William Lukuvi anaandaliwa kuwa Spika wa Bunge la JMT?

William Lukuvi anaandaliwa kuwa Spika wa Bunge la JMT?

Unataka ccm ionekane kama chama chenye kujali sana haki na kupigania maslahi ya wananchi sifa ambayo hicho chama hakina kabisa.

Kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakiwadhulumu wananchi ikiwa ni pamoja na kuwatawala kwa nguvu pasipo ridhaa yao kiasi kwamba sasa hivi hata uchaguzi hamna kabisa katika nchi hii.
 
Kwa kazi aliyoifanya ardhi na ili asichafuke kulinda heshima yake asiangaike na usipika
 
4-1-2022
kati ya saa tatu hadi saa tano unusu usiku
William Lukuvi anafanya majadiliano na baadhi ya vijana wa Dar es Salaam baadhi wakiwa watumishi wa serikali eneo la Masaki na katika maongezi mmoja wao kwa jina la William Ndaki anauliza itakuwaje kama Rais atamtengua nafasi ya Uwaziri.

Siku mbili baadaye maeneo haya kinafanyika kikao kilichompa wazo William Lukuvi alikuwa akifanya mazungumo ya simu asubuhi saa nne na dakika kumi na baadaye mazungumzo ya ana kwa ana mchana na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda.

William Lukuvi anaomba miadi na Kwa Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda kumueleza kuwa anafahamu kuwa tayari yeye ni tatizo amechafuka baada ya Rais kusema anafanya mabadiliko ya baraza la mawaziri.

Anaeleza kuwa anachotaka yeye ni Mizengo Pinda kumuhakikishia kuwa endapo atachukua fomu ya Uspika jina lake litarudi kutoka kamati kuu na kuwa mgombea wa nafasi ya Uspika endapo atatemwa kwenye baraza la Mawaziri.

Mizengo Pinda anamuomba muda ili apate nafasi kumjibu. Usiku wa siku inayofuata tarehe 7-1-2022 wanazungumza na Stephen Wasira na mkutano mwingine unapangwa.

Mtaa wa Mwangosi Dodoma zilipo baadhi nyumba za Lukuvi wanakutana Geoffrey Mwambe, Luhaga Mpina, Job Ndugai, Leornad Chamuriho pamoja na Lukuvi mwenyewe ndipo walipokutania. Kwa mara ya kwanza wanakutana na kumpa pole Aliyekuwa spika Job Ndugai.

8-1-2022
Mkutano wa pili unafuata kati ya Lukuvi na Kabudi, Lukuvi anapewa go ahead kugombea Uspika na mratibu wa kampeni ni Luhaga Mpina anakabidhiwa kazi hiyo.

08-1-2022
Lukuvi anaanza mawasiliano na Wajumbe wa NEC akitumia mmoja ya wanawake ambao amekuwa na uhusiano nao wa kimapenzi bungeni, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 38 ni mjumbe wa NEC kutoka kanda ya Kati.

Mjumbe anaeleza kuwa anataka bajeti milioni 150 kwa ajili ya wajumbe na siku hiyohiyo anaanzisha group sogozi la whatsapp kwa Siri anaanza kuwaadd watu wa karibu Na Lukuvi Bungeni ambao wengi wao ni wabunge. bahati mbaya anamuadd Mbunge mmoja ambaye ni kitengo bila kujua.

Mchana wa tarehe 8-1-2022.

Lukuvi na mwanae wanashauriana kutafuta watu wa kumsaidia kwenye mitandao ya kijami anamueleza lengo lake Na Mtoto wa Lukuvi anakutana na Gladness Lyamuya anamuunganisha na KAWI SHAYO na wanataka kawi atumie akaunti zake za instagram kusifia kazi za Lukuvi kwa sasa.

Lukuvi anasema anaweza kumpa milioni 15 kwa kazi hiyo tayari mwanadada ameshaanza kazi na hela zimeweka kupitia equity bank. Huyu kawi ndiyo mwenye akaunti ya Originaleast zamani sasa ana akaunti inaitwa Politics mtandao wa insta.

Alfajiri ya tarehe 9-1-2022 kupitia Group la Whatsapp. Lukuvi, Job, Mwambe, kabudi, Mpina, Kalemani, Chamuriho wameanza kuchangishana Pesa ili Lukuvi Awe Spika".

Asubuhi ya leo Lukuvi bila kujua anarekodiwa ameenda nyumbani kwa Frank Mtei kumuomba pesa azungumze na shabiby pamoja na matajiri wengineo wa Dodoma kwa ajili ya mbio za Uspika.

Ntawajuza zaidi.
Kuna kosa gani la maadili rushws ama? Sielewi?
 
Ndiyo nafasi ya spika inaweza kugombewa na mtu yeyote mwenye sifa za kuwa mbunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ili uwe mbunge si lazima utokane na chama cha siasa ama mbunge wa kuteuliwa na Rais? Katiba yetu hairuhusu mgombea huru asiyetokana na chama cha kisiasa.

Mtu asiye mbunge anaweza kugombea uspika ila lazima atokane na chama chochote cha kisiasa.
 
Jiwe alilolikataa Mama kiguu anaenda kukutana na katika Mhimili unaoisimamia Serikali likiwa kama Spika wa Bunge, Lukuvi ni Mtu na Nusu
Kumbuka anayepitisha jina la Spika kwenye chama ni Mwenyekiti wa ccm taifa ambaye ndo huyu Rais.

Sasa kama Rais/mwenyekiti hakubaliani na jina hilo unadhani atapitishwa? Lahasha.
 
Kabudi hafai kabisa aende akale hela walizohongwa za Makinikia; mpaka leo hatujui hatma yake!
Hiyo kazi ya Spika wampe Chenge kama wanataka bunge liheshimiwe.
Kwanini umeamua kuwakosea Watanzania kiasi hiki? Yaani kashfa zote za kifisadi alizohusishwa Chenge bado unapendekeza awe Spika?

Hii nchi acha ccm waendelee kuitawala tu. Chenge alikiri hadharani kwamba pesa alizoiba ni vijisent tu halafu leo awe Spika kweli?
 
Kampeni za majitaka na kuchafuana zimeanza, hii ni kutaka kumchafua Spika wetu mtarajiwa!. Fitna hii imefeli kabla haijaanza.
P
Hilo jina si mpaka mwenyekiti wa ccm taifa aridhie ndo lipite? Kwa mamlaka aliyonayo mwenyekiti wa ccm taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna wakupinga anapoamua iwe hivyo.

Nadhani umeona shinikizo alilopata Ndugai hadi kujiuzulu kutoka kwa wabunge na wana ccm kila kona ya nchi.

Hakuna mwana ccm atakayethubutu kuwa uoande mwingine hadharani dhidi ya Rais. Hata maswahiba wa Ndugai walimkana wakawa uoande wa Rais. Acha kujidanganya mkuu.
 
Nimeangalia kwa mbaali saana naona mama kamuacha Lukuvi kwenye uwaziri ili akagombee uspika wa bunge kufuatia kujiuzulu kwa uncle Ayubi Ndugai.

Lukuvi ana experience kubwa sana kwenye mambo ya bunge ni mbunge mkongwe na mwanaccm kindaki ndaki hajaachwa kwa bahati mbaya.

Hakuna mwanaccm ndani ya bunge kwa Sasa atakae mshinda Lukuvi wakipambana kwenye sanduku la kura kwa wabunge wa Ccm

Karibu Willium Vaghing'embe Lukuvi mbunge wa Isimani kua spika mpya wa bunge Letu
Hata mimi nilitabiri hivi. Jamaa yuko very competent kwenye siasa za Tanzania
 
Nimeangalia kwa mbaali saana naona mama kamuacha Lukuvi kwenye uwaziri ili akagombee uspika wa bunge kufuatia kujiuzulu kwa uncle Ayubi Ndugai.

Lukuvi ana experience kubwa sana kwenye mambo ya bunge ni mbunge mkongwe na mwanaccm kindaki ndaki hajaachwa kwa bahati mbaya.

Hakuna mwanaccm ndani ya bunge kwa Sasa atakae mshinda Lukuvi wakipambana kwenye sanduku la kura kwa wabunge wa Ccm

Karibu Willium Vaghing'embe Lukuvi mbunge wa Isimani kua spika mpya wa bunge Letu
Kumbe anaitwa Ayubi Ndugai...!
 
Waste not your time waheshimiwa.
Hon. SPEAKER tayari amekwisha tayarishwa
mbona hamtaki kusikiliza nyimboooo
CCM INA WENYEWE..
Kama siyo kupewa ugaidi,Mbowe alikuwa the right person,kesho ndiyo tomorrow tunyanyuwe mikono juu tumuombee atoke.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Sasa ili uwe mbunge si lazima utokane na chama cha siasa ama mbunge wa kuteuliwa na Rais? Katiba yetu hairuhusu mgombea huru asiyetokana na chama cha kisiasa.

Mtu asiye mbunge anaweza kugombea uspika ila lazima atokane na chama chochote cha kisiasa.
Unajibu kwa utashi wako au kutumia vifungu vya katiba ?

Ebu kasome tena, sifa za mtu kuwa spika wa bunge la Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ili uwe mbunge si lazima utokane na chama cha siasa ama mbunge wa kuteuliwa na Rais? Katiba yetu hairuhusu mgombea huru asiyetokana na chama cha kisiasa.

Mtu asiye mbunge anaweza kugombea uspika ila lazima atokane na chama chochote cha kisiasa.
KATIBA YA NCHI YAKO INASEMA

(1) Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na
Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au
wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge
na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje
ya Bunge.
(2) Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya aina
nyingine yoyote itakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa
madhumuni ya ibdara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Spika.
(3) Mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Spika atatakiwa, kabla
ya kumaliza siku kumi na tano tangu kuchaguliwa kwake,
kuwasilisha kwa Rais tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za
uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya aya ya (d) ya ibara ndogo ya
(2) ya ibara ya 67. Tamko hilo litatolewa kwa kutumia fomu
maalum itakayowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watu ndivyo wanatafutaga madaraka. Huyu lukuvi ex std seven anataka kua speaker. Hata kama kajiendeleza kielimu hana darasa linajulikana zaidi ya kua na vyeti feki. Uspika tunahitaji japo elimu ya chuo kikuu. Kuna naibu speaker msomi sijui wanahangaka nini. Kama ni mtu mwingine mzee kabudi apewe hiyo nafasi sio hawa watu wa madili.
Lukuvi licha ya kushika nafasi kubwa wanataka wao tu waongoze milele.
Binafsi ningeshauri hiyo nafasi apewe kabudi ili nchi iweze kuendelea kunufaika na weledi wake kwenye sheria na uzalendo wake kwa taifa.
Huyo Kabudi na elimu yake ameifanyia nini Tz ukilinganisha na Lukuvi?

Kabudi katuharibia mahusiano ya kimataifa,muongo na mtu wa kuabudu watawala. Kama elimu ndio inamfanya mtu awe mjinga hivi basi bora Lukuvi alietufaa sana kwa nafasi za uwaziri.

Kusoma na kuelimika ni vitu viwili tofauti sana,unaweza kuelimika bila ata ya kuingia darasani,tunahitaji walioelimika sio waliohudhuria darasani na kuwa wapumbavu walamba viatu.
 
NI tayari imeamzia usiku wa saa 7 (00:01am) na alipomalizia kiwaona wamiliki wa mahotel km A Shabiby na FM wa Bambalaga iliyopo viwanja vya Lukuvi Njedengwa huo NI ukweli
lkn Lukuvi hafai mwambieni Azan Zungu ana weledi na sio STD 7
Katika CCM Hakuna anayefaa kwa chochote.
 
Hahaha hata katibu tarafa lazima ukohoe itakuwa hicho cheo ambacho unaweza ukaachiwa kiti cha Rais kwa dharura?

Tusubiri tuone kwa nchi zetu mpaka unakopa kwa lengo la kurudisha ukipita na usipopita unauza ulivyopiga mwanzo
Hajafika kwa Babu akapata kikombe cha uji?
 
Kabudi hafai kabisa aende akale hela walizohongwa za Makinikia; mpaka leo hatujui hatma yake!
Hiyo kazi ya Spika wampe Chenge kama wanataka bunge liheshimiwe.
Huyu mzee wa vijisenti?
 
Back
Top Bottom