"BURIANI WILLIAM MALECELA".
Nakumbuka Mara ya Mwisho kuwasiliana na William Malecela "Le Mutuz" ilikuwa Ni Tarehe 14 February 2023, 8:14 Mchana(Valentine Day).
William alinicheki personally Baada ya Kusoma Posti niliyoandika hapa Siku hiyo ya Valentine nikielezea kuhusu namna gani Fedha ni kila kitu ktk "Material World"Lakini si kila kitu katika "Ulimwengu wa Kiroho"....nilielezea Mfano wa Bilionea Michelle Ferro aliyekuwa Mmiliki wa Kiwanda kikubwa Cha Chocolate Duniani Cha Nutella na Utajiri wa Dollar Bilioni 20 Lakini akafariki Feb 14 Mwaka 2015 ktk Siku ya Valentine ambayo alijiandaa pia kusheherekea.
Lemutuz aliponicheki akaniambia Ujumbe huu ulimgusa na aliupenda, akaniomba Ku-share na Watu Wengi zaidi kwenye Platform zake ikiwemo Instagram.....Aka-share na ameondoka akiuacha pale Instagram ukiwa umewafikia Watu Wengi zaidi kuliko hata vile Ambavyo ningeusambaza Mimi...He was the King of Social Media...Le Mutuz kwa namna ya Maisha yake ya Kujichanganya na kila Mtu aidha Mkubwa au Mdogo kwake ali-share Material zozote Online au Offline za Mtu yeyote ambazo Ni Positive with "Facts".
Ni dhahiri pia William alitambua Kuwa pamoja na Maisha ya Dunia Lakini Mungu aliye Mkuu wa Vyote atavuna kila kiumbe ktk Dunia hii pale aonapo inastahili bila kujali Status ya kiumbe hicho kijamii au kiuchumi, naamini William pia amelala Mahali pema with a positive Mentality iliyoamini Kuwa Dunia yetu hii Ni Mahali pa Kupita na ipo Siku atatwaliwa.
Nitamkumbuka LeMutuz Kama Mtu Aliyekuwa akijiamini, Mtu Real ambaye aliyaishi Maisha yake ayapendayo Bila Woga, asiye Mbinafsi na Aliyekuwa Tayari ku-appreciate Watu Wengine na hata Kusaidia pale alipoweza, Pumzika kwa Amani Mzee wa Downtown, Mbele yetu Nyuma yako Until we Meet Again, Boma Liwanza🤝🙏
Nesi mkunga