unaweza kusema nini ulilipwa?
Nguvu ni moja, ziko in a form of spirit, zikitumika kufanya mema, ndio zinaitwa nguvu za Mungu, zikitumika kufanya mabaya, zinakuwa ni nguvu za giza, ni za shetani!.
Pasco.
 
Nguvu ni moja, ziko in a form of spirit, zikitumika kufanya mema, ndio zinaitwa nguvu za Mungu, zikitumika kufanya mabaya, zinakuwa ni nguvu za giza, ni za shetani!.
Pasco.

Mmmh! Mkuu unazidi kunichanganya!
Nguvu za shetani si ni zile nguvu anazotumia mtu kupitia mashetani? Kwa mfano waganga wa kienyeji!
...
Mkuu umeelewa swali langu kweli? Au ni mimi sielewi?
 
Mkuu mimi ni Muslim na sina elimu ya Bible!
Wacha niwe neutral na nijaribu kukuambia kitu hapo.
...
Hivi vitabu vya dini haviko complete! I mean havijacover mambo yote na vipengele vyote! Hivyo basi, kama unataka upate elimu tofauti tofauti, usiegemee saana kwenye hivyo vitabu! Coz hivo vitabu vyenyewe vinashauri watu kutafuta elimu ktk vyanzo tofauti!
...
Angalia maelezo haya:
Islam inaichukuli bible kama kitabu kisichokamilishwa na kinachakachuliwa! (sorry kwa hili) Yesu aliondoka/ondoshwa/alikufa kabla ya kukamilisha ujumbe, bible iliandikwa na watu tofauti baada ya kundoka Yesu!
Thus why akaletwa Muhamad!
...
Kwa upande wa pili just jiulize kwanini kuna makundi mengi ya kidini wakati wote wanatumia kitabu hiko hiko? Kwa mfano: kuna Lutheran, catholic, Protestarant, na wengineo! Also kuna Sunni, Shia, Ibadh na wengineo!
The logic is that, kama vitabu vingecover angle zote kusingekua na hayo matabaka!
...
Also ukumbuke hivi vitabu viliandikwa zamani na kila leo kunaibuka issue mpya!
...
NB:
SIJAANDIKA KWA LENGO LA KUKASHIFU DINI YOYOTE! Its only matter of logic!
Mkuu Mashax, kwenye mada zangu be free hata kufanya ukosoaji wa dini yoyote in good faith, kwa kutumia just a reasonable common sense. Mimi ni Mkatoliki, sisi tumewekewa kabisa vifungu vya kosma kwenye Biblia, kuna vingine hatufundishi!, mimi nikasoma mwenyewe Biblia, mwanzo mwisho, nikakutana na contradictions kibao!, Bible inasema hivi, kanisa linafanya vingine!.

Kuna kipindi niliishi India, nikaisoma Budhiism, na Hinduism, ndipo nikafunguka macho!, kumbe Christianity na Islam ni dini za juzi juzi tuu, ukizama kwenye Vedas, unakuta Bible ni cha mtoto!. Pia nimesoma kidogo Quran Tukufu for some specific topic, nikakuta kumbe dini zetu hizi mbili za Ukristu na Uislamu, zote zinatumia sheria ile ile moja, sheria ya Musa, kwenye Ukristu inaitwa Kumbukumbu la Torati, kwenye Uislamu ni Taurat, na vitu kama kula ile "kitu" vimeharimishwa, Yesu alikulia Misri na alivaa Kiarabu, zile hijabu ndizo walizovaa kina Bikira Maria, ila wazungu katika kuifitisha kwenye mahitaji yao, wakafanya mabadiliko ili ifiti mambo yao!.

Ndio maana kwenye mada zangu, zijaegemea sana kwenye dini yoyote!.

Just be free to flow!.
Pasco
 
Mmmh! Mkuu unazidi kunichanganya!
Nguvu za shetani si ni zile nguvu anazotumia mtu kupitia mashetani? Kwa mfano waganga wa kienyeji!
...
Mkuu umeelewa swali langu kweli? Au ni mimi sielewi?
Usichanganyikiwa hata kidogo, aliyetuumba ni Mungu na ndie aliyetutia hizo nguvu!, ila Mungu huyo huyo, akamruhusu shetani kutia majaribuni, na akatuachia kitu kinatwa "utashi!" wa kuchagua kumfuata yeye au kumfuata shetani!.

Mfano mimi nilijikuta nimejaaliwa kipaji cha "high convincing power" its a positive power ikitumika vizuri, niliitumia nguvu hiyo kuwaconvince wanafunzi wenzangu katika kutenda yaliyo mema, na wakati nikiwa UDSM, japo sikuwa kiongozi, kutokana na ukaribu na viongozi wa Daruso, nilifanikiwa kuwashawishi wenzangu kutojiunga na migomo isiyo na tija!, na nilifanikiwa, au mtu akiwa na shida, kufanya ushawishi asaidiwe zikiwemo fund raising, hivyo nimezitumia nguvu hizi kutenda mema, hivyo ni kuzitumia vizuri kumpendeza Mungu!.

Lakini mimi huyo huyo licha ya kuzitumia nguvu hizo kutenda yaliyo mema, shetani naye akanipa kishawishi na kuwa na tamaa za ajabu za mambo ya kimwili!, hivyo nilizitumia nguvu hizo vibaya kuwaconvince wadada kunitimizia nilichokitaka tena bila kutosheka na kwa kuwabadili kama nguo!. Huo ulikuwa ni ushetani, hivyo nimezitumia nguvu hivyo kufanya yasiyompendeza Mungu ni kumtumikia shetani!.

Unaweza kukuta hao hao wahubiri waliojaaliwa vipaji vya uponyaji, wengine wakimiliki, makanisa makubwa, hadi bemki na vituo vya TV, wakiponya watu, kufukuza mapepo na kusaidia masikini, huku ni kuzitumia nguvu hizo kufanya kazi ya Mungu, laki hapo hapo unakuta wachungaji hao hao, huwarubuni waumini wao na kulala nao, wengine ni wake za watu na hadi kuzaa nao!, au kuutumia uwezo wao kuwakamua waumini wao hadi kubakisha mifupa, huku wao wakijilimbikizia mali na utajiri mkubwa!, wakivaa mavazi ya gharama,wakitembelea magari ya kifahari, huku wakiishi kwenye mahekalu yaliyojengwa by the beach!, at the expenses za waumini wao masikini!, huku ni kumtumikia shetani!.

Nilisema mahali kuwa the dividing line between nguvu za Mungu na nguvu za giza is very thin!. Usipotumia voices from within, unaweza kujikuta unajidhania unamtumikia Mungu, kumbe unamtumikia shetani bila kujijua!.
Pasco.
 
Mkuu Kamanda, sijasema popote Yesu haponyi nimesema Yesu alifanya miujiza ya uponyaji na hadi kumfufua Lazaro!.

Ninachozungumzia humu ni zile nguvu za uponyaji zinatoka wapi?!. Wengi wanaponywa kwa kutumia neno tuu "Katika Jina Yesu, Uponywe!", au mapepo yatoke!. Jee kinachoponya ni nini?!, ni hilo jina linaingia ndani yako na kukuponya?!, yaani wengi wanadhani ni jina ndilo linaloponya!, No!. Wengine wanadhani ukiisha lija "Kwa Jina la Yesu" hizo nguvu za uponyaji, zinatoka kwa yule muhubiri wa uponyaji, na Yesu analeta nguvu, na kukuingia wewe na kukuponya, na ndio maana ukiisha ponywa unaambia sema "Asante Yesu!".

Ninachofundisha mimi humu ni kuwa hizo nguvu, hazitoki kwa Mhubiri, wala haziletwi na Yesu!, hizo nguvu zimo ndani yetu, ziliwekwa na Mungu mwenyewe ile siku ulipotuumba kwa mfano wake!. Kinachofanywa na Jina la Yesu, ni kuzifungulia tuu hizo nguvu zilizoko ndani yako na kufanya muujiza wa uponaji, Jina la Yesu ni catalyst tuu, nguvu ziko ndani yetu, na namna ya kuzitumia ni kuamini tuu!, ndio maana hata Yesu mwenyewe, wale aliyewaponya, aliwaambia kilichowaponya ni "imani yao!".

Haya sio mambo ya NWO, hii nimkweli tuu ambayo sio wengi wanaifahamu na kuitumia!, nimekuambia sijakwenda hospital more than 20 years nikiumwa chochote ukiondoa ile ajali niliyoipata!, where does hiyo NWO comes in?!.

Kweli hii ninayoifundisha humu, ndio kweli hii hii iliyofundishwa na Yesu mwenyewe, tofauti yangu ni kuwa broader zaidi kuwa ukiamini kuwa you have the powers, hizi nguvu zitafunguliwa na kufanya uponyaji regardless wewe ni wa imani gani!.
Its about opening the gates of powers from within you!.
Pasco.

Umesema hizi nguvu tulizonazo zinatoka kwa Mungu halafu ukakubali Yesu ni mwana wa Mungu mwisho unasema Yesu hausiki mbona kama unajichanganya? nawe ni Mkatolikii...au
 
Usichanganyikiwa hata kidogo, aliyetuumba ni Mungu na ndie aliyetutia hizo nguvu!, ila Mungu huyo huyo, akamruhusu shetani kutia majaribuni, na akatuachia kitu kinatwa "utashi!" wa kuchagua kumfuata yeye au kumfuata shetani!.

Mfano mimi nilijikuta nimejaaliwa kipaji cha "high convincing power" its a positive power ikitumika vizuri, niliitumia nguvu hiyo kuwaconvince wanafunzi wenzangu katika kutenda yaliyo mema, na wakati nikiwa UDSM, japo sikuwa kiongozi, kutokana na ukaribu na viongozi wa Daruso, nilifanikiwa kuwashawishi wenzangu kutojiunga na migomo isiyo na tija!, na nilifanikiwa, au mtu akiwa na shida, kufanya ushawishi asaidiwe zikiwemo fund raising, hivyo nimezitumia nguvu hizi kutenda mema, hivyo ni kuzitumia vizuri kumpendeza Mungu!.

Lakini mimi huyo huyo licha ya kuzitumia nguvu hizo kutenda yaliyo mema, shetani naye akanipa kishawishi na kuwa na tamaa za ajabu za mambo ya kimwili!, hivyo nilizitumia nguvu hizo vibaya kuwaconvince wadada kunitimizia nilichokitaka tena bila kutosheka na kwa kuwabadili kama nguo!. Huo ulikuwa ni ushetani, hivyo nimezitumia nguvu hivyo kufanya yasiyompendeza Mungu ni kumtumikia shetani!.

Unaweza kukuta hao hao wahubiri waliojaaliwa vipaji vya uponyaji, wengine wakimiliki, makanisa makubwa, hadi bemki na vituo vya TV, wakiponya watu, kufukuza mapepo na kusaidia masikini, huku ni kuzitumia nguvu hizo kufanya kazi ya Mungu, laki hapo hapo unakuta wachungaji hao hao, huwarubuni waumini wao na kulala nao, wengine ni wake za watu na hadi kuzaa nao!, au kuutumia uwezo wao kuwakamua waumini wao hadi kubakisha mifupa, huku wao wakijilimbikizia mali na utajiri mkubwa!, wakivaa mavazi ya gharama,wakitembelea magari ya kifahari, huku wakiishi kwenye mahekalu yaliyojengwa by the beach!, at the expenses za waumini wao masikini!, huku ni kumtumikia shetani!.

Nilisema mahali kuwa the dividing line between nguvu za Mungu na nguvu za giza is very thin!. Usipotumia voices from within, unaweza kujikuta unajidhania unamtumikia Mungu, kumbe unamtumikia shetani bila kujijua!.
Pasco.

Ok! Kwa kuconnect na maelezo ya thired yako iliyopita (inayohusu psychic power) NIMEELEWA!
 
Umesema hizi nguvu tulizonazo zinatoka kwa Mungu halafu ukakubali Yesu ni mwana wa Mungu mwisho unasema Yesu hausiki mbona kama unajichanganya? nawe ni Mkatolikii...au
Mkuu Micro, kiukweli unahitajika uelewa wa ziada kuilewa trinity vs spiritual powers. Kwa sisi Watoliki, Mungu Baba (God) ni Mungu, Mungu Mwana Yesu ni Mungu, na Roho Mtakatifu naye pia Mungu, ambapo tunaamini Mungu ni mmoja ila anazo nafsi tatu tunazoziita Utatu Mtakatifu, yaani Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Katika uumbaji, hizo nguvu za Mungu wakati akituumba, Yesu na Roho Mtakatifu walikuwepo, hivyo huyo Mungu aliyemo ndani yetu, pia Yesu yumo ndani yetu na Roho Mtakatifu yumo ndayi yetu in a form of powers, yaani zile powers za Uuungu Mungu alizotupa, ndio Yesu, ndio Roho Mtakatifu kwa mujibu wa Katoliki, hivyo kulitaja jina la Yesu, chenye nguvu sio jina!, chenye nguvu ni Godly powers zilizomo ndani yetu zimehifadhiwa kwenye sanduku, hivyo kulitaja jina la Yesu, kunatoa ufungua wa kulifungulia tuu hilo sanduku na kinachotenda miujiza, sio nguvu kutoka nje, bali zilizoko sandukuni ambapo Jina la Yesu limetumika kuzifungulia!.

Kwa vile watu wote tumeumbwa na Mungu, hata wengine wote wasiomuamini Yesu, pia wanazo nguvu hizi, na kutumia imani ya kile wanachokiamini, hutumika kama ufungua wa kulifungua sanduku la nguvu hizi kutenda miujiza!. Waislamu wakititumia jina la Allah na Mohammad (SAW) ni Mtume wake kuzifungua, zitafunguka, Wahindi wakimtumia Krishna, zitafunguka, Waumini wa Budhiism wakimtumia Budha, zitafunguka!, Wasukuma wakilitumia jiwe, zitafunguka, Wachagga wakimwaga mbege, zitafunguka, Wazaramo wakicheza ngoma, zitafunguka!. Yaani hizi powers ziko lwa binadamu wote, tumepewa freely regarless unaabudu nini, hata asiyeamini kabisa uwepo wa Mungu, anazo na akiitumia imani yake kwa kuamini chochote anachoamini, iwe ni mti, jiwe, maji, kisima, jua, mwezi, nyota, juust name whataver unachoamini, kinazifungua nguvu hizi na zinafanya uponyaji/miujiza!.
Pasco.
 
Hata ukivunjika mguu utaunga tu na utapona.Daktari anavalisha tu P.O.P na kazi nyingine unaifanya mwenyewe kwa kutumia healing power uliyonayo. Kanuni inayotumika ni Law Of Growth. Kupona pia unapswa kuamini . Yaani faith.Watu wengi hawajui maana ya faith. Hufikiri faith ni dini.
 
Nakupata vizuri sana Pasco,inahitaji usome hizi nyuzi kwa kutulia sana ndio utaelewa uwepo na ufanyaji kazi wa hizi Powers.Hapa kuna kitu nataka kujua,ninapokuwa ninasali sasa hivi nimeshaanza kuamini kuwa huwa nafanya kazi ya kuamsha nguvu zilizo ndani yangu mwenyewe ili zifanye kazi,kuna mtu kanishauri kuwa wakati mzuri wa kuomba/kusali ni usiku kati ya saa 6 usiku na saa 10 usiku,naomba unieleze the logic behind ya kwanini usiku na sio mida mingine ili kuamsha hizi powers to work effectively?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,
mada yako ni nzuri sana, samahani kama nitakuwa nje ya hii mada, nataka kufahamu juu ya kitu kinachoitwa maono. kuna wachungaji wengine anaweza kukupa maono kuhusu jambo litakalokutokea na likatokea au lilokutokea hapo nyuma, hii inakuaje/ inatokeaje/ nguvu hii inapatikanaje? Mfano kuna jamaa yangu aliasi familia yake akahamia nyumba ndogo, Mke mkubwa alianza maombi na kufunga baada ya wiki akaja nae kanisani, mchungaji alisema maneno mawili, rudi ulee familia yako vinginevyo kuna jmbao baya litakutokea, jamaa alipuuza within a month jamaa alipatwa na kiharusi akapooza hadi kupelekwa ICU, mwisho wa yote kilichomponyesha ni maombi na kurudi nyumbani na kuomba radhi kwa mkewe. ni mkasa mrefu sana wa kusikitisha. ila naomba kufahamisha juu ya MAONO/ utabiri. na jinsi ya kutafsili ndoto/njozi nawasilisha
 
kwa
Nakupata vizuri sana Pasco,inahitaji usome hizi nyuzi kwa kutulia sana ndio utaelewa uwepo na ufanyaji kazi wa hizi Powers.Hapa kuna kitu nataka kujua,ninapokuwa ninasali sasa hivi nimeshaanza kuamini kuwa huwa nafanya kazi ya kuamsha nguvu zilizo ndani yangu mwenyewe ili zifanye kazi,kuna mtu kanishauri kuwa wakati mzuri wa kuomba/kusali ni usiku kati ya saa 6 usiku na saa 10 usiku,naomba unieleze the logic behind ya kwanini usiku na sio mida mingine ili kuamsha hizi powers to work effectively?
Ili nguvu ziamke zinahitaji utulivu, ukimya, na concentration for peace of mind, hivyo usiku ni ideal time kwa ukimya.

Kusali kunasaidia kujenga imani ya kuzifungua nguvu as a form of meditation and concentration, hata kwa wasio wakristu waki concentrate watafungulia hizo nguvu.
Pasco
 
Juzi nimeota navuta bangi, kiukweli nimeacha kutumia hii kitu kitambo. Nilipoamka niliikumbuka ndoto nikaipotezea. Saa tatu nikaenda kunyoa ndipo nilipojistuki jicho jekundu isivyo kawaida. Pasco kunalolote umaweza niambia. Nilichoandika ni ukweli wanajamvi msidhani naleta utani ni ukweli kabisa
 
Back
Top Bottom